Hotuba ya Imamu mkuu Profesa; Ahmad Al-Tayib Sheikhi mkuu wa Al-Azhar Al-Shareif nchini Indonisia

  • | Wednesday, 24 February, 2016
Hotuba ya Imamu mkuu  Profesa; Ahmad Al-Tayib Sheikhi mkuu wa Al-Azhar Al-Shareif nchini Indonisia

kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema Mwenye kurehemu

Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, swala na salamu zimfikie Mtume wetu Mohammad (S.A.W.) pamoja na jamaa zake na maswahab wake wote….

Enyi hadhira watukufu!!!

Assalamu Alykum warahmatul-lahi wabarakatuh….kisha,

Naanza hotuba yangu kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu na kumsifu kwa sifa njema zote anazozistahiki, kwa kuturahisisha mimi na ujumbe wanaoambatana nami kutoka Al-Azhar Al-Shareif na kutoka baraza la wakuu wa waislamu kufanya ziara hiyo kwa Jamhuri ya Indonisia, na kukutana na raia wake kwa migawanyiko yake yote, na hasa ndugu zetu waislamu, raia hawa wapendwa sana na wanaopewa heshimu kubwa na Misri na wananchi wake kwa sababu ya waindonisia wana roli muhimu sana katika Ummah wa kiislamu na wana athari dhahiri katika historia ya Uislamu na waislamu, na wanaosifika kwa ikhlas katika kushikamana na Uislamu: itikadi yake, matendo yake na matumizi ya sheria yake iliyo bora zaidi.

Na bila ya kuwasifueni zaidi - enyi wananchi wa Indonisia wenye sifa njema- nikisema: kwa kweli Mwenyezi Mungu Ameipa Indonisia uwezo usio na mfano juu ya kutanguliza Uislamu kwa ulimwengu wote kama ni dini inayolingania furaha ya dunia na akhera, dini inayochanganya makuu kuu kwa ubora wake na mapya kwa uzuri wake, na inayoambatanisha mahitaji ya kila mmoja na maslahi za jamii.

Taifa hilo la Indonisia waliweza kugundua vitu vya thamani vya Uislamu mtukufu, na maadili mema yake ya kisheria na ya kitabia, na kuainisha yaliyopo ndani ya dini hiyo kati ya maadili kama vile: uadilifu, usawa, kukubaliana na mwingine, kuchochea kumiliki vyanzo vya nguvu na sababu za maendeleo ya kisayanasi na kiteknolojia, na kumtegemea Mwenyezi Mungu katika matamanio ya kumiliki nguvu hizo za kiroho na kimada.

Mchanganyiko huu baina ya imani, elimu na kufanya kazi umeifanya Indonisia iweza kuwa mwanzoni mwa nchi enedelevu katika eneo hilo la Asia, ikawa "chui"[1] mojawapo "chui" wa Asia kupitia kwa kujitahidi sana na kusaka maendeleo, ikatoa mifano bora zaidi kwamba Uislamu ndiyo dini ya dunia na akhera, na dini ya maisha na utu mzima. Vile vile nchi hiyo imeweza kubatilisha madai ya maadui wa Uislamu kwamba dini hiyo ni dini ya uvivu, kuwategemea wengine, kurejea nyuma kijamii, na kwamba dini hiyo inachelewesha maendeleo ya kiuchumi na ya kisiasa, kwa kutumia dalili na hoja za kimatendo, bali kinyume Indonisia ikawa hivi sasa mfano wa kuiga jambo la kufurahisha sana kwa waislamu, kwa sababu ya maendeleo ya uchumi wa nchi hiyo uliofika kiwango cha juu katika eneo la kaskazini mashariki barani Asia.

Wananchi wa Indonisia wameukaribisha ujumbe wa Uislamu uliowafikia kupitia kwa wafanyabiashara waislamu, ujumbe ulioafikiana na tabia asili ya watu wa visiwa hivyo (Arkhabil) ambapo wamesifika kwa upole, utulivu wa moyo, wema, na kupendelea amani na usalama, pamoja na sifa nzuri sana za itikadi ya Uislamu na sheria yake kati ya uwazi, uadilifu na usamehevu.

Maeneo ya "Nosantara" yalikuwa ya kwanza kupokea Uislamu katika enzi hiyo, kisha Uislamu ukaenea na ukapanua mpaka Indonisia ikawa nchi ya kiislamu iliyo kubwa zaidi duniani kwa idadi ya waislamu wanaoishi nchini humo, na inayosifika kwa mapenzi makubwa zaidi kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake (S.A.W.), kitabu chake, na sheria na hukumu zake.

