Jihadi na Vita

  • | Tuesday, 13 February, 2018
Jihadi na Vita

     Jihadi siyo vita ambayo ina sababu na malengo yake maalumu ya kisiasa, bali Jihadi ni mapigano yanayokuwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu tu, na kama mapigano  yakipita mbali na wigo huo, basi hayaitwi jihadi, lakini yanakuwa kazi mbaya yanayokataliwa na sheria ya kiislamu na maadili yake, na toka hapa tunaweza kuweka ufafanuzi kwamba jihad ni kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu sawa sawa kukiwa kwa kushiriki moja kwa moja katika operesheni za kijeshi (vita) au kusaidia kwa fedha, rai, mawazo, kutoa huduma za matibabu au juhudi zozote zinazofanywa kwa ajili ya kuitetea itikadi na nchi.
     Lakini inatubidi kupambanua baina ya maneno mawili ambayo kuchanganyika baina yao kunapelekea ufahamu mbaya tunapofasiri Jihadi kwa kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu, maneno mawili hayo ni: kuuwa na kupigana, na tofauti kati yao ni kubwa sana, kwani mauaji yanamaanisha kwamba mtu maalumu anamwua mwingine kwa silaha yake, na hii inawajibika kuwepo pande mbili zinazopigana, na jihadi inamaanisha kupigana sio kuuwa. Na tunayoyafikia kutoka uchambuzi huo ni: kwamba amri kwa jihadi katika Uislamu sio amri kwa kuuwa, bali ni amri kwa kupigana au kuwazuia maadui na kupigana jihadi nao kwa ajili ya kusimamisha uadui na mashambulizi yake.
     Na jihadi kwa maana hiyo sio ila jina kuukuu la kiislamu kwa inayojulikana sasa hivi kama wizara ya ulinzi, ambayo ilikuwa inaitwa hivi karibuni kwa (wizara ya vita), au mabaraza makuu ya vita, na mfano wake ni wizara ya kambi katika nchi za kimagharibi, na ingawa majina hayo yote yanaeleza hofu na uadui, lakini hakuna yeyote aliyeshutumu haki za nchi za kimagharibi kuhusu kumiliki wizara ya ulinzi au wizara ya vita kama tunavyosoma shutuma dhalimu zinazofuatwa na mitandao ya kiingereza-kimarekani kwa haki ya Jihadi katika Uislamu. Na sisi tunadai kwamba jina la (Jihadi) ni bora zaidi kuliko jina la wizara ya vita; kwani vita -katika sheria ya kiislamu- inaweza kuwa vita vya kushambulia, na vita vya kutetea sawa sawa, ama Jihadi ni -kwa wenye kufahamu vizuri lugha ya kiarabu- haiwi isipokuwa kwa vita vya kutetea tu.
     Kwa hivyo Jihadi ambayo nchi za magharibi zinajitahidi kuichafua, siyo isipokuwa haki ya kuitetea nafsi, itikadi na nchi. Na mimi sidhani kwamba mwenye akili nzima anaweza kukanusha haki ya kikawaida isipokuwa wanaotaka kuharibu akili.

Profesa/ Ahmad AL-Tayyeb
Imamu mkuu wa AL-Azhar


Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na siasa kali
Kitengo cha lugha za Kiafrika

 

Print
Tags:
Rate this article:
4.0

Please login or register to post comments.