Baada ya kupokea mwaliko rasmi: Mheshimiwa Imamu mkuu ajitayarisha kuizuru Italy ili akutane na raisi wa nchi hiyo na kutoa hotuba bungeni

  • | Friday, 16 October, 2015
Baada ya kupokea mwaliko rasmi: Mheshimiwa Imamu mkuu ajitayarisha kuizuru Italy ili akutane na raisi wa nchi hiyo na kutoa hotuba bungeni

Mheshimiwa imamu mkuu wa Al-Azhar Al-Shareif profesa; Ahmad Al-Tayyib atasafiri katika siku chache zijazo kwenda mji mkuu wa Italy, Roma, katika ziara rasmi, ambapo atakutana na raisi wa kiitaly Bw; Serjo Matarilla ili kujadili masuala muhimu ya pamoja.
Inatarajiwa kwamba mheshimiwa imamu mkuu atatoa hotuba ya kimataifa mbele ya bunge ya kiitaly kwa sehemu zake mbili (Seneti na Wabunge) kuhusu "Dini na Amani", ambapo atazungumza katika hotuba hii kuhusu ujumbe wa amani ambao Manabii na Mitume wote wametumwa nao, pamoja na kusisitiza juu ya umuhimu wa maadili ya uwastani, kuishi pamoja na kukataa vurugu na misimamo mikali.
Ziara hiyo inakuja katika mfumo wa juhudi kubwa alizozifanya mheshimiwa imamu mkuu profesa; Ahmad Al-Tayyib, Shekhi mkuu wa Al-Azhar Al-Shareif, kwa ajili ya kuanzisha mazungumzo ya kistaarabu baina ya mashariki na magharibi, mazungumzo hayo yanayotegemea kuwaheshimu na kuwakubali wingine, na kuimarisha maadili ya demokrasia, uhuru na haki ya binadamu ya kuishi kwa amani.  

 

Print
Categories: Habari
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.