Aibu za Kuvunja mipaka na Kufuata misimamo mikali

  • | Saturday, 9 December, 2017
Aibu za Kuvunja mipaka na Kufuata misimamo mikali

     Kwanza: kuvuka mipaka na kufuata misimamo mikali kunapingana na misingi ya usamehevu na wepesi ambazo sheria ya kiislamu ilijengwa juu yake. Mtume (S.A.W) Alisema: "rahisishieni wala msifanye ugumu".
Pili: kuvuka mipaka na kufuata misimamo mikali husababisha mashaka . Mtume Alisema: "Hakika dini hii ni nyepesi, na yeyote yule atakayeshadidisha  basi dini itamshinda. Hivyo basi, ‎fanyeni amali zenu kikamilifu na kama hamtaweza fanyeni kwa  kadiri  iwezekanavyo, na furaheni kwa  ‎malipo mema. Na tumilieni nyakati za asubuhi mapema, jioni na sehemu ya usiku ‎kufanya ibada".
Tatu: kuvuka mipaka na kufuata misimamo mikali kunampelekea mtu atoke mbali na dini sahihi, imepokelewa kutoka kwa Abi Saeed Al-Khudariy amesema: "Ali amepeleka kwa Mtume (S.A.W) akiwa nchini Yemen kipande kidogo cha dhahabu, basi Mtume Alikigawanya baina ya Al-Aqraa ibn Habis Al-Handhaliy, na moja wa banu Mugashe, na baina ya Uyaynah Ibn Badr Al-Fazari, na kati ya Alqama Inb Allatha Al-Amiriy, kisha moja wa banu Kilaab na baina ya zayd Al-Khayl Al-Twa’ii, kisha moja wa banu Nabhaan, basi watu wa kabila la Quraish na Al-Ansaar wakakasirika na wakasema Mtume Anawapa viongozi wa Najd na anatuacha, Mtume‎(S.A.W) ‎ akasema "hakika nataka kuwatendea  hisani" basi akaja mtu maskini  na akasema "ewe Muhammad mcha Mungu", Mtume‎(S.A.W) ‎akasema "nani anamtii Mwenyezi Mungu nikimwasi, yeye Ameniwekea amani juu ya watu wa ardhi, na nyinyi hamniwkee amani", basi mtu miongoni mwa maswahaba ameomba ruhusa ya kumwua na nadhani kwamba mtu huyu ni Khalid Ibn Al-Waliid, lakini Mtume‎(S.A.W) ‎  amemzuia, na alipoondoka, Mtume (S.A.W) akasema: "hakika watatoka watu ‎ kutoka chanzo wa mtu huyo wanaosoma Qurani isiyopita kwenye koo "yaani wanasoma Qurani bila ya kuitekeleza", wanatoka kutoka Uislamu kama mshale unaotoka haraka kutoka uta, wanawauwa waislamu na wanaacha wanaoabudu masanamu, hakika nikiwakuta  nitawaua kama walivyouwawa watu wa Aad".
Nne: hakika kuvuka mipaka na kufuata misimamo mikali ni sababu ya kuangamiza mataifa kwa mujibu wa hadithi ya Mtume tuliyoitaja hapo kabla: "hakika jambo lililowaangamiza watu waliokuwepo kabla yenu ni kuvuka mipaka ya dini".
Tano: kwamba kuvuka mipaka na kufuata misimamo mikali ni uzushi katika dini, Mtume (S.A.W) akasema: "nakuusieni kwa kumcha Mwenyezi Mungu, kusikia na kutii hata akiwa mtumwa mweusi kutoka uhabeshi aliyekatwa masikio yake, hakika atakayeishi baada yangu atakuta hitilafu kubwa, basi wakati huo fuateni Sunnah yangu na Sunnah ya makhalifa walioongoka baada yangu, ishikamaneni sana kwa "meno", na jiepusheni mambo yaliyobuniwa katika dini kwani kila jambo lililobuniwa ni uzushi na kila uzushi ni potovu".

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.