Daesh: Kuufanya urafiki na wasio waislamu ni kufuru

  • | Thursday, 30 November, 2017
Daesh: Kuufanya urafiki na wasio waislamu ni kufuru

     Kufanya urafiki na wasio waislamu hata wakiwa maadui haizingatiwi kuwa ukafiri bali ni uhalifu mkubwa ambao mtawala anaupitishia adhabu kwa ilivyomzuia haini asikhini tena, lakini haini huyo hubaki mwislamu na haijuzu kuhukumiwa kuwa mkafiri, na dalili inayounga mkono rai hii  ni hadithi iliyosimuliwa na Al-Bukhari kwamba Ali (R.A.) alisema: "Mtume (S.A.W.) alinituma mimi na Az-Zubaiyr na Al-Meqdad Bin Al-Aswad akisema: nendeeni mpaka kufika bustani la “Khakh”  ambapo mtakutana na mwanamke anayesafiri  anaye ujumbe basi chukueni ujumbe huo", akasema Ali "basi tukakwenda haraka haraka kwa farasi zetu mpaka tukafika bustani hilo tukakutana na yule mwanamke, tukamwambia utoe huu ujumbe, akasema: "sina ujumbe", tukasema: "utatoa ujumbe au tutakukagua! Basi akautolea kutoka nyewele zake, tukauletea Mtume (S.A.W.). Na yalikuwa uliomo ujumbe huo  ni: “kutoka Hatib Ibn Abi Baltaa kwa baadhi ya washirikina wa Makkah akiwaambia kuhusu baadhi ya habari za Mtume (S.A.W.), basi Mtume (S.A.W.) akasema: "Ewe Hatib! ni nini hayo?" Akasema Hatib: "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu usiwe na haraka, hakika mimi nilikuwa mgeni sikuwa mmoja wa watu wa Maquraiesh na waliohama nawe walikuwa na husiano za kifamiliya wanazitumia kuwalinda akraba na mali zao, basi nilitamani kuwa maadamu mimi sina unasaba kama huu nifanye tendo linalowafanya maqureshi wawalinde akraba zangu, na sikulifanya tendo hilo kutokana ukufuru au uritadi wangu, wala kwa sbabu ya kuridhi kwa ukafiri baada ya Uislamu”, basi Mtume (S.A.W) amesema: “amesema kweli”, Omar amesema : “ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu unipe ruhusa ya kukata kichwa cha mnafiki huyo”, akasema Mtume (S.A.W) "hapana kwani alishuhudia vita vya Badr Na nini kitakujuulisha pengine Mwenyezi Mungu Aliwatazamia wale waliopigana katika vita hivyo Akawaambia: fanyeni  mnachotaka, hakika mimi nimekuwaghufurieni. Basi Mtume (S.A.W) hakumwua wala hakusema kwamba Hatib Bin Abi Baltaa amrekufuru".
Ijapokuwa Mtume (S.A.W) hakumwua wala hakumkufurisha lakini  kuufanya urafiki na wasio waislamu ni uhalifu mkubwa ambao mtawala peke yake anayeweza kukadiria adhabu yake inayoweza kufikia kunyonga.

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.