Ama kuhusu uhusiano uliopo baiana ya wananchi wa nchi mbili: Misri na Indonisia, basi baadhi ya wanahistoria wanasema kwamba uhusiano huu unarejea wakati kale sana, kisha uhusiano huo ukaendelea kupitia karne ukawa uhusiano wa kibiashara, kisayansi na kitamaduni, baadhi ya mahujjaji waindonisia walikuwa wanakaa baada ya kumaliza amali za Hajj mijini mitakatifu ya Makkah na Madinah, ili wajifunze elimu ya kidini wakifundishwa na walimu wa Al-Azhar na maulamaa wake, wanahistoria wa kiulaya walithibitisha kwamba miaka ya hamsini katika karne ya kumi na tisa imeshuhudia kufika na kukaa kwa kundi la kwanza la waindonisia walioamua kuishi nchini Misri, ambao walikuja kwa ajili ya kusoma katika Al-Azhar Al-Shareif kupitia kwa maulamaa na masheikhi wake, wanafunzi wa kundi hilo walikaa katika sehemu maalum kati ya sehemu za Al-Azhar iliyopewa jina lao nalo ni: sehemu ya Al-Gawi, na machapisho ya Kairo yalikuwa yakichapisha vitabu vya maulamaa wa dini wa Indonisia, vile vile waindonisia waliathirika kupitia kwa wana wao waliokuwa wakisoma na kukaa katika Al-Azhar kwa taharuki za uboreshaji wa mawazo na fikira za kiislamu nchini Misri zilizoongozwa na Imamu Mohammad Abdo na wanafunzi wake baadaye, na taharuki za kitaifa zilizoongozwa na Mostafa Kamel na viongozi wa chama cha kitaifa wakati ule.

Na hivi sasa kuna zaidi ya wanafunzi waindonisia elfu tatu na mia tano wanaosoma katika Al-Azhar Al-Shareif, miongoni mwao wanafunzi mia mbili sitini na mbili wanaosoma bure, na Al-Azhar inatolea kila mwaka tuzo za masomo ishirini kwa wanafunzi wa Indonisia, vile vile idadi ya walimu wa Al-Azhar waliosafirishwa Indonisia imefika walimu thelathini na moja.

Enyi watukufu mlio hadharani!!

Pengine sio la msingi kusema kwamba ulimwengu wetu wa kisasa unapitiwa na matatizo makubwa mengi: kisiasa, kiuchumi na kimazingira, na labda tatizo kubwa zaidi kuliko kwa nchi za ulimwengu wa tatu na mataifa wake ni tatizo la usalama na amani kwa nafsi, heshima, mali, nchi, na kuenea ghasia na fujo, usaliti, kuvunja huruma za wanyonge. Na tatizo lililo gumu zaidi ya hayo ya juu kufanya ukiukaji na jinai za kikatili zinazofanywa hivi sasa kati ya mauaji na umwagaji damu kwa jina la dini, na hasa dini ya "Uislamu" peke yake, mpaka "Ugaidi" ukawa jina la pekee la dini hiyo na sifa hasa kwayo ambapo hakuna dini nyingine kati ya dini tatu za mbinguni inayopewa sifa hiyo, jambo linalozingatiwa dhuluma dhahiri katika hukumu, na udanganyifu unaochekea bongo na fahamu, na haujalii hali halisi ya mambo wala historia, ambapo la dhahiri sana kwamba baadhi ya wafuasi wa dini nyinginezo wamefanya jinai na ukatili mkali sana wakitumia jina la dini zao na kwa shauri la wakubwa wao na watu wa kawaida, basi nifahamisheni kuhusu Vita vya Krusedi katika mashariki ya kiislamu, na vita vya kidini barani Ulaya, na mahakama ya ukaguzi yaliyotangazwa dhidi ya mayahudi na waislamu, je, vita hivyo vyote haviwi ugaidi wa kinyama?, na kumbuko mbaya sana katika historia ya kibinadamu!! Na inawezekana kusemwa kwamba halifu hizo zilikuwa hapo zamani, na kwamba athari zake zilitoweka zikawa hazina alama katika ulimwengu wa hivi sasa..basi niambieni kuhusu yanayoitwa hivi sasa kwa vita vya krusedi vya pili, na mimi sikutamka ibara hii kwa sababu ya mgongano tunaoushuhudia katika malimwengu mawili: wa kiarabu na wa kiislamu, bali ni anuani wa kitabu kilichotolewa karibuni na mtafiti maarufu wa kimarekani anayeitwa: John Faver ambapo kitabu chenyewe kilipewa anuani wa: "Vita vya Krusedi vya pili: vita vikali vipya vya magharibi dhidi ya Uislamu" na kwa bahati mbaya hatuna nafasi ya kueleza yaliyomo katika kitabu hicho au muhtasari wake, na kuna mifano yake makumi ya vitabu kuhusu maudhui hiyo, lakini nilitaka kuthibitisha kwamba upotovu ambao waislamu wachache sana walipatwa nao, wakafanya jinai kali hizo, ambazo maulamaa, wasomi, wenye hekima, wakuu na wa kawaida wa waislamu walizikana kabisa, upotovu kama huu una mifano yake kwa marudufu katika dini na itikadi nyinginezo, ukahimizwa na watu wa dini wakitoa ahadi kwa wanaoufanya kwamba watapata thawabu nyingi peponi.

