Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwengi wa kurehemu mwingi wa rehema

  • | Tuesday, 24 November, 2015
Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwengi wa kurehemu mwingi wa rehema

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwengi wa kurehemu mwingi wa rehema

Shukrani zote kwa Mwenyezi Mungu, Swala na amani zimfikie nabii wa rehema na mtume wa amani Muhammed Bin Abdullah, jamaa zake na maswahaba wake…

Enyi waheshimiwa watukufu wakuu wa waislamu

Assalamu Alykum Warahmatullahi wabarakatuh..,

Mwanzoni kabisa mnipe ruhusa ya kuanza mkutano wetu huu, kwa kujadili msiba wa ugaidi ambao ulimwengu wote ulipatwa nao siku hizi, ukafika mahali na nchi zilizo mbali sana, hatukuwa na matarajio ya kwamba utafika upeo huo, hakika ugaidi wa kikatili umegonga Lebanon ambapo Uarabu na kuishi pamoja baina ya wafuasi wa dini na tamaduni tofauti, ukafika mji mkuu wa Ufaransa Paris wiki iliyopita, mji wa elimu na utamaduni, ukaua wana wake zaidi ya mia moja, ukasababisha madhara na majeraha kwa mamia wengine wa vijana na wananchi wake, wengi wao anatesekwa na majeraha mabaya sana akakaribia kuaga dunia ambapo yuko hali mbaya ya kiafya, na tukifikiria idadi ya familia za kifaransa zinazotesekwa na ambazo hali yake imegeuka kutoka amani, usalama, utulivu na kujipatia anasa za dunia, na tama ya kudumu ya kwamba kesho ni afadhali zaidi kuliko, hayo yote yamegeuka ghafla, yakawa maisha magumu sana ambayo inafanana na maangamizi matupu na huzuni ya kudumu, inayoenea nyumbani, wanawake na watoto…wasio na dhambi hao hawakuwa sababu ya kutukia misiba, maangamizi, na haribifu zilizowafikia.

Hatuwahi kustaafu kutoka janga la Paris, mpaka imefika janga la Jamhuri ya Mali, ambapo mateka kadhaa waliuawa mjini Pamako, na Mwenyezi Mungu pekee ajuaye mustakbali wa wanadamu pamoja na makundi ya kigaidi (mafia ya vifo), na wafanyabiashara wa shari, na wanaoenenza ukatili…

Na tulikuwa tunadhani kwamba tuliopatwa nalo, sisi waarabu na waislamu, katika eneo la mashariki kati ya athari za damu zilizowafikia wanadamu na vitu visivyo hai ndilo mwisho wa maangamizi, na kwamba uharibifu wa nchi kadhaa za kiarabu na za kiislamu mbele ya wenyeji wake na kuwapoteza baharini na nchi kavu, ndilo kila lililofichika nyuma ya siku, lakini tumegundua kwamba jambo hilo linaenea kufikia pande za magharibi, kaskazini, na kusini kama lilivyoenea kwa upande wa mashariki hapo kabla, na pengine wakati umefika kutambua kuwa ugaidi ni itikadi na fikira, bali nakaribia kusema ukweli wenyewe nikisema: kwamba wafuasi wake wana falsafa katika maisha yao, inayorahisisha mauti na kujitolea kwa ajili ya kuitetea, na kwamba ugaidi huo hauambatani wala hautokani na dini yo yote miongoni mwa dini za mbinguni, bali ni ugonjwa wa kifikira na kisaikolojia unaotafutia visingizio vya kuhalalisha kuwepo kwake katika matini za Mutashabih  za dini tofauti na tafsiri ya watafsiri, pia historia na hali halisi ya kisasa zinathibitisha kwamba sababu za kuzuka kwa ugaidi hazihusiani na kuzigeuza dini kwenda dhana batili na za kimakosa, bali mara nyingi ugaidi umetokana na madhehebu ya kijamii, kiuchumi na hata kisiasa, ukasababisha maafa ya maelfu bali mamilioni ya wahanga wasio na hatia kutokana na migogoro ya kimadhehebu na kifalsafa –isiyoambatani kabisa na dini -…

Na mafunzo ambayo wote lazima wayafahamu, na hasa katika hali hiyo ngumu iliyopo katika ulimwengu, ni kwamba ugaidi hauhusiani na dini yo yote, wala utambulisho, na kwamba kutoka dhuluma kubwa, bali ni upendeleo usiokubalika, kunasabisha matukio yanayojiri hivi sasa kati ya jinai za kulipua na maangamizi zilizoenea huku na kule, kwa Uislamu, kwa sababu ya kwamba wahalifu wanaoyatekeleza walifanya hivyo wakisema "Allahu Akbar" wakati wa kufanya jinai zisizokubaliki kamwe…

