Dondoo za hotuba ya Imamu mkuu ya kihistoria kwa Ummah mjini Jakarta

 • | Tuesday, 23 February, 2016
Dondoo za hotuba ya Imamu mkuu ya kihistoria kwa Ummah mjini Jakarta

Imamu mkuu achunguza madai ya ubaguzi dhidi ya wakristo wa mashariki…akisisitiza kwamba:

 • Raia wa Indonisia wana roli muhimu sana katika Ummah wa kiislamu na wana athari dhahiri katika historia ya Uislamu na waislamu.
 • Majaribio ya kufunganisha baina ya Uislamu na ugaidi ni dhuluma kubwa.
 • Waislamu wanatofautisha baina ya dini kama ni uongofu unaotokana na Mungu na baina ya wanaoitumia dini hiyo kwa ajili ya kuhakikisha maslahi yao na siasa ya usaliti na utawala.
 • Haikubaliki kukaa kimya mbele ya ukiukaji unaofanywa dhidi ya waislamu wanyonge nchini Myanmar … vile vile haikubaliki kukaa kimya kuhusu ukaliaji wa mji wa Jerusalem na majaribio ya kuubadilisha sifa yake iwe wa kiyahudi.
 • Nawaombea wenye hekima na busara duniani kuchangia kuyatatua ubaguzi unaofanywa na wasio waislamu dhidi ya waislamu pande zote za mashariki na magharibi.
 • Sijui dini wala kitabu kitakatifu cha mbinguni zinazotia adhabu kali ya umwagaji damu hapa duniani na akhera zaidi kuliko Uislamu.
 • Ummah ulipatwa na mzizi mbaya kati ya wana wake na vijana wake wanaofanya jinai za mauaji, uchomaji na ukatili mbaya kwa miili za maiti sawa ni waislamu au wasio waislamu kwa jina la dini.
 • Al-Azhar Al-Shareif haichelewi kamwe kuonya mara kwa mara kutoka hatari za mawazo potofu yanayolingania ukatili na ugaidi.
 • Imefika wakati wa kutubu kwa watu hawa waliofanya maovu dhidi ya dini yetu, ummah wetu na historia yetu na kurejea haki afdhali kuliko kuendelea katika upotovu.
 • Maulamaa wanapaswa kuhifadhi umoja wa ummah na misingi ya itikadi yake kutoka uharibifu wa wenye misimamo mikali na walikosa uongofu na maoni ya wajinga.
 • Kuiboresha mitaala kutategemea Qurani na Sunnah sahihi, na waliyoyakubali maulamaa wa waislamu, na kujiweka mbali sana na kuzingatia mambo yanayosababisha hitilafu badala ya mambo ya kimsingi yaliyo thabiti.
 •  Tunapaswa kutambua kwamba hali ya kuwa na upendeleo kwa masuala yanayosababisha hitilafu na fatwa zisizo za kawaida, hali hiyo imechangia sana kupatwa na migawanyiko na mizozo kwa ummah.
Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.