Nimekuja nchini Nigeria ili kusisitizia udharurua wa kuungana kwetu dhidi ya wanaotaka kueneza vurugu na ugaidi.
Mheshimiwa Imamu mkuu profesa; Ahmad Al-Tayyib sheikhi mkuu wa Al-Azhar Al-Shareif alisisitiza kwamba wafuasi wa kundi la Boko Haram na makundi yanayofanana nalo kati ya yale makundi ya kigaidi hawawakilishi Uislamu ambao haihusiani nao na vitendo vyao vya kikatili kabisa, akibainisha kuwa Uislamu haikuwa dini ya umwagaji damu au vurugu au kuwaangamiza watu, bali ni dini ya kuhifadhia uhai na amani na kueneza rehema na maendeleo.
Akijibia swali la mwandishi mmoja wa habari kwenye mkabala wa vyombo vya habari wa kimataifa uliofanyika leo katika mahali pa kukaa kwake mjini Abuja, Mheshimiwa Imamu mkuu alisema: hakika sisi tulijifunza na tunawafundisha wanafunzi wetu katika Al-Azhar Al-Shareif kwamba Qur'ani Tukufu ilibainisha njia na mbinu za kulingania kwa Mwenyezi Mungu ikaziweka wazi wazi kwa namna inayozifanya zifahamike na watoto wa umma kabla ya vijana na wakubwa wake, ambapo ilibainisha kuwa ulinginiaji kwa Mwenyezi Mungu lazima uwe kwa hekima na mawidha mema, pia haikumwita ye yote kati ya waislamu abebe silaha na kuwaua watu, na atakayefanya hivyo hawakilishi mfumo wa Al-Azhar hata kidogo.
Mheshimiwa Imamu mkuu akaongeza: kwa kweli sisi tunawaombea hao watubu, kusahihisha makosa yao, kuandamana na jamaa ambayo Qur'ani Tukufu iliisifu, na wajirekebishe sio hapa nchini Nigeria tu bali ulimwenguni kote, akiashiria kwamba Mwenyezi (S.W.) Ameharamisha umwagaji damu, na kwamba Uislamu ulipweka kwa kupitisha adhabu kali mno duniani na akhera kwa yule anayewaua watu na kuhalalisha kumwaga damu zao, na Mwenyezi Mungu (S.W.) Hatawasamehe watu hao wanaowaua watu na wanazimwaga damu zao pasipo na haki, basi mwislamu haijuzu kwake amwue au apigane na mwingine ila akiwa anajikinga nafsi yake, isitoshe, bali Uislamu haikupa jamaa au kundi lo lote haki ya kupitisha adhabu, bali imefanya haki hiyo hasa kwa mtawala au naibu wake katika majaji.
Yule Mheshimiwa alibainisha pia kuwa kuhitilafiana ni jambo la kimaumbile na kwamba uhusiano uilopo baina ya watu lazima utegemee kujuana, akidokezea kwamba makundi hayo yanauchafusha Uislamu, bali wanaopatwa na madhara zaidi ni waislamu wenyewe, akisisitiza kwamba vita vilivyofanywa na waislamu vilikuwa kwa lengo la kujitetea; kwa ajili ya kuzuia hatari ya maadui walio mpakani.
Akaendelea akisema: nimekuja hapa ili kukutana na taifa wa Nigeria wote kwa makundi na migawanyiko yao yote ili kusisitiza umuhimu wa kuungana kwa ajili ya kupambana na wanaoeneza mawazo ya kikali na ya kigaidi, na tutafanya juhudi za pamoja katika kipindi kijacho sisi na wananchi wa Nigeria ili kubainisha mawazo sahihi ya dini na kupigania vita ugaidi kwa namna zake zote.
Akijibia swali jingine kuhusu lengo kuu la ziara, Mheshimiwa Imamu mkuu alisisitiza kwamba ziara hiyo ilikuja kwa mujibu wa kuitika mwaliko wa rais wa Nigeria/ Mohammad Bukhari kwa Al-Azhar ikiwakiliwishwa na Imamu wake mkuu na baadhi ya wanavyuoni wazuru nchi hiyo, na pia kubainisha ukweli wa Uislamu, ambayo ni dini ya amani kwa wanadamu wote na ulimwengu kote, pia ziara hiyo ilikuja kwa ajili ya kubatilisha yale majaribio ya kuichafusha dini takatifu hiyo yanayoendelea mashariki na magharibi.
Akasema: Al-Azhar Al-Shareif tangu zaidi ya miaka elfu moja ilijishughulikia suala la kimsingi la kueneza Uislamu kama alivyokuja nayo Mtume Mohammad (S.A.W.) ambayo ndio dini ya rehema na amani kwa mwanadamu, wanyama, vitu visivyo na uhai bali malimwengu yote, na kwamba ziara hii haina malengo mengine yaliyo mbali na kubainisha ujumbe wa Uislamu duniani, akiongeza kuwa: sisi si wanasiasa, na Al-Azhar haijui siasa wala haijishughlikia nayo tangu mnamo zaidi ya miaka elfu moja.
