Kinachodhuru labda kinafaa .. Janga la Corona kama ni mfano

  • | Sunday, 31 May, 2020
Kinachodhuru labda kinafaa .. Janga la Corona kama ni mfano

     Katikati ya matukio ya kihistoria yasiyo na pumzi ambayo ulimwengu wetu wa kisasa huenda haujaona mifano yake hapo kabla, picha inaonekana mbaya kiasi fulani, lakini katikati ya giza hilo lililojaa wingu, wengine hugundua kuwa hii ambayo ubinadamu unapitia sasa, na tunamaanisha kuenea kwa janga la (Covid 19) inayojulikana kwa virusi vipya vya "Corona"; sio ila somo jipya linaloongezwa kwa masomo hayo ambayo ubinadamu umefaidika nayo katika njia ya maendeleo yake kwa miaka kadhaa.
Licha ya madhara makubwa yaliyosababishwa na kuenea kwa janga la ‎"Corona"‎, ikiwemo vifo maelfu kadhaa ya watu duniani, imegundulika kuwa maradhi haya kwa kiasi kikubwa imechangia kupunguza maasi na kujenga utangamano wa kifamilia.
Ama kuhusu kupunguza maasi, maasi mengi yaliyokuwa yakifanywa kwa wingi, yamesimamishwa hivi sasa duniani kote kwa hofu ya watu kuambukizana "CORONA" katika mikusanyiko ya watu. Miongoni mwa maasi hayo ni kucheza kamari. Michezo hiyo ya kamari iliyoharamishwa katika Qur’an Tukufu, na kuitwa kuwa ni uchafu katika kazi za shetani; tayari imeanza kutangazwa kuwa michezo hiyo ni sababu ya kupoteza mapato na mali na kuingia katika hasara. Mwenyezi Mungu anasema kuhusu kamari: “Enyi mlio amini! Bila ya shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya shetani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa.” [5:90].
Vile vile, ulevi ni katika maasi yaliyotajwa kuwa ni ‘uchafu katika kazi za shetani’ katika aya ya Qur’an tuliyotangulia kuitaja. Ulevi kwa aina zake mbalimbali kama "ulevi wa tumbaku kupitia shisha", bangi, kisha moshi inayotolewa kupitia mirija ya Shisha ambayo watu huipokezana, jambo ambalo linahatarisha afya za wavutaji kama baadhi yao wana Corona. Kukatazwa kwa shisha kuna maana kuwa ulevi ambao umekatazwa katika Qur’an Tukufu, unapungua sasa hivi kwa sababu ya maradhi ya Corona.
Maasi mengine yaliyopungua ni zinaa, ambapo katika nchi mbalimbali, klabu za usiku, baa na madanguro, matamasha makubwa ya muziki, yamefungwa kwa muda kwa hofu ya maradhi ya Corona. Zinaa ni katika maasi makubwa katika Uislamu, ambapo Mwenyezi Mungu Mtukufu Amewaonya wanadamu wasikaribia, achilia mbali kuifanya. Mwenyezi Mungu anasema katika Qur’an Tukufu: “Wala msikaribie uzinzi. Hakika huo ni uchafu na njia mbaya.” [17:32].
Jambo la kufurahisha ni kuwa, marufuku za maasi mbalimbali – klabu za usiku, madanguro, kasino, shisha, baa, maeneo ya kuchezea kamari, matamasha ya muziki – zimewekwa kila nchi duniani, za Kiislamu na hata zisizo za Kiislamu, jambo linaloonesha ufalme na uwezo  wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kubainisha kuwa ugonjwa wa Corona umethibitisha kwamba nchi zinaweza kuzuia aina zote za uovu; kufunga baa, vilabu vya usiku, madanguro, na pia nchi zina uwezo wa kutekeleza sheria za Kiislamu.
Na kuhusiana na athari za virusi vya Corona juu ya utangamano wa familia, tunaangalia kuwa mahusiano ya kifamilia yamezidi kuimarika kutokana na kukaa nyumbani, ambapo mume amsaidie mkewe katika kazi za nyumbani, na kuelimisha watoto hukumu za dini, na kusali pamoja nao sala za jamaa na Taraweh.
Mambo hayo yanathibitisha kuwa ugonjwa huu wa Corona umefichua kuwa kumbe inawezekana kuishi bila kuwa na kumbi za starehe, baa, matamasha, na kampuni za Kamari.
Mwishoni, tunamwombea Allah (S.W.) aiondoshe maradhi hiyo ya Corona na kuhifadhi watu wote duniani.
 

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.