Profesa; Ahmed Al-Tayyib Sheikh mkuu wa Al-Azhar Al-Shareif kwenye mkutano wa kimataifa wa Fatwa kwa anuani ya: "Fatwa…Matatizo ya kisasa na Matamanio ya ujao"

  • | Tuesday, 18 August, 2015
Profesa; Ahmed Al-Tayyib Sheikh mkuu wa Al-Azhar Al-Shareif  kwenye mkutano wa kimataifa wa Fatwa kwa anuani ya: "Fatwa…Matatizo ya kisasa na Matamanio ya ujao"

Hotuba ya Mheshimiwa Imamu Mkuu
Profesa; Ahmed Al-Tayyib Sheikh mkuu wa Al-Azhar Al-Shareif  kwenye mkutano wa kimataifa wa Fatwa kwa anuani ya:
"Fatwa…Matatizo ya kisasa na Matamanio ya ujao"

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

Shukrani zote ni za Mwenyezi Mungu, rehma na amani na Baraka zimfikie Mtume Muhammad na jamaa zake na Swahaba wake..
Karibuni sana enyi wanavyuoni waheshimiwa, wenye wa fatwa na elimu, na wenye mahoja na fadhila, katika nchi yenu ya pili: Misri inayohifadhiwa na Mwenyezi Mungu mwenye nguvu zaidi, na katika   Al-Azhar Al-Shareif na makao rasmi ya Fatwa ya kimisri…karibuni sana, mmetujieni na furaha, Mungu abariki juhudi zenu kuhudhria mkutano  muhimu huo kuhusu: "Matatizo ya Fatwa katika zama za kisasa na matarajio yake katika siku zijazo", na anuani ya mkutano huo inaashiria kiwazi wazi udharura wa kuangalia hali halisi ya mambo yanayojiri kuhusu fatwa, na matatizo yake ambayo yangalisababisha mashaka mengi kwa waislamu.
Hakika –enyi waheshimiwa - nimepata kushughulika kwa fatwa kwa muda wa mwaka mmoja na nusu kabla ya hapo kwenye makao rasmi ya kutoa fatwa nchini Misri, mwanzoni mwa karne hii iliyoanza ikiwa na baadhi ya mizozo na matatizo, ambapo ilikuwa inaendelea vizuri kwa muda mfupi kisha hurudia nyuma kwa mizozo na migogoro wakati mwingine, na hali hiyo imebakia vivyo hivyo mpaka siku hizi, ikionya kutoka majanga na maafa, ambayo tumeshajua ishara zake mbaya, na tungali hatujui yaliyofichika katika siku zijazo na kupitia ghaibu.
Japokuwa sikuomba nipewe nafasi ya kuwa Mufti wala sikufikiria jambo hilo, lakini Mwenyezi Mungu amelitaka akalipitisha, na kwa kweli nilikuwa naogopa sana kuwa katika nafasi hiyo, sio kwa upande wa kielimu na kifiqhi ambapo kila mwanafunzi na mtafiti wa Al-Azhar katika kizazi change anayajua mambo hayo vizuri baada ya kusoma masomo ya kifiqhi kwa miaka tisa, akipokelea elimu hii mara tano kila wiki kwa muda wa masomo yake miaka tisa, lakini nilikuwa naogopa kuhalalisha la haramu au kuharamisha la halali, au kubana lililo wazi na sahili au kuruhusa lililokataliwa, na nilikuwa najituliza kwa hadithi ya swahaba mtukufu Abdul-Rahman Bin Samora, alipoambiwa na Mtume (S.A.W.): "Ewe Abdul-Rahman, usiombea utawala, kwani ukipewa baada ya kuuombea basi utakuwa kitu kigumu na hutaweza kuutekelez vizuri, ama ukiupewa bila ya kuuombea, basi utasaadiwa kuutekeleza vizuri".
Nilikuwa na ningali nafikiria sana madaraka hiyo iliyo muhimu sana katika maisha ya watu, kwani madaraka ya kutoa Fatwa ina shime kubwa nyoyoni mwa waislamu, na hisia za kuitakasa na kuiheshimu kwa hivyo neno linalotolewa na Mufti linamaliza mgongano au mzozo au kisita sita wo wote katika masuala yanayouliziwa, watu wangalipokea fatwa za wenye kutoa fatwa wanaoainishwa kama wanavyopokea dini sahihi ambayo haina wasi wasi, jambo linalofanya fatwa ni jukumu kubwa, na wajibu nzito anaiogopea kila mcha Mungu anayehofia kuhesabiwa na kuadhibiwa.