Na sisi hapa katika baraza la wakuu wa waislamu na katika Al-Azhar Al-Shareif wakati wa kutoa rambirambi kwa jamaa za wahanga barani Ulaya na Afrika, tunataraji kutoka wao wote – na hasa wasomi, wanasiasa na watu wa dini – wasishughulikia maangamizi hayo wakisahau ulazimu wa kutendeana na mambo kutokana na msingi wa uadilifu na ukweli na kuweka mambo katika mazingira yake iliyo sawa kulingana na kutenga baina ya Uislamu pamoja na misingi yake, utamaduni wake na ustaarabu wake, na wale wachache wasiowakilisha waislamu wanaofuata mwenendo wa kiwastani na wapenzi wa kueneza amani dunia nzima hata kidogo, na kwamba sisi waislamu tumepatwa na tungalipita kwa marudufu wa mashambulizi hayo ya kigaidi ambayo yametekelezwa na majeshi na mafia waliojificha nyuma na dini, zikamwagika damu nyingi zetu hazisita mpaka sasa hivi wakati wa kusema maneno yangu haya.

 Na hayakutukia kwamba jambo limechnaganywa bongoni mwa waislamu baina ya jinai hizo na dini ambazo jinai zimenasabishwa nazo…na inapaswa juu ya waliofanya uhalifu wa kuchoma Mushaf Mtukufu na Misikiti ya Mwenyezi Mungu katika nchi za kimagharibi wajue kwamba vitendo hivyo pia ni ugaidi ulio wazi kabisa, bali ni jambo la kuzidisha mawazo ya kigaidi tunayoteseka nayo, basi msijibisha ugaidi kwa ugaidi mwingine, na haikubaliki kamwe kutoka wanaodai maendeleo kuvunja heshima ya mahali na vitu vitukufu vya wengine hivyo mbele ya watu wote.

Enyi wakuu!

 Umefika wakati wa kukabiliana na jukumu hilo linalozidi siku baada ya siku, ambapo hiyo ni Qadari yenu na Qadari yetu sote, na jukumu letu  ikawa ngumu kabisa, na yenye pande kadhaa: na ikawa ni lazima tuelekee kuzima moto na kumaliza sababu za migogoro katika ulimwengu wetu wa kiarabu na wa kiislamu.

Na pengine kuhudhuria kwa ndugu mheshimiwa Bw; Abdul-Kader Shaikh Ali Ibrahim waziri wa Wqfu nchini Somalia leo ni jamabo la kupata tamaa ambapo tutaanza kazi yetu kwa ajili ya kuwasaidia raia wa kisomali wawe na umoja na watoke mbali na matatizo yake ambayo yamedumu kwa muda nyingi bila ya kuwepo kwa sababu au mantiki, wakatesekwa nayo wale watu wa kawaida na maskini kati ya wananchi wa nchi hiyo, ambayo inatarajiwa iwe mnara wa kistaarabu na amani katike eneo la Pembe la Afrika.

La pili katika juhudi za kupambana na fikira za kigaidi kwa hali na namna zake zote, na kuwaalika viongozi wa kiarabu na kiislamu, kila mmoja kulingana na uwanja wake maalum, ili kukausha vyanzo vya mawazo hayo kupitia kazi ya pamoja inayojumuisha mafunzo, utamaduni, vijana, vyombo vya habari, hotuba ya kidini inayodhihirisha ukweli wa Uislamu na sheria zake.

Na la tatu katika kupigania vita dhidi ya hisia za chuki na uchochezi, na kueneza urafiki na mahaba wa kimataifa zilizoitiwa na Shekhi mkuu wa Al-Azhar Bw; Mohammed Mostafa Al-Maraghiy katika ujumbe wake mashuhuri alioutuma kwenye mkutano wa maulamaa wa dini uliofanyika mjini London hapo mwaka 1936 B.K. kutoka karne iliyopita, na katika mazingira hii inanifurahisha kutoa shukrani kwa vijana wa maulamaa wa Al-Azhar wa kiume na wa kike walioongoza misafara ya amani ambayo imepangwa na baraza la wakuu wa waislamu kwa nchi kumi na moja barani Ulaya, Amerika, Afrika na Asia.

 Na baraza litapanga leo (Inshaa Allah) kutuma misafara ya amani kumi na sita kwa ulimwengu kote ili kueneza mawazo ya amani na kusahihisha dhana potovu na kubeba tangazo la pamoja ambalo ni (mataifa wote wa ulimwengu ni sawa katika ubinadamu na kwamba wote wana haki ya kuishi wakiwa na amani, utulivu na usalama).

Hayo ni wajibu za lazima za kidini, kitabia bali za kibinadamu pia ambazo zinazifaradhisha hali ya mambo ya kisasa juu ya baraza la wakuu wa waislamu nayaona ni wajibu zinazohitaji kutimizwa haraka sio baadaye – kama walivyosema wanavyuoni wetu wa Usuul-. Basi tuendelee kazi kwa tukiomba msaada wa Mwenyezi Mungu na Auni na kuunganishwa naye, ambapo yeye ndiye Mtetezi na Msaidizi wetu aliye bora zaidi.

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.