Kuchocheza kuwaua watu kwa kutumia ufahamu usio sahihi wa baadhi ya aya za Qurani na hadithi za Mtume

  • | Monday, 27 November, 2017
Kuchocheza kuwaua watu kwa kutumia ufahamu usio sahihi wa baadhi ya aya za Qurani na hadithi za Mtume

     Moja wa makala za kundi la kigaidi inazungumza kuhusu vitendo na mafanikio ya kundi la Daesh yaliyofanywa na wanamgambo wake katika nchi kadhaa za Ulaya na majaribio yake ya kutumia hujuma hizo katika kuwahimiza ari ya wanamgambo wake ambao bado hawakushiriki katika mashambulizi ya kujitoa muhanga. Na pia wanatumia vitendo vya kigaidi katika kusambaza na kuzungumzia mapato yao na kusifu vitendo vyao kama ni mifululizo inayofungamana, na kila shambulizi ni sehemu ya mfululizo huo, na wakidai kwamba wao wanalenga kwa mashambulizi hayo ulimwengu mzima na kwamba wao wana wasaidizi nchini kote za Ulaya na zisizo za Ulaya ambao bado wanangoja ishara ya kuanza. Wanayafanya hayo yote kwa ajili ya kueneza hofu nyoyoni mwa wananchi na serekali ambayo kwa maoni ya kundi hilo ni makafiri.
Na wanataja waliyoyafanya katika kipindi cha maandalizi na anasimulia namna ya kutekeleza mashambulizi, wakilingana baina ya vitendo vyao na msimamo wa Mtume (S.A.W) kuhusu washirikina wa Makkah wakati wa kuhama "Hijrah" na vipi Mwenyezi Mungu Amemsaidia na kumwunga mkono, wakitoa dalili ya Mwenyezi Mungu: {Yasiin}: )Tumeweka kizuizi mbele yao, na kizuizi nyuma yao, na tumewafunika macho yao; kwa hivyo hawaoni(. Na bado mwandishi anaendelea kutukuza suala la Jihad na kulihimizia, pia akitumani kuwa wanamgambo wa Daesh huko Ujerumani wakifanya mashambulizi yawapa makafiri madhara kubwa. Na anatilia mkazo kwamba waislamu watajua baadaye kwamba Mwenyezi Mungu amefaradhisha juu yao kuwapiga vita makafiri mpaka wafuate Uislamu au wanakufa kwa fedheha yao. Na anataja baadhi ya aya na hadithi katika makala yao:
•    )Na piganeni na washirikina wote kama wao wnavyopigana nanyi nyote. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu yu pamoja na wachamngu(. {Al-Twabah:36}.
•    )Na wauweni popote mwakutapo(. {Al-Baqarah:191}.
•    )Na piganeni nao mpaka pasiwepo fitina(. {Al-Baqarah:193}.
Na sisi tunaweza kuzijibu rai zao kupitia kusahihisha dhana ya vita kama yafuatayo.
Ufahamu sahihi kwa maana ya aya za kupigana vita "Jihaad" katika Qurani tukufu
Kwanza ni lazima tujue kwamba:
1.    Asili ya Uislamu ni kuwaita watu waelekee kwenye njia ya Mwenyezi Mungu kwa hekima na mawaidha mema bila ya kuwalazimisha au kuwaogopesha.
2.    Kupigana vita katika Uislamu kumefaradhishwa kwa ajili ya kuzuia uadui na dhuluma.
3.    Kufahamu sahihi kwa maana ya aya za kupigana vita katika Qurani tukufu.
4.    Tabia za Uislamu ndani ya uwanja wa vita.
Kwanza: Asili ya Uislamu ni kuwaita watu waelekee kwenye njia ya Mwenyezi Mungu kwa hekima na mawaidha mema, bila ya ulazimisho au kuwaogopesha.
