Kuhusu istilahi ya "Waliopotea"

  • | Saturday, 4 November, 2017
Kuhusu istilahi ya "Waliopotea"

     Kuhusu istilahi ya "Waliopotea" katika kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{Siyo ya waliokasirikiwa, wala waliopotea}, [Al-Fatihah:7].
Ilhali istilahi ya "waliopotea" iliyotajwa katika sura ya Al-Fatihah imechochea majadiliano mengi baina ya wataalamu wasiohusika, jambo lililoitolea istilahi hiyo mbali na asili yake katika lugha na kuihusisha kwa maana moja tu, ilikuwa ni lazima kuonyesha suala hilo kwa pande zake zote kupitia uwingi wa maana ya kilugha na kadhalika maana yake ya kiistilahi kwa mujibu wa muktadha wa lafudhi katika aya za Qurani Tukufu. Na kueleza suala hilo kunahitaji kufuata misingi ifuatayo:
1.    Mahali pa kutumia istilahi hiyo katika Qurani tukufu.
2.    Athari zinazotokana na kutumia istilahi hiyo.
Kwanza: Mahali pa kutumia istilahi hiyo katika Qurani
Tukufu.‎
Hakika istilahi ya "upotofu" na yanayonyambuliwa nayo imekuja katika aya nyingi, na  miongoni mwake:
1.    Kauli yake Mtukufu: {Si vibaya kwenu kuitafuta fadhila ya Mola wenu Mlezi Na mtakapomiminika kutoka A'rafat mtajeni Mwenyezi Mungu penye Masha'ril Haram. Na mkumbukeni kama alivyo kuongoeni, ijapokuwa zamani mlikuwa miongoni mwa waliopotea}[Al-Baqarah:198], na maana katika aya hii: (ijapokuwa kabla ya uongofu na Uislamu mlikuwa miongoni mwa wajinga, hamjui vipi mnataja majina ya Mwenyezi Mungu na namna ya kumwabudu.
2.    Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Alipouona mwezi unachomoza alisema: Huyu ndiye Mola Mlezi wangu  ulipotua akasema: Kama Mola Mlezi wangu hakuniongoa, nitakuwa katika kaumu waliopotea [Al-Anaam:77].
3.    Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: ‎{akasema: nilitenda hayo hapo nilipokuwa miongoni mwa wale waliopotea} [Ashuaraa:20] na maana: (nimeua nafsi hii niliyoiua na mimi ni miongoni mwa waliopotea). Yaani nilikuwa mjinga kabla ya kunijia kutoka kwa Mwenyezi Mungu Wahyi inayoharamisha kumwua mtu huyo. Na Waarabu wanatumia neno la "upotofu" badala ya "ujinga", na "ujinga" badala ya "upotofu" na maneno hayo mawili yanatumika kwa maana moja.
4.    Na kutoka maana hiyo hiyo, imekuja kauli yake Mtukufu: {Naapa kwa nyota inapotua, Mwenzenu huyu hakupotea, wala hakukosea} [Annajm:1,2] na maana ya aya hii: kuwa Mwenyezi
Mungu Amemhifadhi Mtume wake kutoka kwenda kinyume cha haki sawa sawa akiwa anakusudia au hakusudii; kwani maana ya upotovu ni: kwenda kinyume cha haki kwa makusudi, na kukosea kwenda kinyume cha haki bila ya kukusudia, na hakika Mwenyezi Mungu Amemhifadhi Nabii wake kutoka mambo hayo mawili. Na kutoka hayo imekuja kauli ya Mwenyezi Mungu: {Tuongoe njia iliyonyooka, Njia ya uliowaneemesha, siyo ya waliokasirikiwa, wala waliopotea.} [Al-Fatihah:6,7].
Na maana ni kuwa: Mwenyezi Mungu Aliwaongoza waislamu kuomba uwongofu ambao Aliwafanya watu wema waifikie, na kuwazuia (waliokasirikiwa) wasiifikie, nao ni waliokataa kukubali haki baada ya kuijua, na (waliopotea) ni ambao hawakufika haki bila makusudio.
Na kufuatia yaliyopita, basi yeyote anayekosea kufikia haki basi ni mpotovu hata akiwa mwislamu, Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake basi hakika amepotea upotofu uliowazi.} [Alahzab:36].
Hivyo, maneno na vitendo zinazoziba ukweli kama uongo, khiana, dhuluma, na kumshirikisha mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu ni miongoni mwa upotovu, na inayodhihirisha hayo ni muktadha wa Qurani kwa istilahi ya upotovu.

