Sheikh wa Al Azhar kwa Rais wa Shirika la Maendeleo la Marikani: Kusimamisha vita na chuki ndio njia rahisi kabisa ya kutatua matatizo ya ulimwengu

  • | Monday, 12 October, 2020
Sheikh wa Al Azhar kwa Rais wa Shirika la Maendeleo la Marikani: Kusimamisha vita na chuki ndio njia rahisi kabisa ya kutatua matatizo ya ulimwengu

     Rais wa shirika la maendeleo la Marekani: Tunashughulika kwa kusaidiana na Al-Azhar kwa ajili ya kutokomeza mizizi ya chuki na ugaidi ulimwenguni Mheshimiwa imamu Mkuu, Profesa Ahmed Al-Tayyib, Sheikh wa Al-Azhar Al-Sharif, amempokea leo, Jumatano, Bwana John Barsa, naibu wa Rais wa Shirika la kimarekani kwa maendeleo ya kimataifa huko Washington, na ujumbe ulioandamana naye.
Raisi wa shirika la kimarekani la maendeleo ya Kimataifa alisema kuwa alikuwa na hamu ya kukutana na Imam mkuu, ingawa ziara hiyo itadumu kwa siku moja, kutokana na kufuata kwake juhudi kubwa na muhimu za Sheikh wa Al-Azhar na Taasisi ya Al-Azhar za kupanda mbegu za kheri na amani kati ya watu na kupambana na aina zote za vurugu na hotuba ya chuki, nazo ndizo zinazotakiwa na shirika la kimarekani kwa maendeleo kwa ajili ya kumheshimu mwanadamu, na kutoa juhudi zinazolenga kutafuta na kutatua matatizo za maendeleo ya kiuchumi na uhuru wa kidini, akisisitiza juu ya hamu ya shirika ya kusaidiana na Al-Azhar kwa ajili ya kung'oa mizizi ya chuki na ugaidi ulimwenguni, na kwamba Al-Azhar ni taasisi ya kidini iliyo muhimu zaidi ambai inatoa mabalozi wanaoenea ulimwenguni kote, akiongeza kuwa juhudi hizo zinazotolewa na Al-Azhar hazihudumu Misri tu, bali pia Uislamu kwa ujumla.
Kwa upande wake, mheshimiwa Imam mkuu alisema kuwa njia iliyo rahisi kabisa ya kutatua matatizo ya maendeleo ya kiuchumi ulimwenguni ni kusimamisha vita na hotuba ya chuki na kupambana na fikra kali na ugaidi, na kupambana na wenye msimamo mkali, bila kujali dini yao, na sio kupigana na dini yenyewe, na hiyo yote haitakuwa ila baada ya kutafuta sababu za kweli za ugaidi na kuzitatua kwa ukweli na usawa, na kufanya lengo kuu ni kumlinda bila ya kuzingatia chochote, akisisitiza mheshimiwa kwamba Al-Azhar ndiye dhamiri ya umma na ndiye wa kwanza iliyogundua hatari za fikra kali na ugaidi na kushughulika kwa kuipigana nazo, Na linalotusukuma kufanya hivyo ni jukumu letu la kidini na la kibinadamu.
 

Print
Tags:
Rate this article:
4.0

Please login or register to post comments.