Uharamu wa kushambulia nyumba za ibada na wale walio ndani yake

  • | Thursday, 28 December, 2017
Uharamu  wa kushambulia nyumba za ibada na wale walio ndani yake

     Kwa jina la Mwenyezi Mungu, na Swala na amani ziwe juu ya bwana wetu Mtume Muhammad (S.A.W) - na baadaye:
Hakika kushambulia nyumba za ibada na kuwaua wale walio ndani yake ni ufisadi katika ardhi na inaenda kinyume na yaliyoletwa na Uislamu, na hukuma yake ni haramu kisheria, na vitendo kama hivyo ni mbali kabisa na Uislamu na mafundisho yake, na sheria ya Kiislamu  na dini zote zimeamrisha kushikilia mambo matano ya dharura nayo ni: dini, nafsi (roho), akili, heshima, na fedha, basi asili katika damu ni kuwa zimelindwa, kama pia nafsi zimehifadhiwa na kutukuzwa, na kwamba kuiua nafsi moja isiyo na hatia ni kama kuwaua watu wote. Mwenyezi Mungu Amesema “Aliye muuwa mtu bila ya yeye kuuwa, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote. Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote” {Al-Maidah: 32}
Haijuzu kisheria kuwa vitendo vya kiadui kama hivyo vinasifiwa kwa Jihad, kwani Jihad katika Uislamu imeruhusiwa kwa ajili ya kuondoa udhalimu na kuzuia uadui, Mwenyezi Mungu Amesema: "Na piganeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu na wale wanao kupigeni, wala msianze uadui. Kwani Mwenyezi Mungu hawapendi waanzao uadui". na Uislamu wa kweli umedhamini kwa wote wakiwa waislamu au wasio waislamu uhuru wa kufanya ibada zao, kuheshimu vitakatifu na nyumba za ibada, kwa hivyo Uislamu ni mbali kabisa na kila mashambulizi yaliyohusishwa nayo kwa uwongo na singizio. Inapaswa juu ya watu wote wajue kwamba matukio haya yote ya kigaidi hayataki ila uharibifu uangamizi na kuchochea fitna kati ya watu, kwa hiyo ni lazima sisi sote tuwe pamoja katika kupambana kwa nguvu na wadhalimu hawa. Mwishaoni tunaomba Mwenyezi Mungu Ailinde Misri na watu wake, na awapatiliza maadui.


Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na Mawazo Makali
Kitengo cha Lugha za Kiafrika

 

Print
Tags:
Rate this article:
5.0

Please login or register to post comments.