Wakati wa kujibu swali kuhusu mahusiano ya kielimu, kulinginiaji na kimafundisho baina ya Al-Azhar Al-Shareif na mashirika ya kidini nchini Nigeria, Sheikhi mkuu wa Al-Azhar alisema: Al-Azhar ni shirika la kufundisha linalofungamana na ulimwengu wa kiislamu wote, ambapo mnamo wanafunzi milioni mbili katika taasisi ya mafundisho ya kabla ya Chuo kikuu, na wanafunzi wengine laki tano katika mafundisho ya Chuo kikuu na masomo ya juu, wakiwemo wanafunzi elfu arobaini wageni waliokuja kutoka nchi 66, Nigeria inashika cheo cha tatu kulingana na idadi ya wanafunzi wageni waliokuja kutoka nchi hiyo baada ya Indonisia na Malysia, akibainisha kwamba safari hiyo inatilia mkazo katika upande mmoja kuwasiliana kimasomo kupitia wana wa Nigeria wanaosoma katika Al-Azhar na walimu tunaowatuma nchini humo ili kufundisha masomo ya kisheria na ya kiarabu kwenye taasisi za Nigeria.
Na katika jibu la swali kuhusu juhudi inazozifanya Al-Azhar Al-Shareif kueneza mawazo ya mazungumzo na kuishi pamoja kwa amani, Mheshimiwa Imamu Mkuu alisisitiza kuwa Al-Azhar ilianzisha "Kituo cha Uangalizi kwa lugha za kigeni", kinachofuatilia masuala yanayojiri ulimwenguni kote kwa lugha nane tofauti, kisha masuala hayo yanafasiriwa kwa lugha ya kiarabu ili yachunguzwe na kundi la wanavyuoni husika ili watayarishe jawabu linalofaa, kisha majibu hayo yanatangazwa baada ya kufasiriwa kwa lugha tofauti kwa ajili ya kuhakiksha maadili ya kusameheana na kuishi pamoja kwa amani.
Akaongeza: vile vile tuna kituo cha habari kinachofuatilia matukio yanayojiri duniani, na kituo cha mazungumzo baina ya dini mbali mbali, na hasa dini ya Ukristo, licha ya Baytul Aaila , pia tumeanza mazungumzo baina ya nchi za mashariki na zile za magharibi kule mji wa Firenza nchini Italia, kisha ziara nyingine za kuelekea Uingereza, Indonisia, Ujerumani, na leo kwa Nigeria ili kuimarisha fikira ya amani, mazungumzo, na kuishi pamoja, vile vile tumetuma kwa kushirikiana na Baraza la wakuu wa waislamu misafara ya amani kwa mbara tofauti duniani ambapo msafara wa mwisho kabisa ilikuwa tangu wiki chache kwa nchi hiyo Nigeria.
Na akijibu kwa swali kuhusu iwapo ushirikiano baina ya Al-Azhar Al-Shareif na Baraza kuu la masuala ya kiislamu nchini Nigeria katika juhudi za kupambana na ugaidi, Imamu mkuu alisema: kwa hakika ushirikiano uliopo mpaka hivi sasa ni wa kiwango cha kiakadimy tu, lakini tumechukua hatua za kiutendaji ili kuomba msaada wa wahitimu wa Al-Azhar katika nchi mbali mbali kwa ajili ya kushiriki katika kuhakikisha roli ya kilinginiaji ya Al-Azhar kwenye nchi zao chini ya usimamizi na ulezi wa Al-Azhar Al-Shareif.
Na kuhusu maoni yake juu ya wajumbe wa Al-Azhar katika nchi mbali mbali, alisema Imamu mkuu: tunapata mara kwa mara ripoti kupitia balozi wa Misri kwenye nchi hizo, akibainisha kwamba balozi hao wanafanya juhudi kubwa ili kueneza mawzo ya kiwastani ya Al-Azhar Al-Shareif, na tunataraji kuzidisha na kukuza juhudi hizo kikubwa katika kipindi kijacho.
Akijibu swali kuhusu michango ya kifedha ya zile programu zilizotunzwa na Al-Azhar kwa wanafunzi wageni, Immau mkuu alisisitiza kwamba Misri ndiyo inayotoa michango ya kutekeleza program hizo, na kwamba Al-Azhar haipokei tuzo kutoka ye yote, na kwamba tuzo za kufundisha zinazotolewa kwa wana wa waislamu na wajumbe Misri ndiyo inazitoa, akibainisha kwamba wanafunzi waislamu wanasoma bure katika Al-Azhar Al-Shareif hata wakiwa wamekuja kutoka nchi tajiri, ambapo huu ndio ujumbe wa Al-Azhar tangu zaidi ya miaka elfu moja.
Mwishoni mwa mkabala huu na waandishi wa habari, Imamu Mkuu alisisitiza kuwa ujumbe inayoubeba Al-Azhar Al-Shareif ni ndio ujumbe wa kueneza amani na usalama ambayo Uislamu ulikuja nayo, akiwaita mataifa wa kiafrika waungane katika malengo na juhudi jambo linalotarajiwa kusaidia kutekeleza matamanio ya mataifa wa bara hilo na matarajio yao.