Mahitaji ya udugu kati ya Manabii

  • | Sunday, 22 October, 2017
Mahitaji ya udugu kati ya Manabii

     Kwa kuwa uhusiano wa udugu ni nguvu zaidi katika husiano za kibinadamu baina ya watu, basi Mtume (SAW) amesifu uhusiano wa mapenzi, upendo, heshima baina ya Manabii wote kwa "udugu", imesimuliwa Kutoka kwa Abu Hurayrah kwamba Mtume amesema: "Mimi ndiye mwenye haki zaidi kwa ‘Issa mwana wa Maryam kuliko yeyote mwingine duniani na akhera" wakasema: vipi Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?, akasema "Manabii ni wadugu kwa upande wa baba, mama zao tofauti, lakini dini yao ni moja, kwani hakuja Mtume baina yake na mimi[1].

Basi Hadithi hiyo imeonyesha uhusiano wa kiina kati ya Mtume wetu Mohammad, (S.A.W) na Manabii wote kwa ujumla, na hasa kati ya Isa bin Mariamu.

Na taarifa hiyo ya Nabii, inawafahamisha waumini umuhimu wa kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya watu wa dini mbili katika nyanja mbali mbali za ushirikiano ambao wanaweza kushirikiana, kama yafuatayo:

Kuishiana pamoja katika amani:

Kuishiana pamoja katika amani pamoja na mwingine ni thamani ya Kiislamu; kwa kuwa Qur'ani ilikuja ili kutangaza kwa watu kwamba dini ya Manabii wote ni moja, kwa hiyo inalingania umoja baina ya watu -hata ikihitilafiana sheria zao- kwa kuzingatia kwamba wananasibishwa kwa asili moja. Kwa hiyo, ulinganio wa Uislamu Unategemea umoja na ushikamano wa kibinadamu kwa manufaa ya wanadamu wote, kufuatia kauli ya Mwenyezi Mungu: {Kwa yakini huu umma wenu ni umma mmoja, na Mimi ni Mola wenu, kwa hivyo Niabuduni}, [Al-Anbiyaa: 92}.

Na kwa ajili ya kutekeleza mawasiliano hayo kati ya wanadamu kupitia zama, umekuja sheria ya Uislamu ikibeba risala ya kiulimwengu inayoafikiana na maumbile ya watu wote mahali popote, hivyo madhumuni ya Uislamu ni huruma na amani inayowajumuisha watu wote, Mwenyezi Mungu akasema: {Nasi hatukukutuma, ila uwe rehema kwa walimwengu}, [Al-Anbiyaa: 107].

Na Amesema pia: {Enyi mlioamini! Ingieni katika hukumu za Uislamu zote, ·wala msifuate nyayo za Shetani; kwa hakika. yeye kwenu ni adui dhahiri}, [Al-Baqarah: 208].

Aya hiyo inawazungumzia waumini ili washikamane na kuishiana pamoja katika amani, na ili waanze mazungumzo na wengine. Na kutokana na hayo, Mtume (S.A.W) Amekiri msingi wa mazungumzo ya kidini bila ya kujali matokeo yake, na Ametekeleza hayo katika barua Alizoziandika kwa wafalme na maraisi ili kubainisha maana ya Uislamu, na miongoni mwa mifano ya mazungumzo na kukutana; ni barua yake kwa Heraclius mfalme wa Urumi, mojawapo ya mamlaka mawili makubwa wakati huo -mwaka wa saba H- basi akamtuma mjumbe akiwa na kitabu kinachoeleza dini ya Uislamu anayoilingania, na ili afungue mazungumzo, basi ameandika ndani yake:

"Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu, ‎kutoka Mohammad, Mtume wa Mwenyezi Mungu, kwa Heraclius ‎mfalme wa Urumi. Amani iwe juu ya anayefuata uongofu. Ama baada, ‎nakulingania kujiunga na Uislamu. ufuate Uislamu ili upate amani; na ‎Mwenyezi Mungu atakupa malipo yako mema marudufu, ukikataa ‎utapata madhambi ya kutoamini raia yako", Mwenyezi Mungu amesema: {Enyi watu wa Kitabu! Njooni kwenye neno lilio sawa baina yetu na nyinyi: Ya kwamba tusimuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe na chochote; wala tusifanyane sisi kwa sisi kuwa Waola Walezi badala ya Mwenyezi Mungu. Na wakigeuka basi semeni: Shuhudieni ya kwamba sisi ni Waislamu}, [Al-Imran: 64].

