Mwanzoni mwa ziara yake nchini Ujerumani … Imamu mkuu akutana na viongozi wa makanisa ya kikristo

  • | Tuesday, 15 March, 2016
Mwanzoni mwa ziara yake nchini Ujerumani … Imamu mkuu akutana na viongozi wa makanisa ya kikristo

Mwanzoni mwa ziara yake nchini Ujerumani …
Imamu mkuu akutana na viongozi wa makanisa ya kikristo..akisisitiza kwamba:
•    Jukumu langu lililo muhimu zaidi ni kueneza usalama ulimwenguni kote na nitamzuru Pope wa Vatikan karibuni.
•    Nina tamaa kubwa mno ya kuunda na kupitisha usalama na amani kwa ulimwengu uliokosa amani.


Mheshimiwa Immau mkuu profesa; Ahmad Al-Tayyib sheikhi mkuu wa Al-Azhar Al-Shareif na mkuu wa baraza la wakuu wa waislamu ameanza ziara yake nchini Ujerumani kwa kutembea makao ya Maaskofu ya Kikatholiki kwenye mji wa Berlin mji mkuu wa nchi hiyo kutokana na mwaliko wa Askofu wa kanisa hilo, ambapo yule mheshimiwa alipokelewa na Askofu Hanz Yujan Yashkah mkuu wa tume ya mazungumzo baina ya dini mbali mbali, mwakilishi wa Vatikan nchini Ujerumani na kiongozi wa mambo ya kidiplomasia ya kigeni mjini Berlin, pamoja na viongozi wa makanisa ya kiinjili, kiorthodhoksia na ya kiyunani (kiigriki) licha ya mkuu wa kituo cha mazungumzo ya kiislamu- kikristo, na askofu Dumyan askofu wa kanisa la kikoptiki nchini Ujerumani.
   Kwenye ufunguzi wa mkutano huo askofu Hanz Yujan Yashkah mkuu wa tume ya mazungumzo baina ya dini mbali mbali katika kanisa la kikatholiki ameelezea furaha yake mkubwa kwa ziara ya Mheshimiwa Imamu mkuu na kuitika kwake kwa mwaliko wa kanisa la kikatholiki akisisitiza umuhimu wa upande wa kidini maishani mwa mataifa.
Akaongeza kwamba ziara ya Mheshimiwa Imamu mkuu kwa kanisa ni ziara ya kihistoria inayotilia mkazo hamu ya Mheshimiwa Imamu mkuu na kuzingatia kwake kwa mazungumzo ya kiislamu - kikristo ya pamoja kwa lengo la kutekeleza maslahi za ubinadamu mzima.
Na katika hotuba yake kwenye mkutano huo, Mheshimiwa Imamu mkuu amesisitiza kuwa usalama na rehema ni misingi ya lazima ya kidini ambayo haiwezekani kuiweka mbali kwa ajili ya kupitisha utulivu na amani duniani, akibainisha kwamba jukumu lililo muhimu zaidi maishani mwake ni kueneza utamaduni wa usalama pande zote duniani, ambapo sisi sote tunashirikiana pamoja katika ubinadamu na ni haki ya wanadamu wote kujineemeka kwa usalama na amani, basi tunapaswa kufanya juhudi zote kwa ajili ya kueneza mawazo hayo baina ya watu wote.
 Yule mheshimiwa akaongeza kwamba: dini tatu za mbinguni zinafungamana na chanzo kimoja, na kwamba Mwenyezi Mungu hakuteremsha dini hizo ila kwa ajili ya kuwaongoza wanadamu ili wapate kufanikiwa hapa duniani na akhera, akikumbusha kwa jaribio la "Baytul A'ila ya kimisri" (Jumuiya ya wananchi wa dini mbili waislamu na wakristo nchini Misri) na mafanikio iliyoyafikia ambapo iliweza kuhifadhi muungano baina ya sehemu mbili za wananchi wa kimisri na mshikamano baina ya wananchi wa nchi moja ambao ni waislamu na wakristo.
Akiendelea hotuba yake Imamu mkuu alisema: "Nimekuja kwenu nikiwa na tamaa kubwa ya kuunda na kupitisha usalama na amani kwa ulimwengu uliokosa amani ili tuweze kuwaokoa wanadamu kutoka shari lililo karibu nao hivi sasa", akielezea kwamba atatolea karibuni kitabu kwa anuani ya: "Kutafuta Usalama".
Mwishoni mwa hotuba yake, Mheshimiwa Immau mkuu alitoa shukrani kwa viongozi wa makanisa ya kikristo kwa kupanga na kuchunga mkutano huo, akielezea upya hamu yake ya kuendelea mazungumzo ya kidini na kuyasukuma mbele, akiashiria kwamba ana nia ya kumzuru Pope mtakatifu wa Vatikan wakati ujao.

 

Print
Categories: Habari
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.