Jukumu la Uislamu katika uongufo wa Dhamira ya Kibinadamu

  • | Tuesday, 15 June, 2021
Jukumu la Uislamu katika uongufo wa Dhamira ya Kibinadamu

  
     Shughuli ya kwanza kwa Uislamu ni dhamira kama walivyosema wanachuoni wa maadili – hakika amani ya moyo huu kutoka kasoro, na uthabiti wa mwelekeo wake kwa heri, inamaanisha kwamba kuna mapatano mengi na neema kutoka Mwenyezi Mungu, Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W amesema: (kwa katika Allah hatazami kwa sura zenu wala mali zenu bali hutazama kwa nyoyo zenu na amali zenu. Uongufo ndani hapa- na aliashiria katika kifua chake..).
Ndiyo kifua kikunjufu kwa ukweli, chenye utulivu katika minhaji njema kinaaminiwa juu ya kichembe na kikubwa, na kinapata muhuri yake ya kisafi juu ya kila kitu na kinazungukwa na baraka za Mwenyezi Mungu, kwani uhusiano wake naye wenye imara na unaendelea daima..
Na tunapenda kupiga mifano inayobainisha vipi moyo inakuwa mzima au vipi dhamira inakuwa safi..
Mtu katika utoto wake na ujana wake inawezekana alipenda kuonekana, na alifurahisha na anaposikia kusifu kwake, na amekuwa alifanya bidii katika lengo hili.. kujionyesha katika tabia ya ubinadamu si ajaabu, na kuridhisha watu hasa katika pande za kwanza kutoka umri ya mtu ni lengo la kikweli, kisha anakua na maono yake yametukuka, na  amerejea kwa Mwenyezi Mungu, mtu anayejionyesha haoni ila watu, yeye anafanya kwa ajili wao, lakini mtu mwenye mwaminifu ameona Mola wa watu basi kwa hivyo anafanya kwa ajili yake ya Mwenyezi Mungu.
Na dini inazingatia usamehe huu, dini inausia na kufanya kazi  kiaminifu  kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kwani mwanadamu angeshiriki watu pamoja na Mwenyezi Mungu ili apate radhi zao basi Mwenyezi Mungu haikubali kazi yake!
Hakika Mwenyezi Mungu haikubali kutoka kazi ila inayokuwa kwa ajili ya peke yake, na kwa hivyo Mumini wa kweli  anaonekana anafanya kazi yake vizuri na hufanya wajibu wake, ni sawa inaonekana na watu ama haionekani, inasifiwa na wakuu wake ama wanaichukia, yeye anaifanya kazi kwa bidii katika hali yoyote na mazingira yoyote.
Na mwanadamu kwa tabia anapenda kumlipwa juu ya kazi yake kifedha au kimaana, na labda anaacha kazi wakati singepatii malipo ya mapema, na ameichelewesha kazi hii au haijali kuifanya anapokuta malipo machache au katika wakati wa baadaye.. lakini yeye kama anasafisha uyakini wake kutendaji kwake kutakuwa bora! Na anahifadhia thawabu yake kutoka Mola wake! Na anazingatia iliyochukua katika siku ya mwisho ni bora na yenye kudumu zaidi..
Jukumu la dhamira hapa ni kuthibitisha mtu juu ya kutekeleza iliyo juu yake hata lau watu wengine wanaikanusha, na katika Hadithi ya Mtume S.A.W. amesema kwa  maansari: " tutakutana baada ya maisha yangu watu waliojipendeza nafsi zao! Walisema: je, utuagize kwa nani? Alisema: toeni iliyo juu yenu, na ulizeni Mwenyezi Mungu iliyo nayo!!
Jukumu linafanywa katika sura kamili, na malipo juu ya Mwenyezi Mungu na Mambo yote ni ya Mwenyezi Mungu.!!
Hakika kukimbilia kwa utoaji lazima kuwa na sababu ya kidhati, lengo yake ni kupata radhi ya Mwenyezi Mungu hata lau watu walikanusha: Mwenyezi Mungu Alisema: (Ambaye hutoa mali yake kwa ajili ya kujitakasa. *Na wala si kwa kuwa yupo yeyote aliye mfanyiahisani ndio anamlipa. *Ila ni kutaka radhi ya Mola wake Mlezi aliye juu kabisa. *Naye atakuja ridhika!){ Al-Layl, 18-21}
Na tunazingatia aya ya Qurani katika kusifu dhamira hizi zilizosafishwa na kasoro, Mwenyezi Mungu amesema: (Siku ambayo kwamba mali hayatoi faa kitu wala wana.* Isipo kuwa mwenye kumjia Mwenyezi Mungu na moyo safi.) {Ash-shura, 88:89}.. safi kutoka uchafu wa udanganyifu na wazimu wa kujiona na kuangaliwa na watu! Mtu asifanya au asiyeboresha kazi yake hata alisikia usifu wake au alipata pesa hafanyi kitu chochote inapokatazwa thamani, na watu waliondoka mbali!
