Dhana ya Uraia kati ya mtazamo wa sheria ya kiislamu na uelewa wa makundi ya kigaidi

  • | Tuesday, 4 January, 2022
Dhana ya Uraia kati ya mtazamo wa sheria ya kiislamu na uelewa wa makundi ya kigaidi

 

     Miongoni mwa sifa za kimaumbile na hisia za kibinadamu ambazo wanadamu wameumbwa nazo, hisia ya kuipenda nchi na kusikia fahari kwa kujiunga nayo, ambapo yeyote mwenye akili timamu huwa na hamu ya kuitetea nchi yake ambayo ni nyumba yake ya kwanza na pahala pa kuzaliwa na kuishi na kuzikwa.

Kuipenda nchi na watu wake ni sifa ya msingi inayotakikana kwa ajili ya kudumisha amani na utulivu, pamoja na kufikia malengo ya maendeleo, ambapo nchi zilizopiga hatua kubwa katika kuhakikisha maendeleo na ustawi ni zile zinazo wananchi wanaopendana na kusaidiana katika kuijenga nchi yao na kuendeleza jamii yao. Ilhali zile nchi zilizokosa hisia hizo zikajaa chuki, migogoro na migombano zinateseka kukosa amani na utulivu wa kutosha wa kutekeleza majukumu yake.

 

Ukimwuliza mtu yeyote: Je, unapenda nchi yako?! Jibu la kimantiki ni ndiyo, bila shaka japokuwa baadhi ya changamoto na magumu anayoyapata nchini mwake lakini maumbile yaliyo sawa yanamwelekeza mtu aipende na kufungamana na nchi yake kwa namna inayodhihirisha usahihi na usawa wa fikra yake na uongofu wa tabia zake.

  Kwa hakika, kuipenda nchi ni sifa mojawapo sifa za kimaumbile wanazo wanadamu wote, kwa hiyo Mtume wetu alishtuka aliposikia kutoka Waraqa bin Noufal kwamba watu wake watamlazimisha ahamie nchi yake kwa kuwa anaipenda sana na amekuwa hataki kuihamia kabisa, na alipokuwa akitoka alisema kauli yake: "Naapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba Makka ndiko nchi bora inayopendwa zaidi kwa Mwenyezi Mungu na kwangu pia na angalau watu wake wamenilazimisha nihamie nisingetoke"

Na kuipenda nchi si sifa ya wanadamu tu, bali wanyama pia, kwa hiyo si jambo la kushangaza kuwa sheria imekuja kuwahimiza wananchi kuipenda na kuitetea na kupigana kwa ajili yake hata mmoja akipotezwa na maisha yake huwa na fadhila kubwa nayo ni kuwa shahidi aliyekufa kwa ajili ya nchi yake, ambapo shahidi huyu amepewa cheo cha juu kabisa na kutunukiwa na Mwenyezi Mungu na watu pia, Mwenyezi Mungu Amesema: {Wala msiseme kwa wale walio uwawa katika Njia ya Mwenyezi Mungu ni maiti; bali hao ni wahai, lakini nyinyi hamtambui} [2/154].

Zaidi ya hayo Mwenyezi Mungu Amewaruhusia wananchi kutangaza upendo wao kwa nchi na kuwa wako tayari kufanya lolote kwa ajili ya nchi hiyo, hata ikiwa ni kupigana na wale wanaotaka kuiharibu nchi na kuwatokeza watu wake kutoka makwao: {Hakika Mwenyezi Mungu anakukatazeni kufanya urafiki na wale walio kupigeni vita, na wakakutoeni makwenu,na wakasaidia katika kufukuzwa kwenu. Na wanaowafanya hao marafiki basi hao ndio madhaalimu} [60/9].

Wakati huo huo Mwenyezi Mungu Amewaelekeza waumini kuwapenda na kuamiliana na wale wasiofanya uadui wowote dhidi ya nchi kwa wema na uadilifu hata wakiwa si waislamu: {Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu} [60/8].

Kwa ajili ya kubainisha tofauti iliyopo kati ya ukweli wa dhana ya uraia katika mtazamo wa sheria ya kiislamu na uelewa wa makundi ya kigaidi hatuna budi kutaja waliyoyasema wenye fikra kali kuhusu dhana hiyo kama ifuatavyo:

Dhana ya uraia kwa mtazamo wa makundi ya kigaidi:

Kwa kuwa makundi ya kigaidi hawatambui haki ya nchi iliyopo juu ya wananchi wake wakakana uwajibu wa kujiunga na nchi na kuona kuwa kuipenda nchi siyo jambo la lazima kisheria, bali walitoa fatwa kwamba kujiunga na makundi yao ni muhimu zaidi kuliko kujiunga na nchi, na kwamba uanachama katika makundi yao ni sababu ya kurahisisha mambo ya mwislamu kidini na dunia ama kujiunga na nchi humbana mtu na kumnyima uhuru wake wa kufanya ibada na kutekeleza maagizo ya dini na kuepukana na makatazo yake.

