Al-Azhar ni Kibla cha kisayansi na marejeo ya kidini kwa Waafrika

  • | Tuesday, 23 November, 2021
Al-Azhar ni Kibla cha kisayansi na marejeo ya kidini kwa Waafrika

     Bila shaka, jukumu la kimsingi liliyofanywa na Al-Azhar barani Afrika katika masuala ya misaada na katika nyanja za elimu na afya na kutuma misafara ya kisayansi, ulinganiaji na matibabu halifichwi na mtu yeyote, hadi kwamba  imesifiwa na mabalozi na marais wengi wa nchi za Afrika, miongoni mwao ni Waziri wa elimu katika Jimbo la Yobe nchini Nigeria, aliyesema hivi karibuni: "Al_Azhar Al_Sharif ni Kibla cha kisayansi na marejeo ya kidini kwetu", Kuna ushirikiano mkubwa sana katika nyanja mbalimbali, kama vile kufundisha lugha ya Kiarabu na uwanja wa kupambana na ugaidi na fikra kali kupitia ushirikiano na taasisi la Dunia la Wahitimu wa Al_Azhar. 
Miongoni mwa mambo muhimu ambayo Al_Azhar iliyafanya katika Afrika:
1- Misafara ya amani: Hii inatokana na jukumu la Al_Azhar katika kufanikisha na kuthibitisha maadili ya mazungumzo na kuishi pamoja; Ambapo Al_Azhar Al_Sharif, kwa ushirikiano na Baraza la Wenye hikima wa Waislamu, walizindua misafara mitano ya amani, ambayo ni katika nchi zifuatazo: Afrika Kusini, Chad, Afrika ya Kati, Nigeria, na Kenya; Kwa lengo la kuimarisha mazungumzo ya kidini ya wastani, kufikia mawasiliano yenye ufanisi kati ya watu wa bara la Afrika, na kukataa na kuepusha mgawanyiko kati ya Waislamu na Wakristo, ili kusisitiza umuhimu wa amani ya ndani katika utulivu wa mataifa na furaha ya binadamu, kwa kuzingatia msimamo wa Sharia ya kiislamu kuhusu kuachana na vurugu na fikra kali.
2- Semina na mikutano ya kielimu: Mnamo Aprili 2019, Kituo cha Uangalizi cha Al_Azhar kiliandaa semina kwa anwani: "Jukumu la Al_Azhar katika kuimarisha Utamaduni wa Amani na Kupambana na fikra kali barani Afrika",  katika Jiji la Al- Bouth Al- Islamia, ndani ya mfumo wa mpango wa kielimu, kiutamaduni, na ufahamisha unaotolewa kwa wanafunzi wa Al-Azhar wa Al- Bouth Al- Islamia, katika uwanja wa uangalifu wa Al-Azhar juu ya kuwafahamisha vijana kuhusu hatari ya ugaidi na fikra kali, pamoja na uangalifu wa kituo cha uangalizi cha Al-Azhar juu ya kuwazuia na kuwakinga vijana kutoka kuanguka katika makucha ya fikra kali na uharibifu.
Pia, Kuundwa kwa mpango huu kunakuja ndani ya mfumo wa juhudi za Al_Azhar Al-Sharif na taasisi zingine za serikali wakati wa Urais wa Misri kwa Umoja wa Afrika mnamo 2019. Kupitia siku hizo tatu, mpango huo ulishughulikia na magaidi mashuhuri zaidi na makundi ya kigaidi wanaofanya kazi kwa uwingi ndani ya bara la Afrika, na kujadili misingi muhimu ya kiakili ambayo watu hawa wanatoka, pia ukaonyesha na ukabainisha njia za kupambana na nguvu hizi za giza, na juhudi za kituo cha uangalizi cha Al_Azhar katika kutoa ulinzi wa kweli kwa vijana wa bara la Afrika; Ili kuwalinda wao wasianguke katika makucha ya vikundi hivi vya fikra kali.
Kwa upande wake, kituo cha uangalizi cha Al_Azhar cha Kupambana na fikra kali kina nia ya dhati ya kuendelea na juhudi zake za kubainisha sura sahihi ya Uislamu na kujibu makundi yenye fikra kali ambao wamepotosha sura hiyo sahihi. kituo cha uangalizi kilizindua mfululizo wa matoleo ya video kwa lengo la kueneza mawazo ya wastani, kujibu tuhuma , na kusahihisha dhana potofu ambayo vikundi vya fikra kali vinaenea kati ya vijana, pia  kituo cha uangalizi kimeandaa hotuba na jumbe za kisasa ambazo zinahutubia vijana kwa lugha wanayotumia, na kwa njia ambazo zimekuwa nguzo kuu katika kuunda akili za vijana na kuunda mielekeo yao ya kifikra.
Miongoni mwa matoleo hayo ni: Matoleo mawili, moja yao ni kwa lugha ya Kihausa likilenga eneo la Afrika ya Magharibi, ambapo kundi la Nigeria Boko Haram, na lingine kwa lugha ya Kiswahili likilenga eneo la Afrika ya Mashariki, ambapo kundi la Al Shabab Al Somalia.
Pia, kituo cha uangalizi kinasisitiza msaada na kuwapa mkono wake kwa hatua hizo muhimu ili kufikia jukumu la chanya na lenye ufanisi katika maendeleo, ambalo linawainua watu wa bara hilo na kuwaondoa mbali na mawazo hayo haribifu na makundi yenye fikra kali, kupitia ushiriki huo mkubwa wa Al_Azhar ambayo ni msikiti na chuo kikuu, katika kuwapa mkono kwa Waafrika ili kuimarisha elimu na afya na kueneza sahihi ya dini.
 

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.