Vyombo vya Habari na Mitandao ya Mawasiliano ya kijamii kati ya kueneza na kupambana na fikra kali

  • | Saturday, 12 June, 2021
Vyombo vya Habari na Mitandao ya Mawasiliano ya kijamii  kati ya kueneza na kupambana na fikra kali

    Kwa hakika makundi ya kigaidi yanatumia silaha nyingine mbali na mabunduki na mabomo, kwa kuwa makundi haya yametambua kuwa vita si lazima iwe kwa kutumia bunduki na risasi tu, bali zipo silaha nyinginezo ambazo hatari yake huwa kubwa zaidi kuliko silaha ya kawaida.
Na kwa kuwa makundi haya yanafanya juhudi kubwa katika kueneza fikra na kutekeleza mikakati yake, yamekusudia kutumia zana na mbinu mbalimbali kwa ajili ya kuhakikisha matarajio na malengo yake. Miongoni mwa mbinu za makundi ya kigaidi katika kueneza fikra kali na kuwavuta vijana wajiunge nayo ni kutumia vyombo vya habari kwa aina zake tofauti kwa lengo la kujitambulisha na kuwavuta watu kwake.
Hivyo, vyombo vya habari ni zana muhimu mno kwa makundi ya kigaidi zinazochangia kwa kiasi kikubwa katika kutangaza fikra zake na kufanikisha mikakati yake mabaya. Pia, ni jambao la kuzingatiwa kuwa namna magaidi wanavyotumia vyombo vya habari inathibitisha mambo mawili makuu:
1-    Kwamba makundi haya yanatambua umuhimu wa kutumia vyombo vya habari kufikia malengo yake na kutekeleza mipango yake, kwa kuwa jamii yetu ya kisasa inaathirika sana kwa vyombo vya habari mpaka vyombo hivyo vinaendesha maisha ya wengi duniani.
2-    Kwamba juhudi yoyote ya kupambana na ugaidi na fikra kali haiwezi kuwa mbali na kutafuta njia ya kuchambua na kuhakiki mtindo wa kifikra wa makundi ya kigaidi kupitia zana zao za mawasiliano na matangazo yao wanayoyatoa katika vyombo vya habari kwa aina zake tofauti.
Hata hivyo, majiribio mengi ya kuchambua yaliyomo (content) ya machapisho ya makundi ya kigaidi kama vile; magazeti, kanda za video n.k. yalifanywa, lakini kwa bahati mbaya majaribio haya yameishia kuainisha na kutaja shughuli wanazozifanya magaidi na wenye fikra kali na kutoa ishara za juu juu kuhusu namna makundi haya walivyofaidika kwa matumizi ya vyombo vya habari kwa lengo la kutangaza sera zake na kuwavuta wengine kujiunga nayo.
Katika makala hii tunaongeza jaribio jipya la kuchambua mchango wa vyombo vya habari katika kukuza na kueneza fikra kali na kufanikisha mipango ya makundi ya kigaidi, wakati huo huo ni jaribio la kuashiria namna vyombo hivyo venyewe vinaweza kuwa njia ya msingi ya kupambana fikra hizo.
Vyombo vya habari kwa mtazamo wa magaidi:
Kwa kuangalia mwenendo wa makundi ya kigaidi katika kutumia vyombo vya habari kwa kufanikisha mipango yake, tunabainika kuwa aghalabu ya makundi ya kigaidi yanatumia vyombo vya habari kupitia magazeti, video na machapisho mengine kwa kuwashawishi vijana kujiunga nayo na pia kwa ajili ya kutangaza mashambulio wanayoyatekeleza, jambo linalomaanisha kuwa vyombo vya habari kwa mtazamo wa makundi ya kigaidi yapo kwa aina mbili:
1-     Matoleo ya kutangaza sera za makundi na vyanzo vyake vya kifikra kwa lengo la kushawishi watu na kuwavuta wajiunge nayo.
2-    Matoleo ya kurekodi vitendo vya makundi hayo kama vile; mashambulio, mazoezi n.k.
Kwa ujumla, matumizi ya makundi ya kigaidi kwa vyombo vya habari na zana za mawasiliano hasa mitandao ya mawasiliano ya kijamii; (Facebook, Twitter, Instagram, Telegram) yamekua sana kwa kupitia wakati kwa kulinganisha hali ilivyo hapo zamani na hali ilivyo katika miaka ya hivi karibuni, jambo linaloenda sambamba na mabadiliko ya enzi na maendeleo ya teknolojia.
Vile vile vyombo vya habari na mitandao ya mawasiliano ya kijamii zinategemewa sana na makundi ya kigaidi katika kueneza fikra na sera zake na kuonyesha harakati zake za kupitisha udhibiti wake katika nchi mbalimbali duniani.
Namna ya kupambana:
Kwa hiyo, juhudi za kupambana na fikra kali na ugaidi hazina budi kushughulikia na kuchambua matumizi ya makundi haya kwa vyombo vya habari katika kukuza na kunadi fikra zake, mapambano hayo yanaweza kuwa katika viwango vitatu vifuatavyo:
1.    Kukusanya data zinazohusiana na makundi haya katika vyombo vya habari na mitandao ya mawasiliano ya kijamii.
2.    Kuzigawa data hii na kupambanua data zinazogusia tawasifu wa makundi haya na harakati zake na data zinazokusudia kueneza fikra na mikakati ya makindi hayo.
3.    Kuchambua kwa makini data zinazofungamana na makundi haya sawa zile zinazoeleza shughuli zake au zile zinazokusanya fikra na mikakati.
La kuzingatiwa kuwa katika upambanuzi na uchamuzi wa data, tunatakiwa kuwa na uelewa wa kutosha kwa ajili ya kutambua data na kuchambua na kuyajibu kwa hoja imara.
Pia, mchambuzi anapaswa kuwa na uelewa wa kutosha kwa ukweli wa makindi haya na misingi yake ya kifikra, pamoja na misingi ya kifikra ya pande za kusambaza habari au data zinazohusiana na makundi hayo.
Licha ya hayo, inatajwa kuwa mapambano ya kifikra dhidi ya makundi ya kigaidi yanahitajika kuwa na ujumla wa namna ya pekee, ambapo juhudi za kupambana na ugaidi isitoshe kuwa katika kiwango cha kijeshi na kiusalama tu, bali yapo mapambana ya aina nyingine ambayo yana umuhimu mkubwa.


