Kituo cha Uangalizi cha Al-Azhar cha Kupambana na fikra kali kilipokea jana Jumapili, Mheshimiwa Balozi Masaaki Noki, Balozi wa Japani huko Cairo, ili kujua jukumu la Kituo cha Uangalizi katika kupambana na fikra kali, na ufuatiliaji wake bila kuchoka kwa shughuli za makundi ya kigaidi ulimwenguni kote, na pia kuzichambua, kuzikanusha, na kujibu tuhuma, ili Kuzuia fikra zake kuingia akilini.
Wakati wa ziara yake kwa Kituo cha Uangalizi, Balozi Masaaki Noki alisema kuwa Al-Azhar hufanya juhudi kubwa na kweli, ili kueneza na kuimarisha picha sahihi ya Uislamu, akisisitiza kuwa ziara yake kwenye Kituo cha Uangalizi ilikuja kwa lengo la kujua zaidi maoni na njia ambazo Kituo cha Uangalizi hufanya kazi, katika wakati huo huo wa kuongezeka kwa kampeni zenye fikra kali za kuwavuta vijana, zilizosababishwa na baadhi ya watu wasiofahamu Uislamu, na zilizosababisha misiba mingi ulimwenguni, ambayo baadhi ya wahasiriwa wake ni kutoka Japani.
Balozi wa Japani ameongeza kuwa juhudi za Al-Azhar katika kueneza hotuba ya wastani na kupambana na fikra zisizosahihi ni muhimu, ili Waislamu wanaweza kuelewa dini hii vizuri na pia wasio Waislamu. Akasema pia "Nimejua kwamba mnafanya kazi kwa lugha 13 na kwamba umefanya kazi nyingi nzuri ambazo zinapaswa kufikia umma, na kwa juhudi hizi endelevu, nzuri, na uvumilivu katika kazi, naamini kuwa utafanikiwa zaidi na zaidi, nakutakia kila la kheri kwenu, na tutafurahi kwa kuwasiliana na kituo chenu.”
Pia, wanachama wa Kituo cha Uangalizi cha Al-Azhar walizionyesha juhudi zao za kusahihisha maoni yasiyosahihi kuhusu Uisilamu, na kupambana na hotuba yenye fikra kali yaliyoenezwa na makundi yenye fikra kali, wakisisitiza kuwa juhudi hizi zitaendelea kuongezwa kwa vifaa vya elektroniki katika kipindi kijacho, haswa kwa kuzingatia tafiti na takwimu ambazo zinaonyesha viwango vya juu kuhusu matumizi ya mtandao kwa sababu ya janga la Corona na hatua na changamoto zilizowekwa.