Dalili na hoja zinazozuia kumkafirisha mwislamu (3)

  • | Wednesday, 1 November, 2017
Dalili na hoja zinazozuia kumkafirisha mwislamu (3)

     Wanachuoni wengi wamelizungumzia suala la kumkufurisha mwislamu, kutokana na umuhimu na cheo hatari katika historia na mawazo ya kiislamu kupitia historia ya kiislamu, na mifano ya wanachuoni hao ni yafuatayo:
Kwanza: imamu Al-Ghazali katika kitabu cha "Faysal Al-Tafrikah" amesema: "ama wasia: ni kuhifadhi ulimi wako usiwakufurisha waislamu "ahlul-Qiblah" kadiri iwezekanavyo, madamu wanasema "hakuna Mungu anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu bila ya kufanya kinyume cha kauli hii, na kufanya kinyume kunamaanisha kuhalalisha kusema uongo na kukunasibisha kwa Mtume kwa sababu au bila sababu; kwani kukufurisha kuna hatari, ama kunyamaza, basi hakuna".
Pili: imamu ibn Taymiyah katika kitabu cha "Majmuul-Fatawah" amesema: "hakuna anaye haki ya kumkufurisha mmoja wa waislamu- hata akikosea- mpaka anajadiliwa kwa hoja, na mpaka haki iwe wazi mbele yake, na mtu ambaye imani yake imehakikishwa kwa yakini, basi imani yake haiondoshwi kwa shaka".
Tatu: imamu Al-Ashaari katika makala za "Al-Islamiin wa Ikhtilaaf AL-Musaliin" anasema: "watu wamehitilafiana baada ya Mtume wao katika vitu vingi, baadhi yao wamewapoteza baadhi nyingine, na baadhi yao wamejiweka mbali na baadhi nyingine; basi wakawa makundi kadhaa, vyama mbalimbali, lakini Uislamu bado Unawakusanya na kuwajumuisha".
Nne: Sheikh wa Al-Azhar profesa Ahmad Al-Tayyib, akazungumzia rai ya imamu Al-Ashaari, amesema: "na hii ni rai ambayo kila wanachuoni ni lazima ashughulike nayo, anapoangalia hali ya waislamu ambao wakawa makundi na vyama vingi".
Na madhehebu ya Al-Ashaari na wanaomwunga mkono rai yao miongoni mwa Ahlul-Sunnah wamechangia kwa nguvu katika kuhifadhi damu ya wana wa umma, kulinda heshima yao na kuhuisha utamaduni wa aya isimayo: {Shikamana na kusamehe, na amrisha mema, na jitenge na majaahili}, [Al-A’raaf:199], na utamaduni wa hadithi isimayo: "mwislamu ni yule ambaye waislamu wanaosalimika kutoka ulimi wake na mkono wake" ….


D. Abdelminiim foad

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.