Hotuba ya Imamu Mkuu kwenye kongamano la "Nguzo za Amani katika Dini Tofauti" Katika Chuo Kikuu cha Monester, Ujerumani

  • | Saturday, 19 March, 2016
Hotuba ya Imamu Mkuu kwenye kongamano la  "Nguzo za Amani katika Dini Tofauti" Katika Chuo Kikuu cha Monester, Ujerumani

Hotuba ya Imamu Mkuu kwenye kongamano la
"Nguzo za Amani katika Dini Tofauti"
Katika Chuo Kikuu cha Monester, Ujerumani

Bibi Mheshimiwa Profesa; Orsola Neles
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Monester
Enyi Mabwana Wanavyuoni Maprofesa na Madaktari
Mabinti na Vijana wanafunzi wa Chuo Kikuu hicho
Assalamu Alykuma Warahmatu Allahi Wabarakatuh
Nakupeni nyote maamkizi mema, nikitoa shukrani zangu zote kwa Profesa; Neles kwa kunialika ili kushiriki katika kongamano hilo la kielimu, na kunipa nafasi ya kuzungumza nanyi na kusikiliza kutoka kwenu, kuhusu suala lililo hatari zaidi kuliko katika ulimwengu wetu wa kisasa, ambapo linatishia mafanikio yake ya kistaarabu, bali limekaribia kusababisha uharibifu mkubwa ulimwenguni mwetu, suala hilo ni suala la "Amani" ya kiinyeji na ya kimataifa, na kulinda staarabu za kibinadamu kutoka kwa hatari mbali mbali zinazozitishia, hatari iliyo kubwa zaidi kuliko ni hatari ya ugaidi ulioenea mabara yote, na ambao ukiachwa bila ya kupambana na kupiganiwa hukua na kupata nguvu zaidi baadaye itakuwa hatima ya lazima nayo ni kurudi nyuma kwa wanadamu wote kwenye hali ya fujo na ukatili, pengine itakuwa mbaya zaidi kuliko wakati wo wote kabla.
Enyi Wanavyuoni na wasomi, nipe ruhusa ya kueleza maoni yangu kuhusu maudhui kiyo kwa njia isiyo kawaida, na maoni yangu hiyo nimeipata kutpitia kwa kujishughulikia suala la kutafuta tafuta "Amani" niliyoikosa kwa muda ndefu, na hasa katika miaka ya mwishoni ambayo nchi za kiarabu zilizopo mashariki zikawa mahali pake ambapo damu zinazomwagika kila siku, maangamizi, uharibifu na hasara kubwa.
Kwa hakika msemaji aliye mbele yenu – Enyi Mabwana!- huwakilisha kizazi kamili, pengine sitakuwa mkosa nikisema kwamba kizazi hicho hawakupata kuishi kwa amani na usalama hata kidogo, bali walikabili vita bila ya kuwepo kwa sabau inayokubalika, nilipokuwa chini ya miaka kumi nimepata kushuhudia maadui wa pande – nchi – tatu dhidi ya Misri hapo mwaka 1956, nikataabika pamoja na wenzangu kwa sababu ya hofu inayoendelea jambo ambalo sitaki kulikumbuka baada ya kumaliza mwaka wangu wa sabini, na haikupita miaka kumi hata vita vya 1967 vilituvamia tukaishi baada ya vita hivyo miaka mitao yenye woga, huzuni na matatizo mengi, ambapo mji wa Sinai umepotea kwa ghafula, na hatari ikawa karibu mno tukateseka kiuchumi, na nikisahau kitu lakini siwezi kusahau kubomoa shule kamili na kwaua wanafunzi wote walikuwa ndani yake.