Pili: Athari zinazotokana na kutumia istilahi hiyo.

Hakika sheria ya Uislamu imezingatia uwiano katika mahusiano kati ya Waislamu wenyewe, na kati ya Waislamu na wengine, na inayojulikana kisheria kuwa wema wa mwanadamu ni jambo linalomrejea kwa manufaa, na kwamba upotovu wake ni jambo linalomrejea kwa dhambi na hupepa pekee matokeo yake Siku ya mwisho, kuna haki kwa M.Mungu na haki kwa jamii, haki ya M.Mungu uhasibu wake kwa Mwenyezi Mungu tu, ama kuhusu haki za jamii, jamii yenyewe ndiyo inayohasibu juu ya kaki zake bila ya kujali imani za mwanadamu, Qurani Tukufu imethibitisha maana hii kwa kauli ya M.Mungu Mtukufu: Sema: {Enyi watu! Haki imekwisha kukujieni kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Basi anaye ongoka anaongoka kwa faida ya nafsi yake, na anaye potea anapotea kwa khasara ya nafsi yake. Na mimi si mwakilishi juu yenu}[Yunus: 108].
Na kulingana yaliyopita, kuwa sifa ya upotovu hutolewa kwa wale wasioongozwa kwa haki, sawa akiwa Mwislamu au asiye Mwislamu, Hiyo haihusiani na taifa fulani, hasa kuwa Qur'ani Tukufu imehotubia kwa huruma watu wa Kitabu na kuamuru kuwafanyia wema, Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu.} [AL - Mumtahina: 8].
Na kwa kuwa kuishi pamoja kwa amani kati ya watu binafsi ni suala la kidini kabla ya kuwa la kitaifa, Mtume (S.A.W) amesema: "Ye yote anayemwua anayeahidiwa hakuoni harufu ya peponi, na kuwa harufu yake inanuswa tangu miaka arobaini".
Hitimisho: kuwa Mwislamu anaamuriwa kujitahidi kufikia haki na kuepuka yote yanayokasirikia Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa mujibu wa dua iliyomo katika mama ya kitabu "Al-Fatiha" katika kauli yake Mtukufu: {Tuongoe njia iliyo nyooka,  Njia ya ulio waneemesha, siyo ya walio kasirikiwa, wala walio potea} [AL - Fatiha: 6, 7].  
Nayo ni dua inayoradidiwa na mamilioni ya Waislamu kwa siku mara makumi. Je, dua hiyo inafanya uchochezi dhidi ya wengine, au kupungua haki za washirika wa taifa?
Vile vile, Mwislamu anapaswa kuepuka kuwashawishi wengine ili isipeleke majibu mabaya, na Qurani ime mwelekeo huu kwa ajili ya kufungwa kwa mlango wa mgongano, Allah Amesema: {Wala msiwatukane hao wanao waomba badala ya Mwenyezi Mungu, wasije na wao wakamtukana Mwenyezi Mungu kwa jeuri bila ya kujua. Namna hivyo tumewapambia kila umma vitendo vyao. Kisha marejeo yao yatakuwa kwa Mola wao Mlezi, naye atawaambia waliyo kuwa wakiyatenda} [AL- Annam: 108].

Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na Fikira Kali
Kitengo cha Lugha za Kiafrika

 

Print
Tags:
Rate this article:
5.0

Please login or register to post comments.