Mtume (S.A.W) ameendelea kuwaita wasio waislamu kufuata Uislamu katika Makkah tangu mwaka wa 610 B.K- mpaka mwaka wa 622 B.K kwa hekima na mawaidha mema, bila ya kuteremshwa aya moja inayomwamuru kupigana vita "Jihad" katika kipindi hicho, ingawa washirikina walikuwa wanapinga Da’wah yake na wanamdhuru yeye na maswahaba wake, bali wakaamuru wajinga wao wampige Mtume kwa mawe, licha ya hayo yote Mtume (S.A.W) hakuamrishwa kuwapiga vita, bali ameamrishwa  kuvumilia  madhara yao kama yaliyokuja katika Qurani, Mwenyezi Mungu Anasema: (Na ingojee hukumu ya Mola wako Mlezi. Kwani wewe hakika uko mbele ya macho yetu, na mtakase kwa kumsifu Mola wako Mlezi unaposimama), {Al-Tuur:48}.
•    Na kauli yake: )Basi wewe yatangaze uliyoamrishwa, na jitenge na washirikina(, {Al-Hijr:94}.
Na hata walipokuwa wanamshutumu Mtume, Wahyi ilikuwa inateremshwa kwa kusema: (Sisi tunajua kabisa wayasemayo. Wala wewe si mwenye kuwatawalia kwa ujabari. Basi mkumbushe kwa Qur'ani anayeliogopa onyo). {Qaaf:45}.
Na wakati madhara yalipozidi na waislamu waliadhibiwa ili wauache Uislamu, imekuja amri ya kuwasamehe, Mwenyezi Mungu Anasema: (Waambie walioamini wawasamehe wale wasiozitaraji siku za Mwenyezi Mungu, ili awalipe kwa waliyokuwa wakiyachuma). {Al-Jathiyah:14}.
Aya hizo zinaonyesha kwamba Mtume Amepambana na akili mbaya ya washirikina kwa kusubiri na kuvumilia na kwa kauli iliyo nzuri kupitia miaka 13, jambo linaloashiria kwamba asili ya Uislamu ni kungoja na kufuata mbinu zote za kiamani wakati wa kupambana na adui, hata aya za "Jihadi" iliyoteremshwa katika kipindi hicho nchini Makkah ilikuwa inamwamuru Mtume awapigane kwa kauli, hoja na dalili, Mwenyezi Mungu Anasema: )Basi usiwat'ii makafiri. Na pambana nao kwayo kwa Jihadi kubwa(. {Al-Furkaan:52}. Na Ibn Kathiir amesema katika tafsiri yake kwamba neno la "Na pambana nao kwayo(, yaani pambana kwa Qurani ambayo ni jihadi ya hoja na dalili.
Na kwamba kuwaita watu wafuate Uislamu haifai kutekelezwa kwa nguvu na kwa mujibu wa aya za Qurani zinazosema:
Mwenyezi Mungu anasema: )Je, wewe utawalazimisha watu kwa nguvu mpaka wawe Waumini?(. {Yunus:99}.
Hii ni aya wazi inayokataza kuwatisha watu na kuwalazimisha kufuata Uislamu.
Pili: vita na Jihad katika Uislamu vimefaradhishwa kwa ajili ya kuzuia uadui na dhuluma.
Hakika kupigania vita katika Uislamu kumefaradhishwa kwa ajili ya kuzuia uadui au kujibu mashambulizi. Na haki ya kulinda nafsi ni haki asili iliyokiriwa na sheria za mbinguni, na wakati washirikina walipomtazama Mtume ili wamwue kwa lengo la kuuangamiza Uislamu, aya ya kwanza ya Jihaad iliteremshwa kwa kuwapa waislamu ruhusa ya kupigana vita kwa ajili ya kulinda nafsi na dini, Mwenyezi Mungu Anasema: (Wameruhusiwa kupigana wale wanaopigwa vita kwa sababu wamedhulumiwa - na kwa yakini Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kuwasaidia(. {Al-Hajj:39}.
Ibn Abbas alisema kwamba aya hii ikateremshwa wakati Mtume na waislamu walipofukuzwa kutoka Makkah, ambapo Abu Bakr Al-Siddiiq alisema wakati huo "watu wamemfukuza Mtume wao! Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea. Mwenyezi Mungu atawaangamiza" Mwenyezi Mungu akasema: )Wameruhusiwa kupigana wale wanaopiganiwa vita kwa sababu wamedhulumiwa(. Abu Bakar akasema baada ya kusikia kwake aya hii "nimejua kwamba tutapigana vita".