Na nilitambua katika masomo yango katika historia ya Fatwa na wenye kutoa fatwa kwamba wasi wasi na kuogopea kosa zilikuwa ni vifaa vya kimsingi vya Mufti, na sababu ya kutulia moyo wake, kuridhika kwa fatwa zote zinazotolewa naye, na majibu ya baadhi ya watu…vile vile mambo hayo mawili yalikuwa sababu kubwa ya kupoteza fatwa, baina ya kuwa na vurugu na kutojali, zikisita sita baina ya kubana na kutokuwa na uweano kwa madai ya kumcha Mungu, na kuwajibika kwa kufuata wahenga wema na fatwa zao kwa upande mmoja, na kwa upande mwingine baina ya kurhusu na kutokuwa na mipaka kwa madai ya kwenda sambamba na matukio ya kisasa na kuambatana na maendeleo, na kweli ni kwamba mbinu mbili ni mbaya kama anavyosema shairi wetu wa kikale….
Lakini hofu ile ilipelekea katika wakati mwingine kujiweka mbali na kuangalia vizuri fatwa kifiqhi, na kufuata mbinu rahisi isiyohitaji kujikalifisha kwa mashaka ya kutafuta jawabu la swali, na kujaribu kugundua hekima na dalili yake, na kulilinganisha na hali halisi ya mambo, mpaka baadhi ya fatwa zikawa katika masuala ya jamii ya kisasa – kwa kuhalalishwa au kuharamishwa – hazihitaji ila kutambua yaliyosemwa na wahenga kuhusu masuala yanayofanana nayo hata kwa kiasi kidogo, wakati ambapo mtafiti wa fatwa hizo hatakuwa na dalili isipokuwa baadhi ya mambo ya pamoja, au sababu dhaifu za kulingana baina ya masuala hayo na yale, ambazo hazizingatiwi katika kuyaunga masuala mawili yanayohusiana na fatwa yawe masuala yanayofanana yanayoafikiana katika hukumu na kanuni ya kiakili ambayo inasema kuwa: "hukumu ya masuala yanayofanana katika yanayohalalishwa na yanayoharamishwa ni moja", ikazoelewa kwamba fatwa nyingi ambazo zinakubali uwezeshaji na ugumu, zipewe hukumu iliyo kali ili kujikinga na kumwaasi Mwenyezi Mungu, na kwa sababu ya kuzuia visingizio na kuwafuata wahenga wema…japokuwa ugumu ambao mufti anaudhani ni kinga kwake mbele ya Mwenyezi Mungu, huo ndio ugumu uliokatazwa na Mtume (S.A.W), akitahadharisha nao katika hadithi yake takatifu: "Rahisisheni wala msifanyi ugumu" , akamwonya anayewasababisha umma kupatwa na mashaka kutoka moto na hasara, akamtamani kuadhibiwa katika hadithi sahihi: "Ewe, Mwenyezi Mungu mtu ye yote atakayewatawala umma wangu akawasababisha mashaka na maangamizi basi umtie mashakani makubwa"
Na sio sahihi kwamba ugumu ambao hadithi takatifu ilitahadharisha nao ni hasa kwa anayewasababisha watu mashaka katika maisha yao ya kila siku, bali unajumuisha pia yule anawasababisha kupatwa na mashaka kwa sababu ya fatwa ngumu ya kisheria inayowasababishia mashaka na kutabika, au inayowasababisha kupatwa na dhiki inayokataliwa na sharia.
Jambo lisilo na shaka ni kwamba hakuna baina ya wanaojishughulikia fatwa ila anayeihifadhi Qurani Mtukufu vyema na mambo ya msingi yaliyopitishwa na wenye fiqhi na wanavyuoni wa vyanzo vya fiqhi, kwamba hukumu inafungamana na sababu kuwepo au kutokuwepo, basi sababu ikikuwepo hukumu inakuwepo, ama sababu isipatikana hukumu haitapatikana, japokuwa hiyo fatwa ya masuala mengi ingalisita sita baina kuhalalishwa na kuharamishwa, ikiwaacha watu katika hali ya kutotulia na kutotumaini na mashaka.
