Uislamu wahimiza kushirikiana baina ya dini na tamaduni mbalimbali kwa ajili ya kuilinda heshima ya mwanadamu na kuzitetea haki zake

  • | Friday, 7 August, 2015
Uislamu wahimiza kushirikiana baina ya dini na tamaduni mbalimbali kwa ajili ya kuilinda heshima ya mwanadamu na kuzitetea haki zake

Hakika sisi tunaishi katika ulimwengu ambao maslahi za umma zimeingiliana, haikubaliki kwa umma fulani kuishi mbali na umma  zingine, kwa hivyo sisi tunahitaji misingi wazi tunaifuata katika uhusiano wetu pamoja na wengine kwa njia inahifadhi maslahi zetu bila ya dini yetu kuathiriwa.
Hakika Uislamu una mtazamo wazi kuhusu njia za uhusiano baina ya umma, jamii, staarabu zingine, na Qurani imebainisha kwamba uwingi na utofauti ni ishara kutoka ishara za Mwenyezi Mungu ( Na katika Ishara zake ni kuumba mbingu na ardhi, na kutafautiana ndimi zenu na rangi zenu. Hakika katika hayo zipo Ishara kwa wajuzi). {Al ruum:22}.
Uwingi au utofauti huo kwa watu wengi kama ilivyotajwa katika aya ni lazima kujengwa juu ya msingi wa (kujuana) kwani mwanzo wa msingi huu ni Qurani tukufu kama Alivyosema Mwenyezi Mungu (Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane.){Al Hujuraat:13}.
Wanahistoria wa magharibi wamejua kwamba: kutoweza  ustaarbu fulani unajengwa kwa umma maalumu bali unajengwa kwa ushirikiano pamoja na umma tofauti.
Hakika anayeangalia na kuichunguza aya hiyo anatubainisha ukweli kamili wenye pande za kiutu kwa ujumla, na kupitia kwa aya hiyo amepata maana tunaweza kuitwa (kujuana kwa staarabu) na kujuana ni maana ambayo aya ya Qurani imetaka kuiainisha na kuikaza, na aya ilikuwa inawazungumza (watu wote) kwa aina zao, hitilafu za ndimi zao, rangi zao, asili yao, kwani asili ya watu wote ni asili moja ya kiutu.
Ni lazima watu wajue kwamba ukweli huo ni msingi wa kiutu na kimaadili katika mtazamo wao kwa nafsi zao, na katika mtazamo wa kila umma na ustaarabu kwa mwengine kama wao ni familia moja. Kwa hakika kujuana kwa staarabu haimaanishi kukubali tu kwa uwingi wa staarabu na aina zake, bali inategemea udharura wa kujenga na kuendelea staarabu ulimwenguni, na kuanzisha ushirikiano wa ustaarabu baina zake, na kubadilishana ujuzi na kujuana, kwani ulimwengu hauhitaji ustaarabu moja, bali unataka maendeleo ya staarabu zote.
Waislamu wametaka kutekeleza mielewoko ya kiislamu hiyo kupitia ushirikiano kati ya ustaarabu wa kiislamu na staarabu zingine na kuathiri na kuathirika na ushirikiano wa ustaarabu uliofanywa, na mawasiliano ya kiilimu baina ya mashariki na magharibi na faida za pande mbili, na mengine yaliyopelekea kutekeleza aya ya Qurani kwa ajili ya kubainisha umuhimu wa kushirikiana na kufanya pamoja kwa ajili ya kuhudumu maslahi za kiutu na kueneza utamaduni wa kuishiana pamoja katika amani.

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.