Maana ya hayo ni kwamba heri kwa maoni yake ni lengo lililopita haraka sio kusudi la kiasili, moyo wake kikweli halina mapenzi kwa heri na kukimbilia kidhati kwake, hakika huu ni moyo si safi.
Na labda moyo ulichangania na matarajio ya dunia kwa mali au shani, lakini Imani inayafukuza na dhamira inabakia kushikana na Mola wake wanampendelea kuliko wote, na hii maana ya kauli ya Mwenyezi Mungu: (Mwenye kumwogopa Mwingi wa Rehema hali kuwa hamwoni, na akaja kwa moyo ulioelekea* (Ataambiwa) ingieni kwa salama. Hiyo ndiyo siku ya daima dawamu.) {Qaf,33:34}
Hakika si kigeni juu ya watu kuwapendeza mali na shani, lakini mapenzi hayo lazima kushindwa mbele ya radhi ya Mwenyezi Mungu na kungojea utoaji wake!
Na tungetafitia juu ya sababu za matetemeko yaliyoteteka umma tungezikuta dhamira hizi zilizokufa, nyoyo hizi zilizokauka, hazina heshima wala hafurahishi na wongofu na halichuki na maovu.
Sunna ilitaja mifano kwa dhamira yenye uhai inaposhinda juu ya kila vishawishi na ilishinda wasiwasi na iliogolea kwa nguvu dhidi ya mkondo na inaokoka!!
Na kutokana na Abo-Dhar R.A. amesema kwamba Mtume S.A.W amesema: (watu watatu wanapendwa na Mwenyezi Mungu, na watu watatu wengine waliochukuzwa naye Mwenyezi Mungu. na kuhusu watu waliopendwa na Mwenyezi Mungu ni: mtu alikuja kwa watu na aliwauliza wao kwa jina la Mwenyezi Mungu, na hakuwauliza wao kwa ukoo baina wao, lakini wao walimzuia ila moja wao alibakia nyuma wao, na alimpa kwa siri, na hajui kwa atia yake ila Mwenyezi Mungu na aliyempewa. Na watu walitembea usiku wao hata wangekuwa walipenda kulala zaidi kuliko kitu chochote kilichosawazisha na walichuka kulala ila mtu moja walisimamisha ili kunisifu na alisoma aya zangu… na mtu alikuwa katika kikosi na walikutana na adui, na walishindwa, lakini yeye aliendelea kupiga vita na alikabili adui kwa kifua chake hata atauwa au atashinda, na kuhusu watu watatu waliochukuzwa naye Mwenyezi Mungu ni mzee mzinifu, fakiri mdanganyifu, na mtajiri dhalimu…"
Ilibainika kwamba watu watatu wengine nyoyo zao zilikufa, na walihalilisha maovu hata lau sababu zake zilizoyasukuma kwa maovu hayo ni dhaifu.
Na kutoka aina ya dhamira zenye uhai, iliyotajwa na hadithi nyingine, juu ya mtu aliyeweza kufanya maovu, lakini yeye alipuuza laza zake na alihifadhia nafsi yake mwenyewe katika hali ya wongofu, na uhusiano wake na Mwenyezi Mungu ni safi.
Na aina ya mtu huyu aliyeajiria mfanyakazi, na mfanyakazi huyu alitimiza kazi yake kisha aliondoka kabla ya kuchukua ajira yake na baada miaka mengi mfanyakazi huyu alirejea ili kuchukua ajira yake ya zamani! Na mwenye kazi alizalisha ajira yake ya mfanyakazi na ajira hii ilikuwa mali nyingi kama utajiri! Na alipokuja mfanyakazi alichukua ajira na uzalishaji wake kutoka mwenye kazi na mfanyakazi alikuwa mstaajabu!
Kituo cha Uangalizi cha Al_Azhar kwa kupambana na fikra kali kinasisitiza kwamba mafundisho ya kidini na maagizo ya kimungu na maana zilizomo zina uwezo wa kufanya ubinadamu kuwa na furaha na raha mustarehe, na kuhakikisha maadili ya udugu wa kibinadamu, na kutoa ubinadamu wote kutoka kwa mizozo yake kubwa. Na kinakiri kwamba Imani inaweka nguzi nguvu kwa mwenendo, na inafanya moyo kama mlindaji msikivu aliyelinda haki na wajibu, bila ya udhalimu au fujo..!
Hakika moyo safi wenye upendo kwa haki uliozingatia juu ya heshima, aliyeshinda kujipendeza, mpenda wa watu haukuwa ila kwa imani thabiti na uhusiano kwa daima na Mwenyezi Mungu peke yake.
Ni ukweli  kwamba simulizi la Qurani juu ya Mwenyezi Mungu na juu ya historia ndefu wa waliotangulia, na juu ya Ufufuo na siku ya kulipwa na thawabu na adhabu na zilizoamirishwa na Mwenyezi Mungu kutoka ibada nyingi, mambo hayo wote ni  vipengele vya kuhakikisha usalama wa moyo na mwelekeo wake thabiti kwa haki na heri.


 

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.