Enyi mabwana nasisitiza kwenu kwamba kuchunguza historia ya: "ugaidi linganishi" likiwa jina hilo ni sawa, kunathibitisha kuwa waislamu walikuwa na kiwango cha juu sana katika uadilifu na ukweli, walipotofautisha baina ya dini, misingi yake na wakubwa wake, na baina ya halifu na jinai za wafuasi wa dini hizo..kwa hakika maulamaa wa waislamu na wanahistoria wao walikuwa wakiita vita vya kigaidi hivyo kwa jina la vita vya franks, wala hawakuvinasabisha kwa dini ambazo majina yake yalitumiwa katika vita hivyo, zaidi ya hapo hawakunasabisha kwa Msalaba, kwani wanatambua vyema tofauti wazi baina ya dini kama ni uongofu unaotokana na Mungu na baina ya wanaoitumia dini hiyo kwa ajili ya kuhakikisha maslahi yao na siasa ya usaliti na utawala, wakizingatia sana kuziheshimu itikadi za wengine na dini zao, japokuwa mateso waliyoyakabili waislamu wa zamani na wangaliteseka hadi hivi sasa katika maeneo mengi yaliyojulikana kwa wote, haikubaliki kukaa kimya mbele ya makosa yanayofanywa dhidi ya waislamu wanyonge kati ya mauji, maangamizi na ulazimisho wa kuacha makazi kwa nguvu nchini Myanmar, katika hali ya kimya kutoka mashirika na taasisi za kimataifa husika, ambazo misingi yake na kanuni zake huzilazimisha kuhifadhi amani na usalama wa mwanadamu na haki yake katika kuishi kwa amani, bila ya kutofautisha baina ya mwislamu na asiye mwislamu.

Vile vile haikubaliki kukaa kimya kuhusu jinai zilizofanywa kwa msikiti wa Al-Aqsa kibla ya kwanza na msikiti mtukufu wa tatu na mahali pa Israa ya Mtume (S.A.W.) kati ya ukaliaji na majaribio ya kuubadilisha uhusika wake uwe wa kiyahudi kwa njia ya kubadilisha majengo yake maarufu ya kiislamu.

Na kama baadhi ya taasisi za kidini za kimagharibi zimejidai kwamba zinawaombea wanadamu wote ulimwenguni kwa kulitatua waliloliita tatizo la ubaguzi dhidi ya wakristo wanaoishi katika nchi za mashariki, japokuwa hali halisi ya mambo inasisitiza kwamba waislamu na wakristo wa mashariki wanaishi pamoja kwa amani na upendo, na kwamba waliyoyateseka baadhi ya wakristo kati ya ubaguzi, ukatili na ulazimisho wa kuacha makao yao katika kipindi cha hivi karibuni sio nyingi ikilinganishwa na marudufu ya matatizo waliyoyakabili maelfu ya waislamu walioangamizwa pamoja na wanawake na watoto wao baharini, walipokuwa wakijaribu kutoroka na kujiokoa kutoka vita kali na ukatili mkubwa wanaoukabili nchini mwao. Nasema kwa haya taasisi kubwa ya kidini katika nchi za kimagharibi, endapo wahusika wake wamejidai kutoa wito hiyo, basi mimi kutokana na jukumu langu nawaombea wenye hekima na busara duniani kusaidia kuyatatua matatizo ya ubaguzi na dhuluma dhidi ya waislamu yanayofanywa na wasio waislamu mashariki na magharibi kwa ajili ya kutekeleza amani na kueneza usalama kwa manufaa ya wanadamu wote mashariki na magharibi.