Kisha vita vya ukombozi vikakuja mwaka 1973, vikawa na hisia mpya tofauti, tumeijua kwa mara ya kwanza kwani hisia ya kushinda ni kinyume kabisa hisia ya mshindwa, na baada ya hapo tumedhani kwamba mashariki ya kiarabu imepata utulivu na inaweza kuanza awamu ya ustawi na maendeleo, na kujiunga kwa nchi zilizotutangulia katika maendeleo na ustawi, lakini hali ilibadilika haraka haraka kwa kuanza awamu mpya ya kuzuka vita kwa aina nyingine mpya, kutokana na mitazmo ya kisasa, ambapo mapigano na uadui hayalengei adui wa nje, bali yanalengea wananchi wa nchi moja wenyewe kwa wenyewe, baada ya kuandaa nchi inayokusudiwa kwa kubuni na kudai mizozo ya kimadhehebu, kidini na kijinsia na kueneza silaha mikononi mwa pande za mizozo ili vizuke baada ya hapo vita kali vinavyosababisha maangamizi makubwa kwa kila kitu.                    
Na akili iliyo sawa hupata kutahayuri ikijaribu kutafutia sababu moja inayowezekana kukubalika kwa maangamizi hayo yote yanayotokea katika nchi kadhaa za eneo, ambapo kujiokoa kutoka mifumo ya kisaliti haiwezekana kuwa ni kisingizio cha kuwaangamiza maraia wasio na dhambi kwa kutumia ndege, na kuziharibu nyumba zao wakiwa na wake wao na watoto wao,ilhali makundi mbali mbali ya kimadhehebu na kidini ziliishi pamoja kwa muda ndefu sana kwenye maneo hayo kwa amani na usalama, na pia dini na madhehebu hizo zenyewe zisizo mpya, bali ni kale mno, zilibaki pia zikiambatana na amani na usalama chini ya ustaarabu wa kiislamu, bila ya kudharauliwa kamwe kiitikadi wala kimapato, bali zikawa kitendakazi kimojawapo cha maendeleo na kuleta mshikamano katika jamii.
Vile vile akili hupata kutahyuri kuhusu kutambua sababu za kuzuka vita hivyo vyote katika eneo moja, na baina ya wananchi wa nchi moja, sio kwa wananchi wengine duniani.
Nilijaribu kutafutia eneo linaloteseka kutoka matumizi ya silaha na umwagaji damu, au makundi ya wakimbizi waliolazimishwa kuacha nyumba zao wakapotea jangwani na baharini bila ya kupata makazi wala vyakula wala madawa ulimwenguni mzima, lakini sikupata eneo lonalotesekwa na maovu hayo ila maneo ya nchi za kiarabu na kiislamu.
Nikajiuliza je eneo letu lilikuwa linapitia matatizo au mabadiliko yanayowajibika kuzuka vita kama vile vilivyoanza na hatujui litakwisha lini? Na je mapinduzi dhidi ya mfumo wo wote kati ya mifumo ya utawala katika enzi yetu hii inaweza kuwa kisingizio cha kuzuka vita vikali vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoendelea kwa miaka kadhaa bila ya kusimamishwa hata kwa siku moja? Na maswali mengineyo mengi sikupata kuyajibu kwa majibu ya kutosha, wazo la pekee nililoliamini ni kwamba Uislamu hasa - na dini zote - haiwezekani kabisa kuwa ni sababu ya maangamizi hayo yanayojiri na yasiyodhibitiwa, japokuwa wanaonufaika kwa vita waliweza kutumia dini kama ni kuni ya kuchoma na kukuza vita na uharibifu...
Enyi Maprofesa na Maulamaa, sitaki kukuchokesha kwa kutaja maelezo mabaya kuhusu maangamizi na mateso ambayo eneo la mashariki ya kati linayapata siku hizi, kwani mnayajua vyema, pengine zaidi kuliko sisi, lakini nataka kusema kuwa sio sahihi kuzotafutia sababu za kuleta amani tulizozikosea katika mafunzo ya dini za mbinguni tu, bali inapaswa kuzingatia hali za kisiasa za kinyeji na kimataifa, na siasa za usaliti wa kimataifa, na mifumo ya kiuchumi isiyoafikiana na tabia nzuri na vidhibiti vyake, ambayo watetezi wake hawaoni dhiki katika kuitumia ili kuwanufaisha wachache na kuwadhuru wengi wao, na kuhusisha maeneo ya kaskazini kwa utajiri, elimu, maendeleo na ustawi, ilhali huyahusisha maeneo ya kusini kwa umaskini, ujinga na mateso, tunapaswa kutafuta na kujadili sababu za kutokuwepo kwa amani kulingana na upungufu huo uliokusudiwa ukingoni mwa bahari ya kati, bali tunatakiwa kujadilu pia mwenendo wa stasrabu kuu za kisasa ambazo hazioni dhiki katika kubuni adui asiyekuwepo kwa ajili ya kumtumia kama ni kisingizio cha kuzuka vita mbali na nchi zake kwa kweli matatizo hayo magumu ya kimataifa nilizoziashiria baadhi ya alama zake mbaya ni sababu ya msingi ya mateso yanayoupata ulimwengu wa kiarabu na kiislamu siku hizi, na bodi la Umoja wa Mataifa lililoanzishwa kwa ajili ya kulinda amani na usalama za kimataifa linaweza kuchangia kuyatatua matatizo ya mashariki ya kati na kumaliza mateso yake kwa ajili ya kuwaokoa wake waliofiwa na mumeo, watu wanaofiwa na jamaa zao, na mayatima ambao hawana dhambi yo yote kuhusu mgogoro huu.