Kwa mfano suala la zawadi za kumbukumbu zinazochorwa kama masanamu, au kujipatia pesa kutoka kazi la kuchora, tukijali tunayayaona hapo zamani na katika siku hizi kupitia televesheni kati ya kuyaangamiza mabaki ya kale yaliyo na thamani kubwa kihistoria katika uwanja wa sanaa ya kisasa, yameangamizwa kwa mujibu wa fatwa zinazojinasibisha kwa Uislamu na sheria yake, na hatusikii kwamba halmashauri ya kifiqhi ilipanga mkutano kwa kuhudhuria wana fiqhi wa zama hii na masheikh wa fatwa katika ulimwengu wetu wa kiislamu ili kubainisha hukumu ya kisheria kuhusu jambo hilo, na kutokana na mabadiliko ya kimataifa na desturi zilizoambatana kuanzisha vitivo vya kusoma historia ya mabaki ya kale, sanaa na utalii, jambo lililowasababishia waislamu utata kuhusu masanamu hayo: Je, masanamu hayo ni zawadi tu si haramu kuyahifadhi, au ni masanamu na najisi haijuzu kwa mwislamu ayahifadhi kamwe?!..Bali, wengi wa wanaojishughulikia fatwa wangalisema kuwa jambo hilo ni haramu kabisa, japokuwa itakuwa bora zaidi kuangalia na kuchunguza sababu kabla ya kutoa hukumu ambayo inatolewa haraka na bila ya kuchunguza kama ni hukumu ya ibada, na maagizo ya sheria kwetu, basi lazima tutekeleze bila ya kufahamu maana na sababu zake, na wala ni hukumu zinazotegemea sababu ambazo zinafungamana kuwepo au kutokuwepo…na kuharamisha kuunda masanamu katika enzi za mwanzo wa Uislamu -aghalabu- kulikuwa na sababu ya kwamba desturi za waarabu wakati huo ambapo walikuwa wanaabudu masanamu na wanayaunda, wakiyafanya miungu badala ya Mwenyezi Mungu, na ilikuwa inatarajiwa kwamba sheria safi itaharamisha kuyaunda masanamu, ili kuzuia sababu ya kuenea ushirikina, na kuilinda dini mpya ambayo inaombea "upewke-Tawhiid" basi, ni nini sababu ya kuharamisha sasa baada ya kuenea Uislamu na kuimarishwa vyema na kukubaliwa na akili, nyoyo na hisia z wanadamu, na ibada ya masanamu imetweka katika nyumba za waislamu wote!!, sisi sote tunajua kwamba waislamu wamepitiwa na mnamo karne kumi na tano Hijria, hatukusikia au kusoma kuwa mwislamu mmoja ameliabudu sanamu badala ya Mwenyezi Mungu, akilifanya mshiriki wa Mwenyezi Mungu, kisha akajidai Uislamu, basi hilo ni jambo lisilokubaliki kabisa kutolewa na mwislamu anayetamka shahada mbili, bali ni jambo lisiloweaekana kwa dalili zifuatazo: Mtume (S.A.W.) ametupa matumaini kabla ya kufariki, akaapa kwa Mwenyezi Mungu kuhakikisha hilo, akasema katika hadithi mtukufu, ilisimuliwa na Bukhari  na Muslim  kutoka Oqba Bin Amer kwamba Mtume (S.A.W) ametoka siku moja akasali {akawaombea} jamaa wa mtu mmoja kama anavyosali juu ya maiti kisha akaondoka kwa minbari akasema: "Nitawatangulieni kufariki, na mimi ni shahidi juu yenu, na mimi kwa kweli nikiapa kwa Mwenyezi Mungu natazamia bonde langu hivi sasa, na hakika nilipewa funguo za hazina za ardhi au funguo za ardhi, na hakika mimi nikiapa kwa Mwenyezi Mungu siwaogopeeni wawe washirikina baada yangu, lakini nawaogopeeni kushindana kwa ajili yake", {kwa maana ya: Dunia}, na kwa mujibu wa kiapo kitakatifu cha Mtume (S.A.W) basi, madai ya baadhi ya wavukaji mipaka ya kwamba wanawaogopea waislamu wawe washirikina yakawa madai matupu, na machafuko yanayopoteza pesa, juhudi na wakati, ujiepushe na athari mbaya zaidi za kueneza fitina baina ya waislamu, na kuzidisha migongano na hitilafu baina yao.