Enyi watukufu mlio hadharani!!

Kwa hakika Mwenyezi Mungu (S.W.), hakuteremsha dini kwa kuwataabisha watu wala kwa ajili ya kuwatia hatarini ya madhara au hofu, bali ameziteremsha kama ni uongofu na rehema, waislamu hasa ni watu ambao huwa mbali kabisa na ugaidi, na vurugu, mauaji, umwagaji damu na kuangamiza roho zinazotokana na ugaidi huo, na mimi hasa hasa sijui dini wala kitabu kitakatifu cha mbinguni zinazotia adhabu kali ya umwagaji damu hapa duniani na akhera zaidi kuliko Uislamu na Qurani takatifu, ambapo Qurani imefaradhisha adhabu ya kulipiza qisasi katika mauaji ya makusudi duniani, na adhabu kali mno katika akhera: {Na mwenye kumuuwa Muumini kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahannamu humo atadumu, na Mwenyezi Mungu amemkasirikia, na amemlaani, na amemuandalia adhabu kubwa} An-Nisaa 93.

Na inakwaje kuuambatanisha Uislamu na ugaidi japokuwa ndiyo dini ambayo Mtume (S.A.W.) ameitangaza kuwa mwislamu wa kweli ni yule: "Ambaye watu husalimika kutoka ulimi wake na mkono wake", akasema: "Mwislamu wote ni haramu kwa mwingine, damu yake, mali zake na heshima yake".. na Uislamu haukutosheleka kuharamisha mauaji  na umwagaji damu tu, bali ukaharamisha kuwahofisha watu hata ikiwa kwa mzaha, akasema Mtume (S.A.W.): "Anayemwashiria ndugu yake kwa fimbo ya chuma, basi Malaika watamlaani mpaka amwache, hata akiwa ndugu yake kwa baba na mama", pia Mtume (S.A.W.) amesema: "Haijuzu kwa mwislamu kumhofisha mwislamu mwingine". Na vipi dini hiyo hutuhumiwa kwa ugaidi, vurugu na ukatili wakati ambapo Mwenyezi Mungu amemsifu Mtume aliyetumwa kwa ujumbe wa dini hiyo akawaambia watu kwayo kama ni: Rehema kwa walimwengu, akasema Mwenyezi Mungu: {Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote} Al-Anbiyaa 107. Naye (S.A.W.) akajisifu kwa kusema: "Enyi watu! Mimi ni rehema iliyotozwa" maana mimi ni rehema ya Mwenyezi Mungu iliyotozwa kwa walimwengu, na atakaetazama vyema katika maana ya aya tukufu na hadithi shariif inambidi kufikia matokeo mawili ya kikweli yasiyo na shaka yo yote nayo ni:           

La kwanza: kwamba rehema kwa dhana yake ya kijumla ni hekima kuu ambayo kwa ajili yake Mwenyezi Mungu Alimtuma Mtume wake kwa watu, na hii ni kwa mujibu wa mtindo wa ufubishaji wa kibalagha uliopo katika aya na hadithi, ambapo aya inaafikiana kabisa kimaana na hadithi kumaanisha kuwa Mtume wa Uislamu hasa ni Mtume wa rehema, na kwamba ametumwa kwa ajili ya kueneza rehema, na kwamba kuwarehemu viumbe ni lengo la kuja kwake duniani.

Na Qurani Tukufu yenyewe inathibitisha ukweli huu kupitia uangaliaji neno la {Rehema}, na idadi ya kutajwa kwake katika Qurani Tukufu, ambapo miongoni mwa fadhila zilizotajwa katika Qurani Tukufu kama vile: ukweli, subira njema, uadilifu, uaminifu, msamaha, ukarimu na mengineo, sifa ya "Rehema" ambayo imekuja mara nyingi kwa kiasi kinachostahiki kutazamiwa, ambapo imekuja kwa tamko zake mara mia tatu, kumi na tano ikilinganishwa na sifa ya {ukweli} iliyokuja mara mia moja arobaini na tano, {subira} mara tisiini, {msamaha}: mara arobaini na tatu, {ukarimu} mara arobaini na mbili, {uaminifu}: mara arobaini, {kutekeleza ahadi}: mara ishirini na tisa.

