Swala za Jeneza zinasimamiwa wapi wakati huu wa kufunga misikiti?

  • | Thursday, 26 March, 2020
Swala za Jeneza zinasimamiwa wapi wakati huu wa kufunga misikiti?

     Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, na Swala na Salamu zimefikia mtume wake (S.A.W.), Familia, Maswahaba, na Wafuasi wake. Ama baadaye..
Si sharti kusimamisha swala ya jeneza misikitini, bali inajuzu kusaliwa mahala popote pa ardhi penye twahara kwa mujibu wa ujumla wa kauli ya mtume (S.A.W): "Ardhi imejaaliwa kwangu msikiti na yenye twahara, basi mtu yeyote wa umma wangu akijiwa na wakati wa swala basi asali". [Sahihi Al-Bukhari].


Bali wanachuoni wote wa fiqhi waliona kwamba asili ya swala ya jeneza ni kusaliwa viwanjani nje ya msikiti, kwa hivyo imamu Al-Sanadi alisema kuhusu swala ya jeneza: "Ndiyo, ni bora zaidi kusaliwa nje ya msikiti kwani aghalabu ya wakati mtume (S.A.W.) alikuwa anasali nje ya msikiti". [Hashia ya Al-Sanadi juu ya Ibn Majah (3/298)]
Ingawa mambo yote mawili (kusali ndani au nje ya msikiti) yanaruhusiwa; basi Imamu Al Bukhari aliandika katika kitabu chake (Sura ya (Swala ya jeneza ndani na nje ya msikiti); jambo linaloashiria usahihi wa mambo mawili katika madhehebu yake, kama wanafiqhi wengine walioona kwamba swala ya jeneza inajuzu ndani ya msikiti bila chuki, nao ni wengi.


Kwa mujibu wa hizo, na kwa kuzingatia hali ya kufunga misikiti ya nchi kwa sababu ya hofu ya kuenea kwa kirusi kipya cha Korona (Covid 19), basi inajuzu kusali swala ya jeneza viwanjani nje ya msikiti, na katika ardhi tupu, na mbele ya Kaburi. Na mwenyezi Mungu ni mjuzi zaidi.

 

Print
Tags:
Rate this article:
5.0

Please login or register to post comments.