Matukio ya mashambulizi ya "Kundi la Al Shabab la Kisomalia" hivi karibuni

  • | Thursday, 2 April, 2020
Matukio ya mashambulizi ya "Kundi la Al Shabab la Kisomalia" hivi karibuni

    Jina la "Kundi la Al Shabab la Kisomalia" limehusishwa na kuenea kwa uharibifu na umwagaji wa damu katika maeneo ya Afrika ya Mashariki, hasa katika nchi ya "Somalia" na "Kenya". Katika "Somalia" hakuna siku mmoja hupita bila ya kuwepo habari ya mlipuko uliofanywa na kundi hili hapa na nyingine huku. Kundi hilo linayalenga maeneo ya vikosi vya serikali na jeshi, mlipuko mwingine unalenga bila ya mpangilio maeneo katika mji mkuu wa Somalia "Mogadishu", uliosababisha vifo vya watu wengi na wengine walijeruhiwa, katika jaribio la kudhoofisha imani ya Wasomali katika nchi yao, na kuwatisha wanajeshi na polisi. Katika "Kenya", kundi hilo linafanya mashambulizi ya kurudia kwa miji ya Kenya iliyopakana na mipaka ya Somalia, kwa kuitikia serikali ya Kenya iliyopeleka vikosi vyake nchini Somalia ndani ya mfumo wa ushirikiano wa pamoja kati ya nchi hizo mbili katika uwanja wa kupambana na ugaidi.
kupitia kufuata "Kituo cha Al-Azhar cha kupambana na mawazo makali" kwa mkakati wa kundi hili limebainisha kwamba limezidisha vurugu katika miezi ya hivi karibuni, na vile vile makundi yake zinazokua nchini Somalia na nje yake, ikitumia fursa ya machafuko, utupu na misukosuko mnamo Desemba 2019, na katikati mwa mji mkuu Mogadishu, washambulizi wa kundi hilo wamefanya shambulio la kigaidi kwa kulipua lori lenye bomu, lililosababisha kuwaua watu takriban 100 na kujeruhi makumi, hayo yametokea katika chini ya wiki moja baada ya shambulio lingine lililofanywa na vikundi vyake mnamo 21 Desemba 2019 uliopita dhidi ya kamanda wa vikosi vya jeshi la nchi kavu la Somalia lililosababisha kuwaua askari 8 wa Somalia.
kabla ya shambulio hilo la 6 Desemba 2019, watu wenye bunduki walioshirikiana na kundi hilo walifanya shambulio lililolenga basi la abiria katika eneo karibu na mipaka baina ya Somalia na Kenya, lililosababisha kuwaua watu 8 miongoni mwao ofisa wa polisi wa Kenya, pia mwezi wa Januari mwaka huu 2010 ulishuhudia mashambulizi ya kigaidi nyingi katika ardhi ya Somalia. Ingawa hatari ya kundi hilo ni kubwa zaidi katika Somalia na kando ya mipaka ya Kenya na Somalia, basi imeweza pia kufanya mashambulizi kama hayo katika miji mikubwa ya Kenya, kama vile "Nairobi", "Garissa" na "Lamu".
Hakika maongezeko hayo yenye hatari na kushangaza kuhusu idadi na namna ya vitendo vya kigaidi vinavyofanywa na kundi hili katika siku za hivi karibuni, sawa kama vikikuwa ndani au nje ya Somalia yanarejesha tena kuleta mwanga kwa hatari ambayo kundi hili linaendelea kuifanya baada ya miaka ya kutangaza vita juu yake, na vile vile yanatoa maswali kadhaa kuhusu malengo na nia ya kundi linalochochea kuongezeka kwa vitendo vyake vya kigaidi, na athari zake kwa hali ya usalama ya baadaye katika Somalia na eneo la "Pembe la Afrika", ambalo linajumuisha Djibouti, Somalia, Eritrea, na nchi za jirani Kenya na Ethiopia.
Kituo cha uangalizi kinaona kuwa tendo hilo la kuongezeka kwa kundi katika siku za hivi karibuni linaijaalia iwe moja ya vikundi vyenye hatari zaidi ya kigaidi katika maeneo ya Afrika ya Mashariki, hasa baada ya kupunguza kwa vitendo vya kundi na makundi ya kigaidi katika Mashariki ya Kati na Afghanistan, jambo lililoonekana wazi katika orodha ya vitendo vya kigaidi katika bara la Afrika katika Januari. Mwaka huu 2020 BK, ambapo kundi lililoongoza eneo la umwagaji damu kwa kufanya karibu ya vitendo 28 vya kigaidi nchini Somalia na Kenya, vitendo hivyo vilitofautiana kati ya mashambulizi ya silaha, milipuko ya kujiua na matendo ya mauaji ambayo yalisababisha vifo vya watu zaidi ya 148 kuuawa na kujeruhiwa. 
Vitendo hivyo vyote vya kigaidi vinaonyesha kuwa kitovu cha kupambana na ugaidi kinaweza kugeuka kwa  Pembe la Afrika, ambalo huzingatiwa sehemu dhaifu ya bara hilo ambalo vikundi vya kigaidi huenda vinalitumia ili kuyazidisha mashambulizi ya kigaidi. Ingawa ya kuongezeka kwa juhudi za ndani, kikanda na kimataifa ili kupunguza uwezo wa kundi hili na kuiondoa kabisa, yote haya hayakumaliza tishio lililotokana na kundi hili ya kigaidi, ambayo ilifanikiwa kupata tena sehemu kubwa ya nguvu yake na kuzidisha vitendo vyake vya kigaidi, ili kuenea tena kwa kiwango kikubwa. hayo ndiyo ambayo kituo cha uangalizi cha Al-Azhar kinatahadharisha, na kinatia mkazo umuhimu wa kuongeza mapambano ya usalama na kiakili dhidi ya kundi hili yenye mawazo makali, kituo cha uangalizi cha Al-Azhar hakibaki nyuma katika kufuatilia mawazo yoyote yaliyotolewa na kikundi hicho au wenzao kutoka kwa vikundi vya mawazo makali na vya kigaidi.
Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na Mawazo Makali
Kitengo cha Lugha za Kiafrika.


 

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
5.0

Please login or register to post comments.