Na hii inamaanisha kwamba Mtume (S.A.W) na waislamu walikuwa hawataki kupigana vita, bali wamelazimishwa ili kuondoa na kuzuia uadui na adhabu walizozipata kutoka washirikina wa Makkah, na hasa baada ya mkutano wa Makuraishi katika Dar Al-Nadwah na uamuzi wao wa kumwua Mtume (S.A.W). Hivyo akili na hekima zinawajibisha kuzuia uadui na kulinda nafsi ya Mtume wetu na kuzuia dhuluma, Mwenyezi Mungu Anasema: )Wameruhusiwa kupigana wale wanaopigwa vita kwa sababu wamedhulumiwa - na kwa yakini Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kuwasaidia. Wale ambao wametolewa majumbani mwao pasipo haki, ila kwa kuwa wanasema: Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu! Na lau kuwa Mwenyezi Mungu hawakingi watu kwa watu, basi hapana shaka zingelivunjwa nyumba za wat'awa, na makanisa, na masinagogi, na misikiti, ambamo ndani yake jina la Mwenyezi Mungu linatajwa kwa wingi. Na bila ya shaka Mwenyezi Mungu humsaidia yule anaye msaidia Yeye. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mtukufu.  Wale ambao tukiwapa madaraka katika nchi husimamisha Sala, na wakatoa Zaka, na wakaamrisha mema, na wakakataza mabaya. Na kwa Mwenyezi Mungu ndio marejeo ya mambo yote(.
Kwa hivyo lengo la kuhalalisha "Jihad" katika Uislamu ni kumnusuru  mnyonge, na kuwapa waumini madaraka ardhini, na sio kuwashambulia wasio waislamu.
Tatu: Ufahamu sahihi kwa maana ya aya za kupigana vita katika Qurani tukufu.
Suala la "Jihad" katika Qurani tukufu na hadithi za Mtume ni miongoni mwa masuala hatari, na makala hii inakuja kwa ajili ya kubainisha ufahamu sahihi kwa aya za Jihad, Mwenyezi Mungu Anasema: )Na wakivunja viapo vyao baada ya kuahidi kwao, na wakatukana Dini yenu, basi piganeni na waongozi wa ukafiri. Hakika hao hawana viapo vya kweli. Huenda (kwa hayo) wakaacha. Je, hamtapigana na watu walio vunja viapo vyao na wakawa na hamu ya kumfukuza Mtume, nao ndio waliokuanzeni mara ya kwanza? Je, mnawaogopa? Basi Mwenyezi Mungu anastahiki zaidi mumwogope, ikiwa nyinyi ni Waumini. Piganeni nao, Mwenyezi Mungu awaadhibu kwa mikono yenu, na awahizi na akunusuruni muwashinde, na avipoze vifua vya kaumu ya Waumini(. {Al-Tawbah:14}.
Amri ya kupigana vita katika aya zilizopita inakusudia watu waliovunja viapo vyao baada ya kuahidi kwao, na kuutukana dini ya Uislamu, na wakawafukuza waislamu nyumbani mwao, na wakamtazama Mtume ili kumwua. Na aya imekuja kwa kusema "piganeni" na sio "uweni" na hii inamaanisha kwamba amri ya kupiga vita imekuja kwa ajili ya kuzuia uadui, sio kwa ajili ya kuwaua.

Nne: Tabia za Uislamu ndani ya uwanja wa vita.
Sheria ya kiislamu haikuamuru kuishiana pamoja katika amani baina ya waislamu na wasio waislamu tu, bali imeweka dhamana za kutosha zinazopunguza kutokea vita na ole wake. Na kutoka sheria hizo ni:
1.    Kukataza kuanza vita pasipo na haki.
Hakika malengo ya kupigana vita katika Uislamu yenye thamani kubwa, kwa hivyo Uislamu hauamrisha kuanza vita kwa ajili ya kuiba mali, kujaalia wahuru wawe watumwa au kueneza uharibifu na ugaidi ardhini, bali umeamrisha kuanza vita ili kuhakikisha haki, na kuweka neno la Mwenyezi Mungu kuwa ndilo juu, kuzuia uadui, kulinda dini, nafsi, mali na heshima. Pia sheria ya kiislamu imeweka misingi kadhaa kwa ajili ya kuepuka madhara yanayozuka na kuvuka mipaka katika kujibu mashambulizi, amesema Mwenyezi Mungu mtukufu: )Mwezi mtakatifu kwa mwezi mtakatifu. Na vitu vitakatifu vimeekewa kisasi. Anayekushambulieni nanyi mshambulieni, kwa kadiri alivyokushambulieni. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu yu pamoja na wachamngu(, {albaqarah:194}.
