Kuua katika miezi mitakatifu ni haramu, huenda kinyume cha sheria ya Kiislamu

  • | Monday, 28 February, 2022
Kuua katika miezi mitakatifu ni haramu, huenda kinyume cha sheria ya Kiislamu

 

     Miezi  mitakatifu ni miezi ambayo Mwenyezi Mungu Mtukufu Ameharamisha kupigana, nayo ni miezi minne, Muharram, Rajab,  Dhul-Qa'dah, na Dhul-Hijjah, ambapo Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema; (Hakika idadi ya miezi kwa Mwenyezi Mungu ni miezi kumi na mbili katika hukumu ya Mwenyezi  Mungu tangu alipo umba mbingu na ardhi. Katika hiyo iko minne mitakatifu. ), “Surat Al-Tawbah (36)” .

    Miezi minne hiyo ilikuwa na umuhimu mkubwa na heshima kwa Waarabu  kabla ya Uislamu. na miezi hii Ilikuwa ni haramu kufanya dhambi lolote kutoka madhambi makubwa.  Uislamu ulipokuja, uliamuru kutopigana, isipokuwa katika hali ya kujibu uchokozi wowote.

Sifa za miezi mitakatifu:-

     Ina sifa kubwa, kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu huzidisha malipo na jaza  kwa waja wake, na pia huzidisha dhambi na hatia, kutokana na ukubwa na wema wake.

      Mwenyezi Mungu mtukufu, Alizuia kupigana  katika miezi hiyo, ambapo alisema; (Wanakuuliza juu ya kupigana vita katika mwezi mtakatifu. Sema: Kupigana vita wakati huo ni dhambi kubwa. Lakini kuzuilia watu wasiende katika Njia ya Mwenyezi Mungu na kumkanusha Yeye, na kuzuilia watu wasiende kwenye Msikiti Mtakatifu na kuwatoa watu wake humo, ni makubwa zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu.) “AL – BAQARA (217)”.

      Mwenyezi Mungu Mtukufu  Amesisitiza uharamu wa dhulma katika miezi mitakatifu, na Mwenyezi Mungu Mtakatifu Amesema: (Msijidhulumu nafsi zenu humo)“Surat Al-Tawbah (36)”.

Makundi ya kigaidi

     Kwa hakika, kuwalenga wasio na hatia katika miezi mitakatifu ni jambo  muhimu mno. jambo hilo linathibitisha ubatili wa itikadi za magaidi , na kufichua uwongo wa madai wao kwamba ni waislamu.

     kituo cha Al_Azhar cha kupambana na fikra kali daima huthibitisha   uwongo wa magaidi. Ushahidi mkubwa wa hilo ni kuwauwa watu  katika miezi mitakatifu, na kwamba vitendo vyote vinavyofanywa na magaidi hawa vinapingana na mafundisho ya Uislamu, na vinapingana na malengo yake, ambalo la kwanza kabisa ni kujihifadhi nafsi ya binadamu.

     Al_Azhar pia inaamini kwamba, wanavyofanya magaidi hawa ni kuondoka dhahiri katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu na mafundisho ya dini zote, na Al_Azhar inasisitiza uungaji mkono wake kwa watu wote wa Kiafrika na wa kiulimwengu ili kukabiliana na ugaidi.

    Pia, Al_Azhar inatumai kuwa jinai hizi zitaongeza tu muungano na azma ya watu wa Kiafrika kukabiliana na ugaidi hadi  utakapong'olewa, na kuomba Mwenyezi Mungu Aipushe Afrika na watu wake kutoka kwa magenge ya mauaji, hujuma na ugaidi weusi.

     Kwa hivyo basi, hapa kwenye Kituo cha Al_Azhar cha kupambana na fikra kali, tunatoa wito kwa umati wa Waislamu wa mashariki na magharibi mwa ardhi,  kuiheshimu miezi hii mitakatifu. Wala wasifanye mabaya humo.

     Pia, Tunatumia fursa hii kuyaambia makundi yenye silaha na mashirika yanayodai Uislamu,: “Acheni kupigana na wasio na hatia katika miezi mitakatifu, ikiwa nyinyi ni Waislamu kweli”.

     Vile vile, hapa katika kituo cha  Al_Azhar tunatuma ujumbe kwa Waafrika wote: “Msidanganyike na sura za kupendeza zinazoonyeshwa na wale wanaodai kuwa wanadini.” Si Mwislamu anayeua, kudhulumu, kuiba na kupora .

     Enyi waja wa Mwenyezi Mungu, inatubidi kufanya mengi mema ambayo Mwenyezi Mungu na Mtume wake Muhammad (rehema na amani zimshukie) walituamrisha katika miezi hii mitakatifu. pia,  tuepushe na uovu na dhulma na vitendo vyote vinavyokatazwa na Mwenyezi Mungu na Mtume wake .

     Mwishoni:  Tunamuomba Mungu atusaidie sote katika ibada yake njema, atujaalie mwisho mwema, atuepushe na maovu, na atuponye na mabaya yote. Ewe Mwingi wa  rehema mwenye kurehemu.

 

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.