Hakika mimi naamini kwamba ni haki ya mwislamu juu yenu – waheshimiwa wenye ijtihad na fatwa – myaangalia upya masuala hayo na yanayofanana nayo, ikipatikana dalili wazi lisiliokubali kubadilishwa, basi hakuna nafasi ya kuangalia upya au kujitahidi kwa maoni hasa, na mwislamu katika wakati huo hana budi ila asikilize vizuri na kuwajibika kwa amri za Mwenyezi Mungu na Mtume wake (S.A.W) akiwa radhi..na isipopatikana dalili kama hiyo basi jukumu linalazimika kurahisisha kwa waislamu wa zama hii, sharti isipingana na makusudio la kisheria na kanuni ya kijumla, mbali sana na kuiga bila ya kufikiri na kuwajibika maana dhahiri ya matini tu bila ya kutambua ishara za kurahisisha na kuondoa dhiki na kuangalia hali, ambapo zinaambatana na masuala hayo, lakini yanahitaji anayezigundua na kuziainisha katika hali halisi ya maisha ya watu.
Na nyinyi – Enyi waheshimiwa mnaopewa nafsi ya kutoa fatwa - hamna haja ya kukumbusha kuwa kutozingatia vyema kwa fatwa za ukafirishaji, kudai kupotea kidini na kuwa na bidaa, na kuchagua fatwa zisizojulikana ambazo zinaimarisha fatwa hizo katika masomo ya kale yetu, haya yote yamepelekea mnayoyaona kati ya mauaji na umwagaji damu pasipo na haki kwa madai ya ukafirishaji na kutoka kwa dini.
Jambo jingine limenivutia, nalo ni suala la "Urf - Desturi" ambalo lina hatari kubwa katika kubadilisha fatwa na kuingia kwake katika uwanja wa ugumu na ukali, na sababu kuu la hatari hii ni kwamba kanuni ya "kubadilika kwa fatwa kutokana na kubadilika kwa desturi" ikawa kanuni lisilozingatiwi sana au inayotekelezwa kwa nadra katika fatwa, na ikitekelezwa huzingatia desturi hasa ya nchi maalumu, kwa ajili ya kuwa na fatwa za pamoja, vivyo hivyo, katika nchi nyingine ambayo haina desturi hiyo, jambo lililosababisha fujo na machafuko kwa raia, wakati wanavyuoni wa nchi fulani wanapojaribu kutoa fatwa isiyoambatana na sheria lakini inafungamana na desturi na mila zao, jambo linazidi kuwa mbaya wakati wa kuzuka mgawanyiko baina ya pande mbili, wa kwanza wanafuata fatwa ya nchi yake ilhali wa pili wanafuata fatwa ya nchi nyingine, na jambo halitasimamia kuchagua fatwa hii au ile tu, bali litageuka ukawa kila upande unazingatia kwamba upande mwingine unafuata fatwa iliyo kosa, na pengine watabadilishana tuhuma ya kuwa wapotovu na wenye bidaa, au wenye mawazo makali, na sababu ya janga hilo ni kufaradhisha fatwa iliyotolewa na desturi hasa katika nchi fulani, juu ya nchi zisizojua desturi hiyo kabisa.