Pia, makundi ya kigaidi yanadai kuwa kujiunga na nchi kunapingana na kujiunga na dini wakidhani kuwa mwanadamu anatakiwa awe na uraia wa upande mmoja ama dini au nchi na kwamba kanuni na sheria za zama ya kisasa zinapingana na sheria ya kiislamu, hivyo mwislamu anapaswa kujiunga na makundi yao ambayo yanaiwakilisha dini yenye malengo ya kutekeleza sheria ya kiislamu.

Wenye fikra kali wakavuka mipaka yote walipotoa madai ya kwamba kuipenda nchi ni aina mojawapo aina za ushirikina, ambapo walidhani kuwa kuipenda nchi humfanya mwislamu akose unyenyekevu na utiifu wake kwa dini na sheria yake na kumgeuza kutoka imani kwenda ushirikina.

Kwa namna hii, viongozi wa makundi ya kigaidi wakaweza kuwakinaisha na kushawishi wengi wa wafuasi wao kuwa uraia unaokubalika katika dini ni ule wa kumwongoza mtu akataa kujiunga na nchi isipokuwa nchi yao wenyewe na asitangaze upendo wake kwa nchi yake kwa madai ya kwamba dhana ya nchi kwa mtazamo wao si nchi anapoishi mtu, bali ni maeneo yanayodhibitiwa nao na sehemu wanayoyatawala kinyume na sheria.

Jambo la kusikitisha sana ni kuona vijana wengi ambao walikuwa wanatakiwa kujenga nchi zao na kuchangia juhudi za kuhakikisha maendeleo ya nchi zao, badala ya hayo wakawa ndio mstari wa kwanza katika wanamgambo wa kuziharibu nchi hizo.

Kwa bahati mbaya, vijana wengi wamechanganyika kimawazo kuhusiana suala la kuipenda nchi na kujiunga nayo, jambo lililosababisha matatizo mengi na ufisadi mkubwa katika nchi kadhaa duniani kwa mikono ya vijana wake ambao wanatakiwa kuwa chanzo cha kujenga na kuendeleza siyo silaha ya kuharibu na kuteketeza nchi.

Kwa hakika mwislamu anapaswa kuipenda nchi yake na kuisaidia iwe nchi ya kuongoza nyinginezo katika pande mbalimbali za maisha akitambua umuhimu wa kutekeleza majukumu yake kwa nchi alipozaliwa na kukua. Vile vile, sheria ya kiislamu imewahimiza waislamu wawajibikie upendo na undugu pamoja na wenzao katika jamii na kukamilishana na wanadamu wote kwa lengo la kuisukuma jamii na kuikuza.

Majibu ya madai ya magaidi kuhusu dhana ya "Uraia":

Uraia kwa dhana yake pana ni kuthibitisha uhusiano na kufungamana baina ya mtu na nchi yake, pamoja na kuthibitisha uhusiano huo, uraia unathibitisha haki na wajibu zilizopo katika katiba ya nchi, pia uraia unajumuisha masharti na vidhibiti vya kuishi katika jamii husika kama vile; kuheshimu kanuni na katiba, kuchunga haki za wengine bila ya kujali dini, rangi, kabila au lolote la kutofautisha baina ya mmoja na mwingine katika jamii moja.

Kwa hakika, Uislamu tangu siku ya kwanza ya kuanzisha jamii ya kiislamu umesisitiza umuhimu wa kuishi pamoja na wasio waislamu kwa kuzingatia matendeano mazuri, mpaka wengi wa wafuasi wa dini hizo wameshuhudia kwamba hawakupata neema ya usalama, utulivu, na amani isipokuwa pamoja na waislamu.

Na kwamba kuwepo baadhi ya hitilafu kati ya wanadamu, hata hitilafu hizo zikiwa za kidini, basi hazizuie kusaidiana katika mambo mengi ya pamoja, bali ni lazima wanadamu wote wasaidiane na kukamilishana kwa ajili ya kupata furaha na manufaa kwa wote.

