Daesh: Kuipenda nchi na uwananchi sio kutoka Uislamu

  • | Wednesday, 6 December, 2017
Daesh: Kuipenda nchi na uwananchi sio kutoka Uislamu

     Hakika tukitafuta vizuri katika dini yetu tutakuta  kwamba Mtume (S.A.W) alielezea upendo wake kwa Makkah nchi yake wakati alipofukuzwa na wenyeji wake na akakwenda kuelekea mji wa Al-Madinah akisema: {Ewe Mwenyezi Mungu Mtukufu utupendeze mji wa Al-Madinah, kama tunavyopenda mji wa Makkah au zaidi}, kwa kiwango hicho Mtume (S.A.W) alipenda Makkah ambayo ni nchi yake, basi vipi wapiganaji wa Daesh wanadai kwamba kupenda nchi na kujinasibisha kwayo ni ukafiri baada ya kusoma hadithi hii wazi, lakini wao wanapooza kama wanavyopooza hukumu zote za dini hiyo nyepesi walioichafua kwa vitendo vyao?!
          Hakika sisi tuna mfano mzuri kwa Mtume Mohammad (S.A.W), ambapo alisema katika hadithi iliyopokelewa na Imamu Ahmad katika kitabu chake cha Al-Musnad aliyepokea kutoka kwa mwanamke aitwaye Fasilah kwamba alisema: "nimemsikia baba yangu anasema: nilimwuliza Mtume (S.A.W.), nikasema: {Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu je, ni ukabila kwamba mtu kuwapenda watu wake hasa? Akasema Mtume (S.A.W.): hapana, lakini ukabila ni kwamba mtu awanusuru watu na jamaa zake hata wakiwa madhalimu}, kwa hivyo upendi wa mwanadamu kwa nchi yake na wananchi si kitu kibaya, bali ni jambo zuri isipokuwa likapelekea kumsaidia mdhalimu hata akiwa ni miongoni mwa jamaa yetu.  

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.