Kituo cha uangalizi cha Al-Azhar chapokea Waziri wa Mambo ya nje wa Serbia na ujumbe ulioandamana naye ili kutambua juhudi zake katika kupambana na fikra kali

  • | Monday, 23 August, 2021
Kituo cha uangalizi cha Al-Azhar chapokea Waziri wa Mambo ya nje wa Serbia na ujumbe ulioandamana naye ili kutambua juhudi zake katika kupambana na fikra kali

     Kituo cha uangalizi cha Al-Azhar cha kupambana na fikra kali kilipokea, leo, Jumatatu, Agosti 23, Waziri wa Mambo ya nje wa Serbia Nikola Silakovic, na ujumbe ulioandamana naye; Ili kutambua juhudi za kituo katika uwanja wa kupambana na ugaidi na fikra kali, na kusahihisha maoni mabaya ya makundi yenye fikra kali, na kuwafahamisha vijana kwa hatari zake.
kupitia ziara hiyo, kituo kwa sehemu zake 13, kilimwonyesha tafiti, ripoti, kampeni na vitabu vilivyoongea fikra kali kwa kukosoa na Kuchambua; kwa lengo la kubainisha hatari zake mbele ya vijana ili kuwalinda, pamoja na kumwonyesha njia ya kazi ya kila sehemu na majukumu zilizopewa.
Mwishoni wa ziara hiyo, Waziri wa Mambo ya nje wa Serbia Nikola Silakovic alizisifu juhudi zinazofanywa na Al-Azhar, kupitia kituo cha uangalizi cha Al-Azhar na sehemu zake kuhusu kupambana na fikra kali na kupambana na makundi.
 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.