Tuhuma ya kutoka mwanamke nje ya nyumba yake kwa ajili ya kufanya kazi

  • | Tuesday, 4 September, 2018
Tuhuma ya kutoka mwanamke nje ya nyumba yake kwa ajili ya kufanya kazi

      Kundi la Daesh linatoa Fatwa kwa kutojuzu kwa mwanamke kutoka nje ya nyumba yake kwa ajili ya kufanya kazi, likitegemea dalili zifuatazo:

Kauli ya Mwenyezi Mungu: {Na kaeni majumbani kwenu}, [Al-Ahzab: 33].

Kauli ya Abdullah Ibn Masuud -R.A- kwamba Mtume (S.A.W) alisema: "mwanamke ni mwenye kujificha, akitoka nje ya nyumba, Shetani akamfanya mwanamke mzuri katika macho ya wanaume, na wakati inapokaa nyumbani mwake, basi akawa karibu na Mola wake ".

 

 

Jibu:

Sharia ya kiislamu imempa mwanamke ruhusa ya kutoka nje ya nyumbani mwake kwa ajili ya kufanya kazi inayoafikiana na maumbile yake, madamu akijilazimisha kwa mambo yaliyofaradishwa na Mwenyezi Mungu na adabu zinazomhusu mwanamke kwa upande wa mavazi yake na mazungumzo yake kwa wageni na kushirikiana nao, kwa dalili ya kutoka mwanamke nje ya nyumba yake wakati wa enzi ya Mtume (S.A.W) kwa ajili ya kujifunza na kufundisha elimu, ambapo ilikuwa miongoni mwa wanawake wasimuliaji hadithi.

Kama pia kutoka kwake nje wakati wa vita pamoja na wanaume kwa ajili ya kuwapa maji, kuandaa chakula, kutibu majiraha yao na kuwachocheza kupigana vita, na wakawa katika hali ya kujificha, kama alivyokuwa Rofaidah Bint Saad Al-Aslamiyyah, na ni daktari hodari aliyekuwa mjuzi wa upasuaji, Mtume (S.A.W) alimchagua kwa ajili ya kufanya upasuaji wakati wa vita, basi yeye alikuwa anatoka nje ya nyumbani mwake na kuchanganyika na wanaume na kutibu waliojeruhiwa kwa mkono wake. Vile vile Umayyah Bint Qays Al-Ghifariyyah, na Um Atiyyah Al-Ansariyyah: aliyekuwa mashuhurui kwa upasuaji na pia akatoka katika vita pamoja na Mtume (S.A.W) kwa ajili ya kutibu waliojeruhiwa na wagonjwa. Na pia Um Saliim: aliyekuwa akamshiriki katika vita vya Mtume SAW na baadhi ya wanawake kutoka Al-Ansaar ambapo walikuwa wanawapa wanaume maji, wanatibu waliojeruhiwa na wengineo wengi.

Ama jibu la dalili yao kwa kauli ya Mwenyezi Mungu: {na kaeni majumbani kwenu}.

Basi makusudio ya amri hapa kwa mwanamke kwa kukaa nyumbani sio kama wanavyodai baadhi ya watu kwamba Uislamu unawalazimisha mwanamke akae nyumbani, wala asitoke nje kamwe; lakini amri hiyo ina ishara nzuri ya kwamba nyumba kwa wanawake ni asili ya maisha yao, nayo ni makao makuu, na kinyume na hayo inakuwa ni dharura tu isiyo na sifa ya utulivu au kuendelea, bali ni haja inayokadiriwa kwa kadiri yake.

Kwa hivyo; maana ya aya inakuwa, kaeni nyumbani zenu wala msitoke ila kwa haja, na ikihakikishwa haja hiyo basi atoke na kufuata masharti na adabu zilizokiriwa na Uislamu, hata kama anatoka kwa ajili ya kwenda msikiti wa Mwenyezi Mungu aliyetakasika.

Print
Tags:
Rate this article:
5.0

Please login or register to post comments.