Al-Azhar Al-Shareif yashutumu mashambulio ya kigaidi katika kaskazini mashariki mwa Nigeria

  • | Wednesday, 15 July, 2015
Al-Azhar Al-Shareif yashutumu mashambulio ya kigaidi katika kaskazini mashariki mwa Nigeria

Al-Azhar Al-Shareif inashutumu mashambulio ya kigaidi ambayo yametekelezwa na wanamgambo wenye silaha wa kundi la Boko Haram dhidi ya miji kadhaa kaskazini mashariki mwa Nigeria, ambapo mashambulio hayo yamesababisha kuwaua zaidi ya watu arobaini na kujeruhiwa kwa makumi.
Al-Azhar Al-Shareif inasisitiza kuwa vitendo vinavyofanywa na makundi hayo kutoka mauaji, kuwachinja na kuwatishia watu wasio na hatia na kuwalengea watoto na wanawake haviafikiani na mafunzo ya Uislamu yenye msamaha ambayo yanakataa vurugu na ugaidi kwa namna zake zote.
Pia, Al-Azhar Al-Shareif inatilia mkazo udharura wa kuunganisha juhudi za kimataifa kwa ajili ya kupambana na makundi hayo yenye mawazo makali, vile vile inaiombea serikali ya Nigeria kufuatilia wahalifu hao na kuwashtaki mahakamani na kuwalipiza kisasi.

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.