Hukumu ya kutisha wenye amani na raia

  • | Thursday, 21 December, 2017
Hukumu ya kutisha wenye amani na raia

     Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na Swala na amani ziwe juu ya bwana wetu Mtume Muhammad (S.A.W) - na baadaye:
Hakika Uislamu umeharamisha kushambulia raia na wenye amani kwa kutukana, kupiga, kuua, au kwa aina yoyote ya unyanyasaji na kutisha. Katika hadithi iliyopokelewa na Imam Muslim kwamba Mtume (S.A.W) amesema: "Yeyote anayemwashiria ndugu yake kwa chuma, basi Malaika wanamlaani mpaka aiache, hata ikiwa yeye ni kaka yake".
Imam Al-Nawawi - Mwenyezi Mungu amemrehemu - amesema: "hadithi hiyo ni kusisitiza juu ya heshima ya Mwislamu na ukatazo mkubwa juu ya kumtishia au kumdhuru, na kauli ya Mtume (S.A.W) "Hata ikiwa yeye ni kaka yake" ni kutia chumvi katika kuonyesha ujumuisho wa ukatazo kwa mtu wowote akiwa anayeshtakiwa au asiyeshtakiwa, na hata ikiwa kwa njia ya mzaha ama siyo, kwa sababu kumtisha Mwislamu ni haramu kamwe, na kwa sababu pengine silaha inamshinda ghafla.
Katika Sunan Abu Dawood, Mtume wa Allaah (S.A.W) amesema: "Haikubaliki kwa Mwislamu amtishe Mwislamu."
Hii ni kuhusu kuashiria na kutishia tu, basi inakuwaje anayeua nduguye na kumwaga damu yake na kushambulia heshima yake takatifu na kumhofisha katika nyumba yake. Hakika anayefanya kama vitendo hivyo anapigana na Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na anafanya ufisadi ardhini, basi anastahiki malipo ya wadhalimu  duniani na adhabu katika Akhera, "Basi malipo ya wale wanao mpiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wakawania kufanya uchafuzi katika nchi, ni kuuwawa, au kusalibiwa, au kukatwa mikono yao na miguu yao kwa mabadilisho, au kutolewa nchi. Hii ndiyo hizaya yao katika dunia; na katika Akhera watapata adhabu kubwa" {Al-Maidah: 33}. Katika hotuba ya kuaga, Mtume (S.A.W) amesisitiza heshima za watu kwa ajili ya kuhifadhi utulivu wao na amani zao, akasema kama ilivyopokelewa na Bukhari katika Sahih yake: "Hakika damu zenu, mali zenu na heshima zenu ni haramu juu yenu kama ilivyo haramu katika siku yenu hii, katika mwezi wenu huu, katika mji wenu huu, je nimefikisha?".
Na anyepepa Silaha juu yetu kwa nia ya kuhofisha au kuua, basi hawi anafuata njia yetu sahihi au sunna yetu kama alivyoambia Mtume (S.A.W). imepokelewa na Abdullahi bin Umar (R.A( kwamba Mtume (S.A.W) amesema: “Yeyote anayetubeba silaha, basi siyo yetu. " Imekubaliwa”. Imekubaliwa na Bukhari na Muslim.
Kwa hiyo, ni lazima tujiende mbali na aina zote za vurugu, mawazo makali na vitisho na pia kukimwa yeyote anayefanya vitendo kama hivyo, vilivyokatazwa na sheria, na kumpatisha adhabu kali, ili tusafishe jamii yetu na kila mfisadi au dhalimu.  Na Mwenyezi Mungu aweze kuhakikisha nia na anaongoza kwa njia sahihi.


Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na Mawazo Makali
Kitengo cha Lugha za Kiafrika

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.