Na kwa kuchunguza ujumbe huo tunauona kwamba unabeba misingi ya mazungumzo katika mbinu wa kiislamu, kama vile:

A: "Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu, kutoka Mohammad Mtume wa Mwenyezi Mungu": ibara hiyo imeonyesha unyenyekevu wa Mtume (S.A.W), kwani ingawa Mtume (S.A.W) anabeba Wahyi wa Mwenyezi Mungu kwa walimwengu wote, lakini ametaja jina lake tu isipokuwa kutoka sifa ya unabii, -Mtume- ili kufikisha amani katika nafsi ya mfalme ujumbe, akianza kwa anuani ya ujumbe wa Uislamu, inayosema kwamba imekuja kutoka Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu.

"kwa Hercules Mkubwa wa Urumi", kwa ibara hiyo Mtume (S.A.W) anawapa watu cheo chao, na hii miongoni mwa heshima ya Nabii, na kutoka heshima ya mazungumzo, ingawa Mtume (SAW) ni mwenye daraja kubwa zaidi kwa tabia ya unabii, Lakini alimwambia Hercules kwa daraja yake ndani ya watu wake "Mkubwa wa Urumi", jambo ambalo ni sawa na tabia  nzuri na upole katika mazungumzo yake Mtume (SAW), na hii ni mafundisho muhimu kwa mlinganiaji anayewaita wasio waislamu wafuate mwislamu, yaani anawapa watu heshima yao  na awazungumzie kwa ulaini.

c. "Amani iwe juu ya anayefuata uongofu": ni ibara inayoafikiana na muktadha ya mazungumzo ya ulinganio wa kufuata Uislamu, kwa hivyo amani katika hotuba ya kiislamu ni anuani ya mazungumzo na asiye mwislamu, nayo ni Sunnah inayofatiwa na manabii, kwa mfano Musa na Haruni (A.S) walianza kwa sentensi hiyo katika mazungumzo yao pamoja na Firauni walipokuwa wanamwita kwa kumpwekesha na kunyenyekea kwa Mwenyezi Mungu, na Qurani Tukufu ilitaja mazungumzo hayo ya Musa katika aya isimayo: {Mwambieni maneno laini, huenda akazingatia au akaogopa}, [Taha: 44]. Na katika kauli yake mtukufu: {Sisi tumekuletea ishara itokayo kwa Mola wako Mlezi. Na amani itakuwa juu ya aliyefuata uwongofu}, [Taha: 47].

Kwa hiyo, thamani ya amani inafungamana na mazungumzo pamoja na asiye Mwislamu katika lugha ya Qurani Tukufu, jambo linaloonyesha kwamba ni mfumo wa unabii, na kwamba waislamu ni lazima wautekeleza kisheria.

D. "nakulingania kujiunga na Uislamu. ufuate Uislamu ili upate amani": ibara hii inasisitiza mbinu unaotegemewa katika ulinganiaji wa Uislamu, nao mbinu wa kuwapa amani kwa wanaolinganiwa kujiunga na dini takatifu, sawa wamekubali kujiunga nayo au wamekataa kufanya hivyo, lakini madamu hawakutangaza vita, Kufuatia kauli yake Mtukufu: {Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu}, [Al-Mumtahnah: 8].

 E. "ukikataa ‎utapata madhambi ya kutoamini raia yako"  ibara hiyo inasisitiza msingi wa uwazi katika mazungumzo ya kueleza Uislamu, basi mwingine akikubali, atapata malipo yake na malipo ya atakayemfuata kwa kukubali Uislamu kutoka watu wake, na kama hatakubali, basi atahesabiwa kufuatia aliyechagua, kwa mujibu wa kauli ya Mwenyezi Mungu: {Na wakigeuka basi semeni: Shuhudieni ya kwamba sisi ni Waislamu}, [Al-Imran: 64].

Huo ni msingi uliowekwa na Mtume (S.A.W) katika ulinganio wake kwa Uislamu, nayo ni kumwacha anayekataa kwani atahesabiwa na Mwenyezi Mungu, Mtume (S.A.W) ametekeleza hayo juu ya wenyeji wa Makkah, katika siku ya ushindi aliposema: "Nendeni, nyinyi ni wahuru",([2]) na hakuwalazimisha kufuata Uislamu, ingawa ulikuwa msingi wa tatizo kati yao, lakini Mtume (S.A.W) hakutumia udhaifu wao ili awalazimishe kufuata Uislamu, bali amewaacha huru, kwa sababu hiyo Mwenyezi Mungu amewapa ushindi nchini Makkah, basi watu wakaingia katika dini ya Mwenyezi Mungu makundi makundi.

 

[1]( Sahih Muslim (4\1837)

[2]( Ibn Hishaam (2\407).

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.