Watoto wapiganaji kwenye kundi la Daesh

  • | Sunday, 10 February, 2019
Watoto wapiganaji kwenye kundi la Daesh

     Kwa mujibu wa mfumo wa kituo cha Al-Azhar cha kupambana na fikra kali kuhusu kuangalia na kufuata makundi ya kigaidi ili kutambua mbinu za kisasa  na dhana yanazozieneza kupitia fikra zake kali, Kituo hicho kimetoa uchunguzi wake mpya kuhusu watoto wapiganaji kwenye makundi ya kigaidi, hasa kundi la Daesh, ambapo kimeashiria kupitia kwake juu ya mkakati unaotumiwa na makundi hayo kwa ajili ya kuwafanya watoto wajiunge nayo na njia zao za kuwalazimisha watoto wapigane pamoja nayo kuanzia ushawishi kwa njia ya pesa, hisia, hata kufikia michezo na kupitia njia ya mawasiliano ya kijamii.

Uchunguzi uligundua kwamba makundi ya kigaidi yalianzisha fikra ya kutumia watoto katika safu zake kwa ajili ya kufikia malengo yake na kutia amani kwa mbeleni mwake, jambo linaloonyesha kwamba makundi hayo yanatumia njia na zana zote ili kufikia malengo yao na kusambaza mawazo yao na kusimamisha "Khilafa" yake ya batili ambayo haiwezekani kuanzisha bila ya juhudi.

Aidha makundi ya kigaidi yanawapa mafunzo kwa watoto kwa ajili ya kutekeleza hukumu za kuua wengine, kwa lengo la kuwatishia maadui na kuwapa malezi "wapiganaji wadogo wa Khilafa" na kuhifadhi kwa mbeleni mwake inayodhamini kwake "kubakia na kueneza". Pia kundi limewezekana kuunda jeshi la "watoto wadogo" lililoitwa "wapiganaji wadogo wa Khilafa" baada ya kubadilisha mawazo yao kwa sababu ya kuwajiunga kwa makundi hayo.

Uchunguzi unasisitiza - katika Sehemu  yake ya pili – kuwa mashambulizi ya kigaidi yanafanywa na watoto wapiganaji wa Daesh, ili msomaji ajue halifu za kundi hilo kuhusu kukiuka kubwa katika haki ya utoto wao, jambo linalothibitisha kwamba kila anayejinasibisha na makundi hayo ya kigaidi, basi  hakuna huruma na ubinadamu moyoni mwake. Vile vile uchunguzi huo umezungumzia sababu zinazosaidia kuwageuza watoto hawa wawe hawana huruma, na uchunguzi umeashiria kwamba elimu ni nguzo ya kimsingi ambayo kundi hilo limewezekana kupata matokeo haya ya kutisha, kwa hivyo tumeainisha sehemu kutoka uchunguzi huo kwa mfumo wa kielimu ya Daesh, kwa ajili ya kuashiria mitaala yote ya kielimu yaliyotekelezwa na kundi hilo katika shule zake mbali mbali.

Baada ya kushindwa kundi la Daesh, na kupoteza kwake kwa aghalabu ya maeneo yaliyokuwa chini ya udhibiti wake nchini Iraq na Syria, na kutokana na kuzidi hofu ya kurudi  tena watoto hawa waliotumia fikra kali kwa njia zaidi, na kuwapata mafunzo ya kijeshi yaliyowafanya wawe na uwezo wa kutekeleza mashambulizi ya kigaidi, basi nchi imekuwa inahitaji kuweka mikakati ya kukabiliana na wanaorudi tena kutoka kwao, kwa hivyo tumenukuu majaribio ya baadhi ya nchi katika kukabiliana nao na kuwarejea kwao na kuwaunganisha tena katika jamiil. Mwishoni, uchunguzi umetaja alama zilizoashiria kuwepo kwa fikra kali, ambazo wazazi wanaweza kugundua mapema kuhusu watoto wadogo, na jinsi ya kuwalinda kutoka kujiunga na makundi hayo ya kigaidi, na hatua muhimu ya kuwaepusha kuathirika na fikra kali hizo.

 

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
2.0

Please login or register to post comments.