Mkakati wa Kuihujumia Al-Azhar

Na; Abdul-Nasser Salama

  • | Saturday, 9 January, 2016

Siamini kwamba kuna miongoni mwetu asiyetambua roli ya Al-Azhar kuuhifadhi usalama wa kijamii, au umuhimu wake kuueneza uwastani wa kidini, sio nchini Misri pekee, bali katika aghalabu ya nchi za ulimwengu wa kiislamu. Siamini pia kwamba kuna miongoni mwetu anayekataza roli ya Al-Azhar kutufundisha mafunzo ya dini yetu kama ipasavyo, kupitia maulamaa wanaotuhotubia juu ya minbari msikitini, au kupitia redio ya Qurani Tukufu, au kupitia masomo shuleni, au mahali popote, siamini kwamba kuna miongoni mwetu asiyetambua roli ya kihistoria ya Al-azhar kuupigania ukoloni wa kigeni, na kuwahimiza wananchi dhidi ya ukaliaji wa kizayuni, na kufundisha misingi na vyanzo vya dini barani kote, siamini kwamba kuna asiyetambua kwamba Al-Azhar inafundisha Fiqhi kwa madhehebu nne tu, sio zaidi, basi haifuati kabisa Uwahabi ulio na misimamo mikali, wala Wadaesh walio na mwenendo wa kikatili, wala ugaidi wa Khawarij.

Pengine mambo hayo niliyoyataja juu ni sababu ya hujumu kali inayoelekezwa dhidi ya Al-Azhar na Imamu wake wakati huu, kupitia jumuiya isiyofichika sawa kwa kiwango cha madhumuni wake au pande zinazoiunga, na katika kuhakikisha mkakati huu ambao ukawa wazi sana, na unaolengea kueneza vurugu na ugaidi katika eneo lote, ili kuandaa kuzuka vita vya madhehebu ambayo alama zake za mwanzo zilidhihiri katika nchi kadhaa zilizo karibu nasi hivi sasa, japokuwa na majaribio hayo ya kuwasha moto ya fitina katika eneo letu Al-Azhar ingali ndiyo taasisi pekee ya kidini yenye imara, na yenye ukweli, kwa maulamaa wake, inayoweza kutekeleza jukumu lake kama ipasavyo, jambo ambalo wale wachochezi na wenye mawazo batili na wahaini wanalitambua vyema.

Basi baada ya muda fupi mno ya kufichika kwa mmoja wa wale wanaosukumwa kuihujumia dini, ila ajitokeza mwingine akidai kwamba yeye ni mwenye jitihadi na mawazo ya kuporesha, katika juhudi za kugawanya majukumu, chini ya idara ya mkakati ambayo haijaona aibu kutangaza uovu na uhalifu, mpaka wakafika kiwango cha kutumia tamko la kuishtaki Al-Azhar kimataifa, kwa tuhuma ya kueneza ugaidi, na kuizingatia Al-Azhar ni kundi la kigaidi n.k. kati ya tuhuma batili zinazoeleza ufisadi wa akili za watu hao, wakati ambapo serikali na mamlaka rasmi zimebaki kimya, jamabo ambalo likidumu zaidi basi Misri italipa thamani ghali ambayo ni kupatwa na jinai kali za ugaidi na vurugu, kama zinavyotesekwa nayo nchi zinazotuzunguka mahali pote.

Kwa hakika majaribio wazi yanayojiri hivi sasa kwa lengo la kuzihujumia usuulu za dini (vyanzo vya dini) na juhudi zinanzofanywa na pande kadhaa ili kuichafusha Al-Azhar na maulamaa wake, yanahitaji kukabiliwa na msimamo rasmi, ili kumaliza ghasia hiyo, kwani msimamo wa kiraia hapa utapelekea vurugu na mapigano, na sidhani kabisa kwamba itakuwa sahihi kuwaombea maulamaa waheshimiwa wa Al-Azhar wajiingiza katika mahojiano ya aina yo yote na wale wajinga wasioamini kamwe kuwepo muumbaji wa ulimwengu, kwa hiyo mazungumzo au mahojiano kama hii hayatakuwa na faida yo yote ambapo itategemea vitabu visivyo na ukweli wo wote pamoja na maneno mabaya yasiyostahiki kusikilizwa.

Sisi hapa hatukataa mazungumzo au kufanya mahojiano, lakini wakati huo huo tunasisitiza kwamba mazungumzo ya aina yo yote lazima iwe na usawa, inalazimika kwa vidhibiti vya akili, mantiki, usawa wa kielimu, na isitegemee kuwatangulia wale wahaini, au wasio na tabia iliyo sawa, au wenye mawazo maovu, ili kuingia mahojiano kama haya kwa lengo la kubadilisha mazungumzo iwe magombao na mahojiano iwe nafasi ya kulaaniana na kuhujumiana na mtu mheshimiwa kama Imamu mkuu wa Al-Azhar hasa, jambo liliomfanya yule mheshimiwa ajizuie wakati wote kujiingiza katika magombano na mgogoro kama hii, kwa mujibu wa hekima iliyomwezesha atambue mkakati mbaya ulioandaliwa dhidi yake na Al-Azhar nzima.

Lakini wakati huo huo japokuwa tunamwunga mkono katika kukataa kujiingiza katika mahojiano na wale wapumbavu, lakini hali ya mamabo kitaifa na kimataifa likawa hatari mno, jambo linalotulazimsha kuzuia maovu haya ya kila siku ambayo yamezaa vurugu, ugaidi, na kuzuka hali kuu ya ghadhabu na kutokuwa radhi, pia limepelekea kuenea hali ya uchochezi nchini Misri, ambapo tumetambua ukweli ya hali, na kwamba haya ni kama kuunda mizizi ya fitina na sababu ya kuzuka moto unaoweza kuchoma jamii nzima.

Enyi mabwana! Maneno yo yote kuhusu hotuba ya kidini, na unaoitwa uporeshaji wa aina yo yote, lazima itokane na Al-Azhar peke yake tu, na yo yote kinyume haitakuwa na faida wala haitapelekea ila ghasia na vurugu zaidi, basi mjiepusheni na matendo na maneno hayo mkiwa hamtaki kusababisha ghasia.

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.