Vile vile, Uislamu unapambanua baina ya wanaopigana vita na wasiopigana, Mwenyezi Mungu (S.W.) Amesema: )Asaa Mwenyezi Mungu akatia mapenzi baina yenu na hao maadui zenu, na Mwenyezi Mungu ni Mweza, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu(7). Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu(8). Hakika Mwenyezi Mungu anakukatazeni kufanya urafiki na wale walio kupigeni vita, na wakakutoeni makwenu, na wakasaidia katika kufukuzwa kwenu. Na wanao wafanya hao marafiki basi hao ndio madhaalimu).(9(,{Al-Mumtahanah:7-9}.

 

Inakumbukwa kuwa Al_Azhar Al-Shareif imechukua hatua kadhaa katika kusisitiza dharura wa kuimarisha kuishi pamoja baina ya wanadamu wote bila ya kumbagua yeyote kwa msingi wa rangi au dini au kabila au chochote chengine. Miongoni mwa hatua zilizochukuliwa kwa lengo la kuhakikisha na kueneza fikra hiyo, mkutano uliofanyika nchini Misri kwa kushirikiana kwa taasisi, mashirika, wakuu wa dini mbalimbali duniani na washiriki wengine wengi wanaoshughulikia masuala ya kueneza amani na kupambana na mizozo na migombano.

Washiriki wa mkutano huo wameafikiana kutoa tangazo liitwalo "Tangazo la Al-Azhar la Kuishi pamoja kwa Amani" ambalo limekusanya matokeo ya mijadala na mazungumzo mengi yaliyofanywa na walioshiriki kwenye kongamano lile, tungependa kutoa mwangaza baadhi ya yaliyokuja katika tangazo hilo kupitia mistari michache yafuatayo:

Kwanza:     

Istilahi ya “Uraia" ni istilahi thabiti katika Uislamu, katika katiba iliyowekwa na Mtume (S.A.W) inayoitwa “Katiba ya Madinah”, mikataba na ahadi za Mtume zilizohusiana na kuainisha uhusiano baina ya waislamu na wasio waislamu. Na tangazo hilo lina hamu ya kusisitiza kwamba uwananchi sio ufumbuzi ulioagizwa kutoka kwenye nchi za kigeni, bali ni kukumbuka mfumo wa utawala uliopitishwa na Mtume (S.A.W) katika jamii ya kiislamu ya kwanza kabisa alyeianzisha Mtume ambayo ni nchi ya Madinah.

Jambo lisilojumuisha kadri yoyote kutoka katika ubaguzi au kudharau kundi lolote miongoni mwa makundi ya jamii wakati huo, bali imekusanya siasa za kukiri kuwepo dini, ukoo na jamii mbalimbali, kutofautiana huko hakufai kuwepo isipokuwa ndani ya wigo wa uwananchi kamili na usawa ambayo zilitajwa katika “Katiba ya Madinah” kutangaza kuwa “Makundi tofauti ya kijamii kidini, ukoo ndio Umma mmoja, na kwamba wasio waislamu wana haki sawa sawa na waislamu, na wana wajibu sawa sawa na waislamu, maana wanaishi katika nchi moja".

Pili:

Kwa Hakika kukiri dhana ya uraia, usawa na haki kunawajibika kulaani vitendo vinavyopigana na msingi wa uraia, na kulaani vitendo visivyokubaliwa na sheria ya kiislamu, ambavyo vinatokana na msingi wa kupambanua baina ya mwislamu na asiye mwislamu, jambo linalopelekea kuzuka udharau, kutojali, na kudhulumu, licha ya kufanya mauaji na kuwahamisha wachache kutoka kwa makazi yao kwa dai la kwamba wanafuata dini tofauti jambo lisilokubalika na Uislamu wala dini yoyote nyingine.

Pia, la kwanza miongoni mwa vitendakazi vya kuimarisha utashi wa pamoja linadhihiri katika nchi inayozingatia uwananchi unaotegemea katiba yenye kuyatunza maadili ya uwananchi, usawa na kuhukumiwa na kanuni, kwa hivyo tunasema kwamba kuiweka mbali dhana ya uwananchi inapelekea nchi, taasisi za kidini wenye utamaduni na wanasiasa kufeli, na kuathiria vibaya maendeleo, na inawapa wafisadi nafasi ya kuharibu nchi, utulivu wake, hatima yake na mapato yake.

