Hatari za makundi ya kigaidi katika afrika pamoja na kueneza janga la Corona

  • | Sunday, 5 July, 2020
Hatari za makundi ya kigaidi katika afrika pamoja na kueneza janga la Corona

     Katika wakati ambayo nchi za Kiafrika zinapambana na janga la Corona ambalo limeeneza kwa njia kubwa katika nchi zote za Afrika, kwa mfano idadi ya watu waliombukizwa virusi vya Corona nchini Kenya sasa imefikia zaidi ya elfu tano, pia idadi ya watu waliopoteza maisha yao hivi sasa imefikia mia moja na thelathini. Hali ambayo inawatia wasiwasi viongozi na raia wa nchi hiyo na nchi nyingine katika Afrika. 
Na ingawa hali hiyo mbaya kwa sababu ya janga la Corona ambalo limekwishasababisha vifo vya watu wengi, tunakuta kuwa makundi ya kigaidi nchini za kiafrika zinaeneza hofu na fazaa na utisho katika nyoyo za raia.
Kwa mfano, kuna kundi la Boko Haram katika nchi nyingi za Afrika ya Magharibi, ukiongozwa na Nigeria na pia kundi la Al-Shabab huko Afrika ya Mashariki, hasa katika Somali, na mashambulio ya Al-Qaeda huko Afrika ya Kaskazini, vinazuia kuwepo amani na usalama nchini.
Hakuna shaka kuwamba kuna changamoto na matatizo yanayoyakabili bara la Afrika na kuzuia katika harakati zake za kuelekea maendeleo ya bara hili kwa nyanja zote za kiuchumi, kielimu, kisiasa na kijamii pia. Na umuhimu wa vikwazo hivi ni kuenea makundi ya kigaidi katika kote Afrika, na jambo hili limeibua wasiwasi nyingi, sio tu kwa kiwango cha viongozi wa bara hilo, lakini pia katika kiwango cha mashirika ya kimataifa.
Katika miaka ya mwishoni, nchi za Afrika zimefanya juhudi kubwa kwa ajili ya kupambana na makundi ya kigaidi yaliyokuwepo kwenye nchi zao. Pamoja na hiyo, kuongezeka kwa makundi haya mapya ya kigaidi, machafuko ya kisiasa, udhaifu wa serikali za Kiafrika katika kupambana na makundi hayo, kuhitaji zaidi kwa vikosi vya kijeshi, na kutokuwepo ushirikiano kuhusu masuala ya usalama na ya kijeshi, mambo yote hayo yamezuia mafanikio ya nchi hizi katika vita vyao dhidi ya makundi ya kigaidi.
Na hakuna shaka kwamba hatari ya kuongezeka kwa makundi ya kigaidi katika nchi zingine za ulimwengu, hasa katika Ulaya, imewalazimisha viongozi wengine wa Ulaya kufikiria sana kusaidia nchi za Afrika katika kupigana na ugaidi. 
Tukiangalia kwa ukweli kwamba nchi za Afrika zimechukua uamuzi wa kuongeza ushirikiano katika maswala ya kijeshi na usalama na kujaribu kuwepo kutatua kwa ugaidi ambao upo ndani ya nchi kupitia ushirikiano wa nchi za Kiafrika, tunaona kuwa matumizi haya yanaathiri vyema ili kupunguza kwa hatari ya makundi hayo ya kigaidi ndani ya nchi zake. Pia inaweza kupunguza eneo kubwa linaloyatawala makundi hayo.
Na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres pia alionya juu ya athari mbaya kwa kuwepo makundi ya kigaidi na yanayoendelea barani Afrika. Ambapo akizungumzia kuhusu shida kwenye bara la Afrika lililosababishwa na mashambulio haya ya kigaidi, Guterres alisema katika mkutano wa kupambana na ugaidi uliofanyika katika mji mkuu wa Kenya Nairobi mwezi uliopita: “Kwa hakika, familia ndio zinaathiriwa zaidi na ugaidi, ambayo inatishia usalama na amani kwa jumla. Alisisitiza pia kwamba ugaidi haupaswi kudhoofisha maendeleo na utulivu wa bara la Afrika, na kwamba kuna dharura katika ulimwengu wote kwa ajili ya kuunga mkono na bara hilo na kulisaidia katika kuondoka kutoka mgogoro wake wa sasa. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa pia alitaka ulimwengu wote kuwasaidia viongozi na watu wa bara la Afrika katika vita vyao dhidi ya ugaidi.
Na kituo cha Al-Azhar kwa kupambana na mawazo makali kinaendelea kufuatilia matukio yote yanayofanya katika kote bara la Afrika, kwa ajili ya kufuatilia, kuchambua, kukataa, na kujibu juu ya shubha za makundi za kigaidi, na ili pia Al Azhar daima ipo katikati ya matukio, pamoja na watu wa bara la Afrika, ikiwaunga mkono kwa hoja nguvu na kuwasaidia kwa uongozi bora na kuwapa ulinzi muhimu kutokana na mawazo mabaya.
Hakika mtazamaji kwa historia ya Al-Azhar hakuti vigumu au haoni taabu katika kutambua michango ya taasisi kubwa hiyo na athari yake nzuri ndani na nje ya Misri; ambapo Al-Azhar imejalia kwa kuinua thamani ya ubinadamu na kueneza utamaduni wa amani na ushirikiano duniani kote. Na kwa sababu zote hizo tunaweza kusema bila shaka yoyote kwamba Al-Azhar – kwa kweli – ni  mojawapo ya taasisi kubwa duniani ambazo zinajaribu kwa njia kubwa kuokoa ubinadamu kutoka ulimwenguni ambao umejaza kwa vurugu na ugaidi, pamoja na mazoea ya chuki na ubaguzi na yote yanayopigana na misingi ya kibinadamu, hakika katika hayo upo ukumbusho kwa mwenye moyo au akatega sikio naye yupo anashuhudia. 
 

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
5.0

Please login or register to post comments.