Aya hiyo imesisitiza ulazimisho wa kuwashambulia maadui kwa kadiri walivyowashambulia waislamu, na aya hii ikibainika uharamu wa kuvuka mipaka katika kujibu mashambulizi, basi kuna aya nyingine zinaeleza maana hiyo hiyo, Amesema Mwenyezi Mungu mtukufu: )Na piganeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu na wale wanaokupigeni, wala msianze uadui. Kwani Mwenyezi Mungu hawapendi waanzao uadui(. {albaqarah:190}.
Hakika Uislamu unawahimiza waislamu kumaliza kwa haraka vita na migogoro wakati maadui wanapotaka kufanya suluhisho, Amesema Mwenyezi Mungu mtukufu: )Na wakielekea amani nawe pia elekea, na mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ndiye Mwenye kusikia Mwenye kujua(. {alanfal:61}. Na kauli yake: )wakielekea amani(, inamaanisha kwamba Mwenyezi Mungu anataka kulinda damu kuagiwa na kuimaliza migogoro, kwani vita  havibakishi wala havisazi.
2.    Kukataza kuua wanawake, watoto na makasisi:
Na miongoni mwa hadithi zilizokuja katika suala hilo:
Mtume (S.A.W) Alikasirika na hakukubali alipojua kwamba mwanamke mmoja aligunduliwa ameuliwa, imepokelewa toka kwa Sulayman Ibn Boraidah, toka kwa baba yake amesema: Mtume (S.A.W) alipomwakilisha mtu awe kiongozi wa jeshi au kikosi, alikuwa anamwusia kumcha Mwenyezi Mungu yeye na waislamu wanaokwenda naye, kisha anasema: )pigeni vita katika njia ya Mwenyezi Mungu, shambulieni wanaokushambulia tu, pigeni vita wala msivuke mipaka, wala msidanganyi, wala msiharibu miili ya waliokufa, wala msimwue mtoto mdogo(.
Na imepokelewa kutoka kwa Anas Ibn Malik, kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu Amesema: )nendeni kwa jina la Mwenyezi Mungu na kufuatia mila ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, wala msimwue mzee mkubwa, wala mtoto, wala mdogo, wala mwanamke, wala msivuke mpaka, na kusanyeni ngawira zetu, na suluhisheni na tendeni mema, hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wanaowatendea mema(.
Na imepokelewa kutoka kwa AL-Aswad Ibn soraiee: kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu Alipeleka kikosi siku ya vita ya Hunayn ili kupigana na washirikina, basi wakapigana nao mpaka wakawauwa watoto wao, walipomjia Mtume Akawaambia )kwa nini! mmewaua watoto hao"? Wakamjibu "kwa sababu wao ni wana wa washirikina", akasema je! Wabora wenu ni wana wa washirikina? naapa kwa yule ambaye nafsi ya Muhammad iko mkononi mwake hakuna nafsi ila anazaliwa kwa maumbile “Fitrah” abadilisha maumbile hayo(.
•    Pia Mtume (S.A.W) amekataza kuwauwa wanawake, watoto wakati wa vita.
•    Hitilafu katika itikadi haihalalisha  damu ya mwingine, kwa hivyo jibu la Mtume (S.A.W) lilikuwa wazi sana aliposema akiwazungumzia maswahaba "je, wabora wenu sio isipokuwa wana wa washirikina".
•    Suala la kukataza kuwauwa wanawake na watoto wasioshirikiana katika vita limeafikiwa na wote.
Mwishoni tunaweza kusema kwamba historia ya waislamu ni wazi sana, na Al-Azhar Al-Sharif inasisitiza kwamba vitendo vya makundi yenye misimamo mikali havihusiani chochote na Uislamu.

 

Print
Tags:
Rate this article:
5.0

Please login or register to post comments.