Ukweli wa pili tunaoweza kuufahamu kutokana na aya na hadithi ya Mtume ni ujumla wa Rehema ya Mtume (S.A.W) kwa walimwengu wote, kwa maana ya kwamba yeye ni "Rehema" ya Mwenyezi Mungu kwa viumbe vyote na kwa watu wote, na kwamba rehema yake siyo hasa kwa waislamu tu, lakini inajumuisha mataifa yote na watu wote - kwa mujibu wa aya-, na hii inayoonekana kutoka neno la {walimwengu wote}, ambalo dhana na maana yake haihusiani na ulimwengu wa kibinadamu tu, lakini inajumuisha pia malimwengu yote yanayodhaniwa na wanasayansi, wanafalsafa na wahenga, na wakayaainisha katika malimwengu ya binadamu, wanyama, mimea na vitu visivyo na uhai.

Na nyinyi mkiangalia kwa haraka sira ya Mtume (S.A.W.) basi mtashangaa kutoka ujumlisho wa rehema yake kwa malimwengu yote haya, kuanzia vitu visivyo na uhai hadi mwanadamu, ambapo Mtume (S.A.W) alikuwa na uhusiano wa upendo na amani pamoja na vitu visivyo na uhai, imetajwa katika kauli yake tukufu (Uhud ni mlima unaotupenda na sisi tunaupenda), na katika kauli yake (kwa hakika mimi najua jiwe moja katika Makkah lililokuwa linanipiga salamu kabla ya kutumwa kwangu na mimi nikalijua hadi hivi sasa). Na jambo lililo wazi zaidi ni kukataza kwake kwa majeshi ya waislamu wasiangushe nyumba za maadui wakati wa kupigana vita, au kuyabomoa majengo yao, au kuikata miti yao, au kuiondosha mimea yao, hayo na mengine imekuja katika amri wazi kabisa za Mtume (S.A.W) ambapo Mtume (S.A.W.) amesema: "msifanye chuki wala khiyana wala ukatili wala msiwauwe mtoto". Na katika hadithi nyingine (……….. msikate mti, wala msiondoshe mitende, wala msiangushe nyumba), na nyasia nyingine zilizofuatwa na maswahaba wake na makhalifa wake baada ya kufariki kwake, kama vile wasia wa Abu Bakar (R.A.) kwa jeshi la Usama ambapo amewaonya kuwaua watoto, au mzee mkubwa, au mwanamke, au mtumishi, au makuhani, au kuchinja mnyama isipokuwa kwa dharura ya ulaji na kwa kiasi yake bila ya kuvunja mipaka katika nchi za maadui.

Enyi mabwana, sio nyinyi tu bali walimwengu wote, mna haki ya kulinganisha na kutafakuri kuhusu tofauti kati ya tabia hizo za hali ya juu sana ya kibinadamu iliyotawala panga za waislamu, katika vita zikazizuia zisivunje mipaka ya uadilifu hata katika mapigano na maadui, mnaweza kutambua tofauti baina ya vile vita vya waislamu na vita vya kisasa, vinavyowaangamiza wanawake, wanaume, watoto kwa njia ya mauaji ya kimbari, na kuziangusha nyumba na kuviondoa vijiji kamili kutoka dunia, ili watu wote wanjua kutambua kwa yakini kwamba Uislamu ndiyo dini ya rehema na kwamba Mtume wake (S.A.W) ni Mtume wa rehema.

Enyi mabwana tukitaka kufuatilia alama za kutekeleza rehema hiyo katika ulimwengu wa binadamu, wanyama, mimea na vitu visivyo na uhai, tutahitaji wakati mwingi sana, lakini nimekusudia kutoka muhtasari huu wa haraka kujiuliza: inakuwaje kuituhuma dini hiyo kwa ni dini ya vurugu, ukatili, ugaidi na kuwatishia watu wasio na hatia, japokuwa dini hiyo yenyewe inategemea rehema kimaana, kimada na kimalengo. Kwa hakika dini hii ya kikweli haikutuhumiwa kwa tuhuma dhalimu kama hizo ila kwa sababu ya baadhi ya mzizi mbaya kati ya wana wake na vijana wake wanaofanya jinai za mauaji, uchomaji na ukatili mbaya kwa miili za maiti sawa ni waislamu au wasio waislamu kwa jina la dini, wakidhani kwamba wao wanapigana vita kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na wanachangia ustawi wa dola la kiislamu, wakamkafirisha kila mtu anawapigana au anakataa mawazo yao yasiyo sawa na madhehebu zao potofu, zisizokubaliwa na Uislamu, bali inazikana kabisa.