Sheikh wetu wana wa fiqhi na vyanzo mhakiki, mwanachuoni mheshimiwa; Ahmed Fahmy Abu Sennah katika kitabu chake cha pekee katika kuelezea mtazamo wake kuhusu sheria ya kiislamu kwa anuani wa: "Desturi / Urf na mila kwa maoni ya wanafiqhi" amepitisha kwamba Urf ni chanzo cha kisheria katika kujenga sheria ya kiislamu, na hayo baada ya kuamini kuwa desturi za watu na mila zao zinabadilika kutokana na hali zao, na hii ni utangulizi wa kwanza usiokubali utata wala hitilafu, kisha sheikh huyu akaongeza utangulizi wa pili ambapo ameainisha msimamo wa sheria kuhusu desturi hizo akisema: "sheria ikitoa hukumu moja inayofafanuliwa kuhusu desturi hizo, basi watu wangepata mashaka na taabu, na watatoka nje ya makusudio ya Uislamu ambao umejengewa maslahi za waja…{Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote} (Al-Anbiyaa: 107), na sheria ikitoa hukumu nyingi kuhusu desturi hizo, basi maslahi hizo zinazobadilika na hali zinazotofautisha, basi wajibu za watu zitakuwa nyingi, na katika hali watu wangepata mashaka kwa masharti na kanuni zake, kinyume na sheria ambayo kimsingi imejengwa msingi muhimu wa (uchache wa wajibu/ makalifisho) kwa hiyo hekima ya Mwenye hekima na ujuzi zaidi ililazimika kupitisha hukumu za kijumla zisizo na ufafanuzi, bila ya kujali kubadilika hali au muktadha, ikiwaombea wajuzi wa kufananisha hukumu na matukio (wenye ujuzi wa kutumia Qiyas) wafafanue hukumu hizo, na hilo ni lango kubwa kutoka milango ya desturi unaojengewa sehemu kubwa ya hukumu, na hakuna mwanafiqhi aukana hata mmoja, nao pia ni hoja thabiti na dalili wazi juu ya utukufu wa sheria na kutakasika kwake, na kwamba sheria hiyo ya kiislamu inafaa mahali po pote na wakati wo wote".
Jambo jingine analiongeza sheikh mheshimiwa katika kubainisha hekima ya uzingatio wa sheria kwa chanzo za "Urf" nalo ni kwamba sheria imezingatia kuchunga Urf unaofaa, katika yaliyotungwa kwa watu na sheria kati ya hukumu tofauti ili iwe rahisi kwa watu wazifahamu na kuzitekeleza maishani mwao, na wala wasiwe na dhiki kwa sababu ya ugumu wa kuzitekeleza, basi kwa hiyo urf ulio sahihi ikawa na nafasi na athari kubwa katika sheria ya kiislamu.  
……………………………………………………..
Na niliyoyataja – Enyi mabwana – kuhusu suala la kutunza masanamu sio la pekee kuhusiana na maisha ya waislamu katika karne ya kumi na tano Hijria, bali kuna masuala mingine mengi ambayo yanatofautiana katika umuhimu wake kulingana na maisha ya watu, na baadhi yake ni masuala ya kimsingi, na baadhi nyingine hayana umuhimu wo wote, lakini yametumiwa ili kutoleza fatwa kali zilizowashawishi waislamu wasichukua nafasi yao kati ya mataifa, Je, la kubalika kiakili - kwa mfano – suala la mwanamke kushughulikia mambo ya ujaji – na masuala mingine – yawe sababu ya tofauti kubwa, wakati ambapo mwanamke akawa afisa, mwendeshaji wa ndege, profesa wa chuo kikuu na waziri katika serikali…je masuala ya mwanamke katika desturi hizo zinazobadilika yangali hayo hayo ya masiku ya kuwahukumia wanawake wabaki hemani na majaumba?!
Enyi mabwana wanavyuoni!
Sitaki kuzungumza mengi nisiwatabisheni, lakini mna jukumu kubwa, na aghalabu ya maumivu wa watu na matatizo ya familiya na nyumba zilizoharibika yalikuwa kwa sababu ya fatwa kosa, na hukumu zilizotegemea desturi zinazofaa mazingira fulani lakini hazifai katika mazingira nyingine, au zilitegemea desturi kale zilizobadilika mara nyingi, na fatwa zilizojengewa na desturi hizo zingalitumiwa kikamili, kama sheria imesimama katika enzi maalum, na katika mazingira ya kijiografia maalum..
Kisha fatwa hizo za kigeni kwa mahali na wakati ni nini msimamo wake kutoka tuliyoyahifadhi vyema kati ya kauli yake Mwenyezi Mungu (S.W.): {Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yo yote ila kwa kadiri ya iwezavyo} Al-Baqara: 286. Na {Hapendi Mwenyezi Mungu kukutieni katika taabu} Al-Maidah: 6. Na kauli yake: {Wala hakuweka juu yenu mambo mazito katika Dini} Al-Hajj: 78. Na hadithi ya akina mama wa waumini Bi; Aisha (R.A.): "Mtume (S.A.W.) hakuombewa kuchagua baina ya mambo mawili ila huchagua jambo rahisi zaidi isipokuwa ni dhambi" , bali ni nini msimamo wa fatwa hizo kutoka yaliyosomwa na wakubwa wa fiqhi na vyanzo vyake katika kuchunguza masharti na kanuni za kurahisisha kama vile:
1.    Desturi iliyopitishwa.
2.    Mashaka huleta kurahisisha.
3.    Jambo likibanwa hubanuka.
4.    Lililopitishwa na desturi ni kama lililowekwa masharti.
5.    Kubadilika fatwa kwa kubadilika mahali, wakati, hali na watu.
Mwanafalsafa wa madhehebu ya fiqhi ya Malik imamu Shihabu-Din Al-Qarafy Al-Misry ana maneno mazuri sana ya kujitenga na hatima ya fatwa na wenye kutoa fatwa katika kitabu chake "Udhibiti katika kuzitenga fatwa na hukumu na matendo ya kadhi na imamu" ambapo amesema: "Mufti apaswa akijiwa na mwombaji fatwa na hajui akiwa ni mmoja wapo wa raia wa nchi yake, asimpe fatwa yake ya kawaida kuhusu jambo hilo mpaka ajue nchi ya mwombaji fatwa huyu, na akiwa ni mgeni kutoka nchi nyingine amwulize wana desturi maalum nchini mwake kuhusu tamko hilo au la? Na likiwa tamko linajulikana nchini mwake amwulize je, desturi ya nchi ile inaambatana na desturi ya nchi hii kuhusu tamko hilo au la? Na hilo ni jambo la lazima kwa maulamaa wote, na kwamba tabia mbili zikiwa katika nchi mbili tofauti katika desturi zao, basi hukumu zao hazitakuwa sawa".
Pia anasema katika kitabu chake "Al-Forouq- tofauti": "Basi, jambo lo lote linalobadilishwa katika desturi lazima mufti alikubali, na linaloondolewa aliondoa, na wala usitosheleze na yaliyoandikwa vitabuni kamwe, bali, ukijiwa na mtu mgeni wa nchi yako akikuuliza fatwa: basi uaitendeana naye kwa mujibu wa desturi ya nchi yako, bali umwulize juu ya desturi za nchi yake na umtendeane kutokana na desturi ya nchi yake kisha umpe fatwa bila ya kujali desturi ya nchi yako na yliyomo vitabuni mwako. Basi hii ndiyo haki iliyo wazi, na kutosheleza kwa matini kwa milele ni upotofu katika dini, na ujinga kwa malengo ya maulamaa wa waislamu, na wahenga wema waliotangulia".
Enyi mabwana wakati umekuja ili tufufue vito ghali kama hayo (mafundisho ya kale) katika mabaki yetu ghali, na tuyasafishe kutoka uzembe ambao uliwanyima watu urahisi wa sheria na rehema yake, na tutumie maelezo hayo katika kila linalohusiana na fatwa, ambapo maelezo hayo peke yake ndiyo yanayoweza kuwahimiza watu wajilazimike na hukumu za sheria takatifu, nayo peke yake yanayoweza kulinda mwana fiqhi na mufti kutoka kuwataabisha watu na kuwalazimisha kutekeleza hukumu nzito, nayo pia yanayoweza kuhifadhi kutoka fujo wa fatwa ambayo inasababisha kuhalalisha la haramu na kuharamisha la halali na kuwahimiza watu wasiogope na dini.
Enyi mabwana nasikitika sana nikiwatabisheni kwa hotuba yangu ndefu, na ninatumai kwa mkutano wetu huu uwe mwanzo mzuri kwa enzi mpya ya fatwa kwa kupanga mambo muhimu vizuri, na kuchunga desturi na malengo ili tuweze kupambana na hali halisi na matatizo yake na mambo mapya yanayotushuhudia kwa fatwa zinazoimarisha jamii zenye amani na usalama zikitawaliwa na sheria yenye msamaha inayofaa kila wakati na mahali.

Shukrani sana kwa kunisikiliza vizuri
Assalamu Alykum Warahamatullahi Wabarakatuh
Imeandikwa katika Al-Azhar Al-Shareif
Tarehe: 1 Dhul-Qe'ada 1436 H.J.
   16 Agosti 2015 B.K.

Sheikh Mkuu wa Al-Azhar
Ahamed Al-Tayyib

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.