Kwa upande wa vyombo vya habari tunaweza kusema kuwa ni silaha yenye ncha mbili, ambapo vyombo hivyo vinaweza kuchangia kueneza fikra za kigaidi kama wanavyofanya kupitia zana zao za habari yakiwemo magazeti na matoleo mengi ya kusoma, kuangalia au kusikia kwa lugha mbalimbali.
Ncha ya pili ya vyombo vya habari ni hali ambayo tunaweza kuiita (Ushawishi Bure) au (Matangazo ya Bure) kwa jina la makundi ya kigaidi ambayo humaanisha kuyatangazia makundi haya bila ya kuwa na kusudio lolote. Hali hiyo hutukia wakati vyombo vya habari ya kawaida na mpaka watu binafsi wanaposambaza habari za makundi haya na shughuli zao kwa nia ya kutangaza maovu yao na kuwafedhesha, lakini kwa hakika mbinu hiyo imefeli katika kuchukiza watu katika makundi haya na kuwafanye vijana wajiepukane nayo, bali – kwa bahati mbaya – wengi wakawa na udadisi mkubwa wa kutaka kuelewa na kufahamu zaidi kuhusu makundi hayo.
Kutokana na hayo, tunabainisha kuwa vyombo vya habari na mitandao ya mawasiliano ya kijamii katika siku zetu hizi zinahitajika kuangaliwa kwa mtazamo wa aina yake, kwa kuwa suala la kugusia habari za makundi ya kigaidi linaweza kupelekea matokeo mabaya zaidi lisingetolewa kwa namna ya kupambanua baina ya kuyashutumu makundi haya na kuyatangazia.


Wengi wa waliojiunga na makundi ya kigaidi kama vile; Daesh, Al-Shabab, Boko Haram na makundi mengine hawakuwa na maelezo yoyote kuhusu makundi haya kabla hawajajiunga nayo, lakini walipata kuelewa kuhusu makundi haya kupitia kwa vyombo vya habari ama mitandao ya mawasiliano ya kijamii.
Hata hivyo, vyombo vya habari na mitandao ya kijamii inaweza kuchangia sana katika juhudi za kupambana na kukausha machimbuko la ugaidi na fikra kali kwa kutakeleza mikakati madhubuti ya kuwatahadharisha vijana kutokana na ushawishi na ulaghai wa makundi haya, pamoja na kutosambaza habari za makundi haya kwa namna inayowavutia watu.
Kwa kweli, suala la uhusiano uliopo baina ya vyombo vya habari na mitandao ya mawasiliano ya kijamii na kuenea kwa fikra kali na ugaidi ni suala linalostahiki kujadiliwa kwa makini kwa lengo la kuainisha njia bora ya kutumia vyombo hivyo ipasavyo kwa kukomehsa juhudi za magaidi za kueneza fikra zao.
Damu nyingi zimegawika na wahanga wengi wamekosa maisha yao na makazi yao pamoja na maelfu ya waathirika kwa ugaidi na vitendo vya kikatili wanavyovitekeleza magaidi wakifuata udanganyifu na matamanio maovu ya wahalifu na maadui wa ubinadamu na amani.
Kwa kutumia silaha hiyo hiyo wanayoitumia magaidi; vyombo vya habari na mitandao ya mawasiliano ya kijamii ulimwengu wetu wa kisasa unaweza kushinda vita yake dhidi ya ugaidi na vurugu sharti kutambua mbinu inayofaa katika mapambano haya.
Mwishoni, Kituo cha uangalizi cha Al-Azhar cha Kupambana na fikra kali kinapenda kuwahamasisha waandishi wa habari, wanaharakati wa mitandao ya kijamii na wadau wa kushughulikia masuala ya kuchambua na kupambana na fikra kali wajitahidi katika kuongeza juhudi zao za kufichua ukweli wa makundi ya kigaidi na kuwatahadharisha vijana na umma kwa jumla kutoka sumu inayochanganyikiwa asali katika baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya mawasiliano ya kijamii kwa lengo la kuwadanganya watu.
Pia, kituo hicho kinatoa angalizo muhimu kuwa namna ya kutoa taarifa inayowahusu magaidi inaweza kuwa sababu ya ukuzaji wa makundi haya na kuyapa nguvu badala ya kupigana nayo na kuwakinga watu hasa vijana kutokana na fikra mbaya zinazotolewa na makundi haya.

   
 

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
4.0

Please login or register to post comments.