Na Al-Azhar Al-Sarif wakati wa kubeba jukumu la kubainisha na kuhubiri kwa dini huo mbele ya Mwenyezi Mungu siku ya Qiyama, na haichelewi kamwe kuonya mara kwa mara kutoka hatari za mawazo potofu, na kwamba mawazo hayo hayaambatani kamwe na Uislamu, Qurani na sheria, na kwamba watu hawa waliokosa njia sawa wakadanganywa wakadhani kwamba wanafuata uongofu wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa makusudi au kimakosa, wakafanya maovu dhidi ya Uislamu zaidi ya maadui ya Uislamu wenyewe, na wamechafusha sana Uislamu, wakatoa maelezo yasiyo sahihi kwa Uislamu, jambo ambalo maadui wa Uislamu wakiwa ndani ya ulimwengu wa kiislamu au nje yake wakalichukua kama ni kisingizio cha kuihujumia Uislamu na kushutumu dini hiyo na misingi yake, wakijeli Mtume wake, Sunna zake na sheria yake, na Al-Azhar ingaliwaita vijana hawa ikiwa na tamaa ya kwamba wahalifu hawa wana nafasi ya kutubu na kujipatia uongofu wao tena, na kutambua kwamba Mtume (S.A.W.) alikuwa ametuonya kutoka hatari za mawazo makali wanayoyashikilia na kufuata ambayo yamewapelekea nasi pamoja nao kwenye fitina hizo kali kwa kusema: "Enyi watu! Jitahadharini kutoka mawazo makali katika dini, ambapo jambo hilo lilikuwa kati ya sababu za kuwaangamiza watu waliokutangulia", na kwa kusema: "Wameangamizwa wanayo mawazo makali" maana: walio na misimamo mikali kimaneno na kimatendo.  

Na kwa mujibu wa kauli ya Mwenyzi Mungu: {Na kumbusha, kwani ukumbusho huwafaa Waumini} Adh-dhariyat 55. Tunawakumbusha hawa waliotufanya dhuluma na wameishutumu dini yetu, umma wetu na historia yetu, kwamba kurejea haki ni bora zaidi kuliko kuendelea katika batili, na kwamba wakati wa kutubu na kujilaumu na kujirudisha ukweli wakijuta kuhusu maovu waliyoyafanya kwa dini na umma wao umefika, na kwa hakika Mwenyezi Mungu (S.W.)  - kama wanavyojua – hungojea usiku ili akubali tawba ya mja wake aliyefanya dhambi mchana, na hungojea mchana ili akubali tawba ya mja wake aliyefanya dhambi usiku...{Hakika Mwenyezi Mungu hasamehe kushirikishwa, na husamehe yaliyo duni ya hilo kwa amtakaye} An-Nisaa 48, {Hakika rehema ya Mwenyzi Mungu iko karibu na wanao fanya mema}Al-A'raaf 56, {Sema: Enyi waja wangu walio jidhulumu nafsi zao! Msikate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu husamehe dhambi zote. Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu}Az-Zumar 53.

Hayo na ninajikumbusha mimi na maulamaa wa ummma kwa wajibu wetu ambayo tutaulizwa nayo mbele ya Mwenyezi Mungu siku ya Qiyama, nayo ni kujitahidi sana kama tuwezekenavyo kati ya kazi na kutoa nasiha ya wenyewe kwa wenyewe kwa ajili ya kuhifadhi umoja wa ummah na misingi ya itikadi yake kutoka uharibifu wa wenye misimamo mikali na walikosea uongofu na maoni ya wajinga.

Pia tunapaswa kutambua vyema umuhimu wa kuimarisha Fiqhi ya kurahisisha na kupambana na mawazo makali na vurugu, pamoja na kupambana fikira za kuhalilisha na kubadilisha kila kitu kiwe cha kimagharibi na kuharibu uhusika wa waislamu na nguzo zao thabiti na mafundisho ya kikale yao katika wakati ule ule.