Enyi Mabwana!
Nataraji kunisamehe kwa maneno yangu haya yaliyo wazi wazi ambayo labda hayazoeleka katika hotuba za minasaba ya aina hiyo lakini najua vema kwamba nawahotubia marafaiki watukufu ambao sidhani kwamba mbinu yao katika kujadili matatizo na masuala magumu haitegemei kuchagua baadhi ya maudhui na kuacha nyinginezo ili kufikia matokeo yaliyo sawa…jambo lililoniwajibisha kuzungumza kwa lugha hiyo wazi bila ya kuficha cho chote, na haya niliyoyasema juu ndiyo maoni ya aghalabu ya wasomi, wenye kutafakuri na wachunguzi wa nchi za mashariki, na vyombo vya habari na mitandao ya mawasiliano ya kijamii zinayatolea kama ni jambo thabiti lisilo na shaka.
Ama kuhusu nguzo za amani katika dini mbali mbali, siwezi kuzidisha leo neno moja kuliko niliyoyasema kabla kuhusiana na maudhui hiyo kwenye mikutano ya mazungumzo baina ya dini mbali mbali katika miji mikuu ya nchi kadhaa barani Ulaya, Marekani na Asia, tangu miaka kumi na tano, na nisikufanyeni kutaabika naomba ruhusa ya kujumlisha maoni yangu kuhusu maudhui hiyo kwa kuzingatia dini ambayo ninajiunga nayo nikiamini msamaha na rehema zake kwa walimwengu:
Kwanza: Kwa hakika dini za mbinguni zimeteremshwa kwa ajili ya kumwongoza mwanadamu kwenye njia ya kufurahika duniani na ahkera, na kumfundisha maadili ya rehema, ukweli na kheri, na kwamba Mwenyezi Mungu amemtukuza mwanadamu zaidi kuliko viumbe vingine vyote, akamfanya ndiye khalifa wake ardhini, akaiharamisha damu yake, mali yake na heshima yake…na mkisikia au mkisoma kwamba dini miongoni mwa dini za mbinguni imehalalisha kumwaga damu au kuvunja haki, basi tambueni kuwa kuna uongo na khiyana katika habari hiyo kuhusu ukweli wa dini inayohusika..
Pili: Sisi waislamu tunaamini kuwa Uislamu sio dini inayojitengana na dini za mbinguni zilizotangulia kama vile Ukristo, Uyahudi na Uhanifa (Dini ya Kiibrahimiy), isitoshe bali Qurani Tukufu inatufundisha kwamba dini ya Kiungu ni dini moja tu ambayo jina lake ni Uislamu, kwa maana ya unyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu na kumwabudu, na kuusilimu uso kwake, na kwamba inayojulikana kama ni dini katika mazungumzo yetu haya ni: jumbe za kiungu zinazofungamana katika mfululizo wa dini moja…
Kwa hiyo tumekuta kwamba dini ya Uislamu inaafikiana na jumbe zilizoitangulia kuhusu vyanzo vya itikadi na misingi ya tabia, na ianfungamana kabisa na jumbe hizo, ambapo kuwaamini Manabii na Mitume waliotangulia na kuaviamini vitabu vya mbinguni vilivyoteremshiwa Mitume hao ni sehemu ya kimsingi ya imani ya mwislamu aliyemwamini Mohammad (S.A.W.) na Qurani.