Tatu:

Kwa mujibu wa yaliyodhihiri katika miongo iliyopita hasa vitendo vya ukatili, uhalifu na ugaidi vinavyofanywa na wanaojinasibisha na dini, na kwa mujibu wa vitendo vinavyowalengea wafuasi wa dini na tamaduni nyinginezo katika jamii yetu kama vile kuhamisha, kuhofisha, kuteka nyara, washiriki wa mkutano wa Al-Azhar wamekubaliana kutangaza kuwa dini zote ziko mbali na ugaidi kwa aina zake zote, wakiulaani ugaidi sana.

Na wanawataka wanaotuhumu Uislamu au dini yoyote nyingine kwa kuhusiana na ugaidi, kutotoa tuhuma hizo kabisa, kwani kuzipachika tuhuma hizo kwa dini kumewafanya watu wengi hasa wa kawaida (wasio na elimu) kuzoea kuzifungamanisha dini na ugaidi wakiwazingatia wafuasi wa dini ndio magaidi.

Nne:

Hakika kulinda maisha ya wananchi, uhuru zao, heshima yao na ubinadamu wao na haki zao zote ndiyo wajibu wa kwanza kwa nchi ambayo haifai kupuuzwa, kwa ajili ya kulinda maisha ya wananchi na haki zao, pia haifai katika hali zote kuzizuia nchi kutekeleza wajibu hiyo.

Kwa hakika wafuasi wa dini zote wana majukumu ya pamoja kwa mujibu wa kujinasabisha kwa uraia mmoja na hatima moja, majukumu hayo yanatubidi kushikamana na kusaidiana kwa ajili ya kulinda uwepo wetu kwa upande wa kisiasa na kijamii kwani maslahi zetu ni moja na dhuluma ni moja, jambo linalotulazimisha kuzidisha juhudi za pamoja na kuzigeuza hisia hizo nzuri kwa kazi ya kikweli katika nyanja zote za maisha, kijamii, kitamaduni na kitaifa.

Tano:

Hakika Al-Azhar kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za kidini na zisizo za kidini kama vile; Vatican na Baraza la Wakuu wa Waislamu na taasisi nyinginezo kunafanya juhudi kubwa za kudumisha maelewano na kusisitiza umuhimu wa kufahamiana baina ya pande zote kwa lengo la kuhakikisha na kutimiza maadili ya uwananchi, usawa na uhuru.

Miongoni mwa juhudi zinazoendelea kuunda tume ya pamoja ya undugu wa kibinadamu na kupitisha "Waraka wa Undugu wa kibinadamu" unaolenga kutangaza maadili ya kuishi pamoja kwa amani baina ya wanadamu wote kwa mujibu wa misingi ya kisheria. Kwa hakika tunaweza kusema kwamba "Waraka wa Undugu wa kibinadamu" ni katiba mpya ya kuishi pamoja kwa amani baina ya waislamu na wasio waislamu, hivyo ni nakala ya kisasa ya "Mkataba wa Al-Madinah" ambapo mikataba yote miwili ina malengo hayo hayo japokuwa mazingira iko tofauti.

Hakika Mtume (S.A.W) Ametoa mfano wa kushirikiana kamili na mkataba ulioandikwa baina ya kundi moja la watu waliopanda meli moja yenye ghorofa mbili, basi watu waliochukua ghorofa ya chini walipotaka kujaza maji walikuwa wanapitia walio ghorofa ya juu, basi baadhi yao wakasema "tungefanya utundu katika ghorofa yetu ili tusiwaudhi walio juu?" Mtume (S.A.W) Akasema kuhusu tukio hilo "watu wa ghorofa ya juu wakiwaacha kutekeleza wanayoyataka, wote wataangamizwa, ama wakiwazuia wote wataokoka".

Kwa mtazamo huo wa kwamba sote tuko kwenye meli moja tungesaidiana na kupendana tungefanikiwa sote, ama tungegombana na kuvutana tungefeli na kuangamizwa. Pia, kwa ajili ya kutekeleza mahitaji na masharti ya uraia tunatakiwa kuwaelimisha watoto na ndugu zetu wawe na hisia za undugu, upendo, unyenyekevu na usamehevu na kutendeana na wanadamu wote kwa mujibu wa misingi ya pamoja inayowajumuisha watu wote katika ulimwengu huu.

Kwa ufupi, uraia ni dhana inayotumiwa kuashiria uhusiano unaotakiwa kuwepo baina ya watu wanaoishi katika nchi moja, dhana inayoashiria namna ya kufungamanisha wanaoishi katika jamii moja. Ule uhusiano unatakiwa kuwa na misingi ya kusaidiana na kushirikiana kwa ajili ya kujenga nchi na kuendeleza jamii.

 

 

 

 

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.