Ugaidi na athari zake mbaya juu ya uchumi wa nchi

  • | Tuesday, 16 February, 2021
Ugaidi na athari zake mbaya juu ya uchumi wa nchi

     Bila shaka sisi sote tunajua kuwa ugaidi ni mojawapo ya changamoto na matatizo makubwa yanayoukabili ulimwengu kote katika wakati wa hivi sasa, bali ndio tatizo hatari zaidi linalohangaisha jamii za kibinadamu, na hivyo kutokana na athari zake mbya juu ya maendeleo na ustawi wa kimataifa.
Uchumi wa nchi huathirika sana na vitendo vya kigaidi vinavyoshambuliwa na makundi yenye siasa kali, ambapo takwimu za kimataifa zinaashiria kwamba hasara ya nchi moja ilivyosababishwa na mashambulizi ya kigaidi inafika dola milioni 12 kwa mwezi, na kila siku hasara hiyo inaongezeka  katika nyanja zote za kiuchumi.
Makundi ya kigaidi hulenga kwa mashambulizi yake – kama kawaida yake – kudhoofisha uchumi wa nchi, na kudamaza maisha ya watu. Kwa hivyo makundi hayo yanaelekea kushambulia viwanja vya ndege, sekta ya utalii, uvuvi, petrol na gesi asili, bandari, na sekta zingine ambazo zinaathiria vibaya hali ya nchi.
Vilevile, ugaidi unasababisha kupunguza uwekezaji wa kimataifa katika nchi na ukosefu wa ajira, mfumuko wa bei, kufilisika kwa mashirika ya kifedha, kusitasita makampuni na kadhalika.
Mbali na hasara ya kiuchumi kutokana na vitendo vya kigaidi, nchi inatumia fedha nyingi katika kupambana na ugaidi, badala ya kuzitumia katika miradi ya kimaendeleo inayowahudumia wananchi kama vile barabara, shule, hospitali n.k. Kwa ujumla, tunaweza kusema kwamba ugaidi ni adui wa uchumi.
Hakika kuhisi usalama na amani ni neema kubwa na ndio msingi wa mafaniko, kwani taasisi zote haziwezi kukua na kupata maendeleo katika kazi zake ila katika kuwepo mazingira ya amani na ya usalama. 
Kwa hiyo basi, Kituo cha Uangalizi cha Al-Azhar kwa kupambana na mawazo makali kinaona kwamba nchi zinazopambana na makundi ya kigaidi zinapaswa kutekeleza mambo matatu muhimu; la kwanza ni kujitahidi katika kupambana na makundi hayo kwa kutumia silaha kupitia vikosi vya kijeshi. La pili ni kuhakikisha usalama wa kifikra hasa katika akili za vijana ambao ni rahisi sana kuvutiwa na makundi ya kigaidi, na kuimarisha uzalendo na kuipenda nchi, na jambo hilo linahakikishwa kupitia wahusika na maulamaa. La tatu ni kushajiisha wananchi kufanya bidii na kukuza uchumi wa nchi. Na kituo cha Al-Azaha kinaongeza kuwa amani na usalama na utulivu ni njia ya mafanikio na maendeleo. 
 
 

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
3.9

Please login or register to post comments.