Bali Qurani yenyewe inatubainisha kuwa dini iliyopitishwa na Mwenyezi Mungu kwa Mohammad ni ile ile dini iliyopitishwa kwa Nuh, Ibraham, Mussa na Isa (A.S.), jambo linalotuelezea upatanisho uliopo baina ya Uislamu na dini nyingine za mbinguni zilizoitangulia na hasa hasa: Ukristo jambo lililo wazi na halihitaji kubainishwa.
Tatu: Kuna mambo matatu ya kikweli katika Qurani ambayo yanasababishana, mambo hayo yanahusiana na mtazamo wa Uislamu kwa ubinadamu, na kuainisha uhusiano amabo waislamu lazima washikamane nao katika miamala yao na wengineo: ukweli wa kwanza ni kwamba matakwa ya Mwenyezi Mungu kuhusu viumbe vyake yanalazimika kuumbwa katika maumbile mbali mbali kidini, kiitikadi, rangi, kilugha na kijinsi na kwamba kutofautiana kwao ni thabiti haibadiliki kamwe wala haimaliziki, na ukweli wa pili ambao unasababishwa na wa kwanza ni kwamba uhusiano baina ya makabila haya na mataifa hao ni uhusiano wa kujuana ambao unamaanisha kusaidiana kwa pamoja, Qurani Tukufu imetaja uhusiano huo kwa tamko la "Al-Taaruf- kujuana" katika aya namba 13 katika sura namba 49, na uhusiano uliopo baina ya kweli hizo mbili ni uhusiano wa kusababishana kimantiki, kwani haikubaliki kwamba Mwenyezi Mungu Amewaumba watu tofauti katika dini zao, na wakati huo huo Awapa ruhusa ya kugeuza uhusiano uilopo baina yao ukawa mgogoro au mapigano au hata vita, ambapo hali hii inapingana na uhuru wa kutofautiana kiitikadi baina ya watu mbali mbali, na kuwalazimisha watu wote kufuata imani maalum katika wakati wa kupigana vita jambo linalowafanya watu kufuata itikadi moja..hapo ndipo ukweli wa kihistoria unajitokeza ambao ni kwamba waislamu hawakutumia panga dhidi ya watu wengine kwa sababu ya itikadi au dini zao, ila wakipiganiwa na maadui, basi hapo ndipo kupigania vita ni lazima kwa ajili ya kujibu uadui sio kwa sababu ya kutofautiana katika dini.. ama ukweli wa tatu ambao unahusiana na kweli mbili zilizopita kama ni tokeo la kawaida la kweli mbili hizo ni uhuru wa itikadi, ambapo Uislamu ulizingatia sana kuzihifadhi itikadi zote, na naweza kuwakumbusheni kwa jambo mnalolijua vyema na mnalihifadhi kabisa nalo lililotajwa katika aya mbili zifuatazo: "Hapana kulazimisha katika Dini. Kwani Uwongofu umekwisha pambanuka na upotofu" Al-Baqarah: 25, "Basi atakaye, aamini. Na atakaye, akatae" Al-Kahf: 29, na hadithi yake Mtume (S.A.W.) aliposema: {Ye yote atakayechukia Uislamu akawa myahudi au mkristo, basi haifai kulazimishwa kuacha dini yake}.
