Dondoo za Taarifa ya Mwisho ya Mkutano wa Al-Azhar kuinusuru Al-Quds

  • | Thursday, 18 January, 2018
Dondoo za Taarifa ya Mwisho ya Mkutano wa Al-Azhar kuinusuru Al-Quds

     Mheshimiwa Imamu Mkuu katika taarifa ya mwisho wa Mkutano wa Al-Azhar wa kimataifa wa kuinusuru suala la Al-Quds:
•    Mji wa Al-Quds ndio mji mkuu wa milele wa nchi huru ya Palestina.
•    Inapaswa kutambua rasmi na kimataifa kwa uhuru wa nchi ya Palestina.
•     Utambulisho wa kiarabu wa mji wa Al-Quds ni jambo lisilo na shaka wala halikubali kujadiliwa tangu miaka maelfu maelfu.
•    Tunakataa kabisa ule uamuzi dhalimu wa mamlaka ya kimarekani, ambao hauzidi ila kuwa maneno matupu.


•    Tunaunga mkono wananchi mashujaa wa Palestina na mapinduzi wao wa kuikomboa nchi yao kutoka ukaliaji haramu wa kizayuni
•    Tunaambatana na juhudi za wapalestina na taharuki zao dhidi ya maamuzi dhalimu zinazowapora haki zao katika mji wa Al-Quds na Msikiti Mtakatifu wa Al-Aqsa.
•    Mkutano inaheshimu sana hisia za mataifa wa kiarabu na wa kiislamu na waadilifu duniani kulinusuru suala la Al-Quds.
•    Mkutano unaunga mkono pendekezo la Al-Azhar Al-Shareif kuufanya mwaka huu wa 2018 ni mwaka wa Al-Quds Al-Shareif.
•    Mkutano unaambatana na shauri la Al-Azhar Al-Shareif la kupitisha mtalaa wa kufundishwa katika taasisi za Al-Azhar na Chuo Kikiuu cha Al-Azhar kuhusu suala la Palestina.
•     Mkutano unayahimiza mashirika yote ya kimataifa kuuhifadhi utambulisho wa Al-Quds na kushikilia haki za kisheria za wapalestina kwenye mji huu.   

Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na Mawazo Makali
Kitengo cha Lugha za Kiafrika

 

Print
Tags:
Rate this article:
5.0

Please login or register to post comments.