Imamu Mkuu katika mkutano wake na Askofu wa Kanisa la Kiinjili mjini Berlin, Ujerumani

  • | Friday, 18 March, 2016
Imamu Mkuu katika mkutano wake na Askofu wa Kanisa la Kiinjili mjini Berlin, Ujerumani

Imamu Mkuu katika mkutano wake na Askofu wa Kanisa la Kiinjili mjini Berlin, Ujerumani:

•    Ziara yangu mjini Berlin inalengea kuhuisha uhusiano wa kudumu baina ya dini mbili Uislamu na Ukristo.
•    Ni lazima kuanzisha mahusiano ya kirafiki baina ya wanavyuoni wa dini ya kiislamu na wakuu wa dini ya kikristo kabla ya kufikiri kuhusu kueneza amani na usalama baina ya mashariki na magharibi.

Mheshimiwa Imamu Mkuu profesa; Ahmad Al-Tayyib Sheikhi mkuu wa Al-Azhar alikutana na Askofu Markous Drogeh Askofu wa Kanisa la kiinjili mjini Berlin.
Katika mkutano huu, Askofu wa Kanisa la kiinjili mjini Berlin alieleza furaha yake kwa ziara ya kihistoria ya Imamu mkuu nchini Ujerumani, akisisitiza kwamba ziara hiyo inazingatiwa maendeleo makubwa yanayoimarisha mazungumzo baina ya dini na kueneza maadili ya kusameheana.
Askofu Drogeh alisisitiza pia heshima yake mkubwa kwa Mheshimiwa Imamu Mkuu na roli yake katika kueneza ujumbe wa amani kwa ulimwengu wote, akiashiria kwamba kuna mahusiano makubwa baina ya kanisa la kiinjili mjini Berlin na kanisa la kikoptiki nchini Misri, akitoa mwaliko kwa Sheikhi mkuu wa Al-Azhar ili ashiriki katika kuanzisha jumuiya nchini Ujerumani itakayokusanya dini tatu za mbinguni, akampa Imamu Mkuu zawadi iliyo ni kitabu kinachozungumzia wazo la kuanzisha jumuiya hiyo.
 Kwa upande wake, Mheshimiwa Imamu mkuu alisisitiza kuwa alikuja mjini Berlin sio kwa ajili ya kutafuta uhusiano mpya unaotazamiwa kuziunganisha dini mbili Uislamu na Ukristo, akitilia mkazo imani yake kwamba kuanzisha mahusiano ya kirafiki baina ya wanavyuoni wa dini ya kiislamu na wakuu wa dini ya kikristo kabla ya kufikiri kuhusu kueneza amani na usalama baina ya mashariki na magharibi.
Yule Mheshimiwa akaongea jaribio la "Baytul A'ila" jumuiya ya kuwaunganisha waislamu na wakristo miongoni mwa wamisri iliyoanzishwa na Al-Azhar Al-Shareif na Kanisa la Kikoptiki la Kimisri, vile vile alisifu madokezo ya Askofu mjerumani kwa ajili ya kuanzisha jumuiya ya dini tatu mjini Berlin, akisisitiza kuwa Al-Azhar iko tayari kutoa misaada ya lazima ili kutekeleza jambo hilo.


 

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.