Nne: Qurani tukufu inasisitiza kwamba Mwenyezi Mungu hakumtuma Mtume Mohammad (S.A.W.) ila kwa ajili ya kuwa rehema kwa walimwengu wote, na neno la walimwengu ni la kijumla zaidi kuliko waislamu, bali katika falsafa ya kiislamu ni kwa ujumla zaidi kuliko dunia ya wanadamu, ambapo linajumlisha wanyama, mimea na vitu visivyo hai, imekuja hayo katika Qurani tukufu kwa njia ya kumhotubia Mtume Mohammad (S.A.W.) kwa kusema: "Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote" Al-Anbiyaa: 107, naye Mtume amejisifu akiwaambia watu wote kwa kusema: {Kwa kweli mimi ni rehema iliyotuzwa}, na wakati hautatosha kwa kuzungumzia matendo mazuri ya Mtume (S.A.W.) na walimwengu hao wote, lakini nitatosheleka kwa kuashiria tu kwa mafunzo yake ambayo alikuwa akiwaombea maswahaba wake walazimika kwayo kama vile kuharamisha kumwua mzee, mnyonge, mwanamke, mtoto na kipofo katika majeshi ya maadui, na kuharamisha kuwaua wanyama wa maadui ila kwa sababu ya dharura ya kula, na kuharamisha kuziharibu nyumba za maadui na mimea na nyuki zao.. na la ajabu kwamba tunafundishwa maadili ya kuwarehemu wanadamu, wanyama, mimea na hata vitu visivyo hai yatufikia katika mazingira ya kupigana vita na maadui wanatuchukia na wanatutakia maangamizi na maovu, lakini hakuna la kushangaa tukitambua kwamba hiyo ndiyo rehema aliyoieleza Mtume (S.A.W.) aliposema: {Kwa kweli mimi ni rehema iliyotuzwa} na ambayo imejumlisha walimwengu wote hata maadui wenyewe, Mtume huyo mwenye kurehemu wanyama alituambia kwamba mwanamke mmoja aliingizwa motoni kwa sababu ya kufunga paka bila ya kumwacha ale au kumpa chakula, na alituambia pia kwamba mtu mmoja alimpa mbwa maji baada ya kujua kwamba mbwa huyu anasikia kiu katika siku iliyokuwa joto sana basi alistahiki kusamehewa na Mwenyezi Mungu akaingizwa peponi..
Tano: Maelezo ya Qurani hayahusiani kufungamanisha Uislamu kwa amani kutokana na msingi wa rehema tu, bila ya kujali waislamu wamesifika kwa maadili haya mema au wameyaacha kwa hiari au pasipo na hiari, bali Qurani imetaja neno la " As-Salam " kwa wingi kwa hali ya kuzingatiwa, mpaka matamshi ya Usalama na Uislamu yakawa kama ni pande mbili za dinari moja tukiweza kufanya tashbihi hiyo, na dalili ya kutosha juu ya haya ninayoyasema ni kwamba neno la "As-Salam" kwa minyampuliko yake limetajwa katika Qurani mara mia moja na arobaini ilhali neno la "Vita" lilitajwa pamoja na minyampuliko yake mara sita tu, kwa hivyo si la kushangaa kwamba Uislamu ilipitisha msingi wa Amani kama ni chanzo muhimu miongoni mwa vyanzo vya matendeano baina ya waislamu na wasio waislamu, na kwamba falsafa ya Qurani haina nafasi ya mahusiano ya kugongana wala kupigana na wasio waislamu wasiofanya uadui.
Enyi Wanavyuoni Watukufu!
Vipi tunaweza kutekeleza na kutumia dhana ya amani katika dini ipasvyo katika hali halisi ya kisasa? Na hebu shikeni jibu langu nililotaja mwishoni mwa hotuba yangu hii nalo ni: tunapaswa kwanza kuunda amani baina ya wakubwa wa dini mbali mbali wenyewe, na sio baina ya wakubwa wa dini moja, na hilo ni tatizo kubwa linalohitaji mazungumzo kwa ajili ya kutafuta mambo ya pamoja yaliyopo baina ya dini tofauti ambayo ni mengi na yanastahiki kuzingatiwa, ambapo wakubwa wa dini mbali mbali endapo hawataafikiana na kuyatatua matatizo yao wenyewe kwa wenyewe basi hakuna tamaa kwamba wataweza kutoa wito za kuleta na kutekeleza amani na kuihubiri baina ya watu, kwani anayekosa kitu hawezi kukitangulia kwa mwingine…
Ama kuhusu namna ya kufanya hivyo basi hilo ni jambo nililotaka kulijua kutoka kwenu enyi waheshimiwa.
Nakushukuru sana kwa kunisikia kwa uangalifu;
Assalamu Alykuma Warahmatu Allahi Wabarakatuh

        Ahmad Al-Tayyib
Sheikhi Mkuu wa Al-Azhar

 

Print
Tags:
Rate this article:
5.0

Please login or register to post comments.