Al-Azhar Al-Shareif yamwomboleza Prince Soud Al-Faysal..

  • | Saturday, 11 July, 2015
Al-Azhar Al-Shareif yamwomboleza Prince Soud Al-Faysal..

Na inasisitiza kuwa: historia itakumbuka kwa milele misimamo yake ya kihistoria kuhusu masuala ya Umma zake mbili: ya Kiarabu na ya Kiislamu

 

Kwa imani thabiti kwa majaliwa ya Mwenyezi Mungu na Kadari yake, Al-Azhar Al-Shareif na Imamu wake mkuu Profesa; Ahmed Al-Tayyib, Sheikhi mkuu wa Al-Azhar Al-Shareif yamwomboleza Prince Soud Al-Faysal Bin Abdul-Aziz Al Soud, waziri wa mambo ya nje wa zamani wa Ufalme wa Uarabuni wa Saudia, ambaye alifariki jana jioni baada ya kupatwa na maradhi.  
Al-Azhar Al-Shareif inasisitiza kwamba historia itakumbuka uaminifu wake na misimamo yake ya kihistoria yenye ujasiri kuhusu masuala ya Umma zake mbili: ya Kiarabu na ya Kiislamu, na kwamba haiwezekani kwa mwarabu au mwislamu ye yote kusahau busara na uzoefu wake wa kidplomasia uliochangia maendeleo na ustawi wa Ufalme wa Uarabuni wa Saudia, na kusaidia na kuleta utulivu ulimwenguni mwa Kiarabu na Kiislamu, na pia kwamba wamisri hawawezi kusahau misimamo yake ya kihistoria katika kusaidia na kuunga mkono Misri.
Na Al-Azhar Al-Shareif; wakati wa kumwomboleza marehemu wa Umma – inatolea rambirambi kwa Mlezi wa Misikiti miwili mitakatifu Mfalme/ Salman Bin Abdul-Aziz, Mfalme wa Ufalme wa Uarabuni wa Saudia, na kwa ukoo wa Al Soud wote, na kwa raia ndugu wa Kisaudia, ikimwombea Mwenyezi Mungu – mwenye nguvu zaidi – Amrehemu na Ampe marehemu maghufira, na Amwingize peponi mwake, kwa ajili ya kumlipiza juhudi zake katika kuhudumia Uarabu na Uislamu, na Aihifadhi Ufalme wa Uarabuni wa Saudia na umma mbili: ya Kiarabu na ya Kiislamu kutoka kila shari na mabaya.

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.