Je, Uislamu unawazuia wasio waislamu kuingia Makkah na Msikiti Mtakatifu?

Suala la kumi na nne: nini hukumu ya kuwazuia wasio waislamu kuingia Makkah na Msikiti Mtakatifu?

  • | Saturday, 29 August, 2015

Makkah ni mahali takatifu pa Mwenyezi Mungu (S.W.) Amemwekea mtume Ibrahiim mahali hapo " Na pale tulipomweka Ibrahim pahala penye ile Nyumba tukamwambia: Usinishirikishe na chochote; na isafishe Nyumba yangu kwa ajili ya wanao izunguka kwa kut'ufu, na wanao kaa hapo kwa ibada, na wanao rukuu, na wanao sujudu". (Al-haj:26), na Mwenyezi Mungu Akamwamuru mtume Ibrahim kuwatangaza watu, na Amemwambia kwamba anapowatangaza watu watamjia kwa miguu au wakipanda “ngamia” ili kumwabudu Mola Mlezi wa Nyumba hii, na kwamba watakuja kutoka kila njia karibu au mbali:"  Na watangazie watu Hija; watakujia kwa miguu na juu ya kila ngamia aliye konda, wakija kutoka katika kila njia ya mbali."(Al-haj:27) na wao wote watakuja kwa nyumba hii ili kuizunguka (kuitakasa) na kusali na kutenda wanayoyaamrishwa kutoka kutukuza ibada za Mwenyezi Mungu:"  Ili washuhudie manufaa yao na walitaje jina la Mwenyezi Mungu katika siku maalumu juu ya nyama hoa aliowaruzuku. Basi kuleni katika hao na mlisheni mwenye shida aliye fakiri. 29 .Kisha wajisafishe taka zao, na waondoe nadhiri zao, na waizunguke Nyumba ya Kale"(kutufu).  (Al-haj:28.29).

Mahala hapo si mahali pa kitalii, japokuwa UNESCO au taasisi zengine zinapazingatia mahali hapo ni mahali pa kitalii, ambapo mahali hapo pameainishwa ili kuwa mfano mzuri wa kuigwa, ardhini nzima kwa sababu pana amani bila ya kuwepo woga juu ya ye yote, watu wakapajia ili kusali na kupazunguke (kutufu) na kushuhudia ibada zao, na mpaka siku hii hatusikii kwamba utawala wo wote umemzuia mtu miongoni mwa watu wanaokwenda kutekeleza ibada kati ya wanaozunguka au wanaosali au wafanyaji Umrah au mahujjaji wasiende kutekeleza ibada zao au kuwazuia kuzunguke Nyumba mtukufu ya Kale.

Ama kupageuza mahali hapa pawe mahali pa kitalii sio jukumu la mtu ye yote, ambapo Saudi Arabia au ulimwengu wa kiislamu wote au ardhi nzima hazina uwezo wa kugeuza mahali hapo takatifu, kutoka Nyumba mtukufu ya Mwenyezi Mungu kuwa mahali pa litalii, kwani kufanya hilo ni haki ya Mwenyezi Mungu peke yake sio haki ya ye yote mwingine, na kuna mahali pengi ulimwenguni panahusu dini, watu wa jinsia maalum, au mataifa maalumu, na mahali hapo pana utukufu, na heshima na pengine hairuhusiwi kuingiwa ila kwa watu maalumu, basi hatuoni kwamba msimamo huu unavunja haki za mtu au uhuru wake, bali unahifadhi haki za watu hawa walioainishwa na Mwenyezi Mungu peke yao kuhusika na mahali hapo, kwani ni sheria na mahli pa ibada zao" Kila umma tumewajaalia na ibada zao wanazo zishika. Basi wasizozane nawe katika jambo hili. Na waite watu kwendea kwa Mola wako Mlezi. Hakika wewe uko kwenye Uwongofu Ulio Nyooka "(Al-haj:67), na inaposemekana kwamba mahali hapo panawahusu wanaouamini utukufu na cheo chake kwenye Mwenyezi Mungu (S.W.), na kuamini thawabu ya ibada katika mahali hapo kwa mujibu wa maagizo ya Mwenyezi Mungu miongoni mwa ibada za kuzunguka (kutufu), usalama, rukuu na sujudu, basi hilo ni jambo linalopaswa kuheshimiwa, na kuheshimu sifa hasa za mahali hapo, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi zaidi

 

Print
Tags:
Rate this article:
4.5

Please login or register to post comments.