Na kutambua pia hatari ya mafundisho katika kuimarisha Fiqhi ya kurahisisha na fikira ya kuishi pamoja, na kuporesha mitaala kutokana na mafunzo ya Qurani na Sunnah sahihi, na waliyoyakubali maulamaa wa waislamu, na kujiweka mbali sana na kuzingatia mambo yanayosababisha hitilafu badala ya mambo ya kimsingi yaliyo thabiti.

Na kati ya inayotakiwa kutambuliwa kisheria kwa dharura, bali ni wajibu, kuomba fatwa kutoka wenye elimu, wanaojilazimika kwa madhehebu za watu wa Sunnah, na walio na uzoefu na busara kwa mambo ya kisasa, na hutambua hatari ya maoni yasiyoafikiana na waliyoyakubali maulamaa wa ummah, au yaliyochaguliwa na aghalabu ya maulamaa na wana fiqhi kwa muda wa zaidi ya karne kuni na nne, na kufahamu kwamba upendeleo kwa masuala yanayosababisha hitilafu na fatwa zisizo za kawaida, hali hiyo imechangia sana kupatwa na migawanyiko na mizozo kwa ummah wakati huu, hali ialiyopelekea kuzipa baadhi ya nchi za kigeni kujiingiza katika masuala hayo, zikiwa na mikakati mibaya ya kuwaangamiza waislamu kama zinavyopenda, na matokeo mabaya ya hayo yalikuwa ni kwamba tukawa tunapigana wenyewe kwa wenyewe.

Tena hatuna suluhisho – enyi mabwana waheshimiwa- ila kwa kushikamana na kamba ya Mwenyezi Mungu, na amri yake katika kauli yake: {Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu: vile mlivyo kuwa nyinyi kwa nyinyi maadui naye akaziunganisha nyoyo zenu; kwa neema yake mkawa ndugu. Na mlikuwa ukingoni mwa shimo la Moto, naye akakuokoeni nalo. Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainishieni Ishara zake ili mpate kuongoka} Aal-Imran 103. Na hilo kwa kuepusha kutekelezwa ahadi ya Mwenyezi Mungu kwetu alipoitaja katika kauli yake: {Na mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala msizozane mkaingiwa woga, na zikapotea nguvu zenu. Na subirini. Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wanaosubiri} Al-Anfal 46, na pia ahadi ya Mtume (S.A.W.) katika kauli yake: "Mataifa wamekaribia kuungana dhidi yenu kutoka pande zote duniani kama wanavyoungana walaji juu ya kisahani cha chakula chao, tukasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu: hivyo kwa sababu ya kwamba sisi tutakuwa wachache siku ile? Akasema: bali mtakuwa wengi, lakini mtakuwa wengi bila ya faida yo yote kama maji ya mvua mzito, baada ya kuwa maadui wenu hawawaogopeni, na Mwenyezi Mungu hutupa Wahan nyoyoni mwenu. Tukasema: Wahan ni nini? Akasema: kupendelea dunia na kuchukia mauti".

Enyi maulamaa wa ummah kwa madhehebu zake zote tunapaswa kutafakuri vyema mfanano uliotolewa na Mtume usio na mfano katika hadithi hii mtukufu, ambao unatoa mfano wa kisahani kilichojaa chakula kitamu, na mzunguko mwake kuna wanaotaka kula sana, wanaoitiana kwa ajili ya kukila chakula hicho, mbele ya walinzi wa kisahani hicho na wamiliki wake, ambao wamejishughulikia masuala madogo yasiyo muhimu kabisa, na tukikumbuka mfano huo wa Mtume tukautumia katika kuelezea hali ya waarabu na waislamu siku hizi, na waliopewa na Mwenyezi Mungu kati ya vitu vya thamani kubwa vinavyoonekana na visivyoonekana ambavyo vingi sana, na tamaa za mataifa mengine katika vitu hivyo, tukitambua mfano huo tutafahamu sisi tumefika wapi hivi sasa kuhusu yaliyotajwa hadithini ambayo imekaribia kutabiri hali halisi yetu ya siku hizi baada ya kutajwa kwake kwa muda wa karne kumi na tano.

Je, yupo anaye kumbuka?

 

Nakushukuru sana,

Na Assalamu Alykum warahmatul-lahi wabarakatuh

 

[1]  "Chui" ni jina la nchi nne zilizopo barani Asia zilizojulikana kwa maendeleo zaidi nazo ni: Sengapore, Taiwan, Hong Kong na Korea kaskazini.

Print
Tags:
Rate this article:
5.0

Please login or register to post comments.