Imamu Mkuu katika mkutano wake na waziri wa ulinzi wa Ufaransa :Tunaheshimu msaada wa kudumu wa Ufaransa kwa Misri…..na ugaidi hauhusiani na eneo letu la kiarabu tu bali umepindukia ulimwenguni kote

  • | Monday, 27 July, 2015
Imamu Mkuu katika mkutano wake na waziri wa ulinzi wa Ufaransa :Tunaheshimu msaada wa kudumu wa Ufaransa kwa Misri…..na ugaidi hauhusiani na eneo letu la kiarabu tu bali umepindukia ulimwenguni kote

Mheshimiwa Imamu mkuu wa Al-Azhar Al-Shareif profesa; Ahmed Al-Tayyib alikaribisha leo asubuhi waziri wa ulinzi wa kifaransa Jane Eve Lordian, na ujumbe wanaoambatana naye, ili kutambua mtazamo wa mheshimiwa imamu mkuu kuhusu matukio yanayojiri kwa pande tofauti za kienyeji na kimataifa.
Mheshimiwa imamu mkuu alisema: kwa hakika Al-Azhar Al-Shareif inaheshimu msaada wa kudumu wa Ufaransa kwa Misri, hasa hasa msaada wake wa daima kwa vikosi vya kijeshi vya kimisri na kupigana na tatizo la siasa kali na ugaidi ambalo linaenea kama kansa, na tunatamani ushirikiano zaidi baina ya nchi mbili katika fremu hiyo, akiongeza kwamba Al-Azhar inahifadhi husiano za kielimu na kitamaduni na Ufaransa ambapo viongozi wa Al-Azhar wamepata masomo yao katika vyuo vikuu vikubwa vya kifaransa.
Yule mheshimiwa amesisitiza kuwa ugaidi hausimami kwenye mipaka ya eneo letu la kiarabau tu bali umepindukia kufikia ulimwenguni kote jambo linalohitaji kupambana nao kwa pamoja, sio mapambano ya kiusalama tu, bali ni lazima kufanya kazi ili kuwakinga vijana kutoka hatari ya mawazo makali, akiashiria kwamba Al-Azhar ni tayari kuwapa maimamu wa Umoja wa Ulaya, na hasa wa kifaransa mazoezi, kulingana na programu maalumu ambayo inatosheleza mahitaji ya jamii zao na kuimarisha maegemeo na kuzuia kuwavutia na kuwapa matayarisho kupambana na matatizo ya kisasa na kuwafundisha Uislamu sahihi ambao Al-Azhar inaufundisha tangu zaidi ya miaka elfu moja.
Mheshimiwa ameeleza kuwa Al-Azhar imechukua hatua za kikweli katika miaka ya mwishoni katika kuporesha mawazo na sayansi za kiislamu, ambapo aliangalia upya katika mitaala yake amabayo inafundishwa katika vipindi tofauti vya elimu jambao linalodhamini kuunda kizazi kinachoweza kubeba ujumbe safi wa Al-Azhar kwa ulimwengu wote, ikaanzisha kituo cha uangalizi kwa lugha za kigeni ili kuangalia kila vinayoyatoleza vikundi vya kigaidi vyenye silaha kutoka mawazo makosa kuhusu Uislamu na ikajibisha mawazo hayo, na kwa upande mwinginie Al-Azhar inawasiliana na ulimwengu wa nje kupitia kuanzisha matawi ya Muungano wa Wasomi wa Al-Azhar ili kusambaza ujumbe wa Al-Azhar katika nchi kadhaa ulimwenguni, na kutuma misafara ya kueneza amani kwa kushirikiana na Baraza la waislamu wenye hekima chini ya uongozi wa mheshimiwa imamu mkuu kwa nchi tofauti duniani barani Ulaya, Asia, Afrika na Marekani kwa lengo la kuimarisha usalama katika jamii na kueneza utamaduni wa kusameheana na kuishi pamoja, licha ya ziara kadhaa za mheshimiwa imamu mkuu kwa baadhi ya miji mikuu barani Ulaya kwa lengo la kusisitiza kwamba usalama ndio ujumbe wa dini zote za angani, yule mheshimiwa alimpa waziri wa ulinzi nakala ya ripoti iliyoandaliwa na msafara wa usalama uliofanya ziara kwa Ufaransa hapo karibuni.
Kwa upande wake waziri wa ulinzi wa Ufaransa alielezea shukrani zake na furaha yake kwa kukutana na mheshimiwa imamu mkuu, akielezea heshimu yake kwa Al-Azhar Al-Shareif na imamu wake mkuu kwa sababu cheo kikubwa cha Al-Azhar ulimwenguni kote, na kuridhi kwake kwa mtazamo wa imamu kuhusu matukio yanayojiri ulimwenguni.
Waziri wa ulinzi wa Ufaransa alisistiza kwamba kuna uhusiano wa kihistoria baina ya Misri na Ufaransa ambao unazingatia ushirikiano na maslaha ya pamoja, akiongeza kwamba Ufaransa inazingatia kuwa Misri ina roli ya kimsingi katika usalama wa eneo, na kwamba Misri inahitaji sana mitaala ya Al-Azhar ya kiwastani ambayo inaonyesha mafundisho ya kusamhehana ya Al-Azhar, na inahitaji pia michango ya Al-Azhar katika uwanja wa kuwatarisha maimamu wa kifaransa na kuwapa uzoefu wa kupambana na mawazo ya kigaidi ambayo Uislamu unayakataa, akiheshimu utashi wa Al-Azhar kuwaelimisha maimamu  barani Ulaya.
Mwishoni mwa mkutano waziri wa ulinzi wa Ufaransa aliashiria kuwa atamfahamisha raisi wa Ufaransa ambaye atahudhuria sherehe ya ufunguzi wa mfereji mpya wa Suze, na kwa waziri wa mambo ya mdani wa Ufaransa kwa kuwa yeye ni mhusika wa moja kwa moja juu ya maudhui hiyo mjadala uliofanyika kuhusu kuelimisha maimamu wa kifaransa katika A-Azhar.

Print
Tags:
Rate this article:
3.0

Please login or register to post comments.