Mwenendo wa Imamu katika kuimarisha amani duniani

  • | Sunday, 25 September, 2022
Mwenendo wa Imamu katika kuimarisha amani duniani

     Hapana shaka kwamba juhudi za Imamu Mkuu Prof. Ahmed Al-Tayyib, Sheikh wa Al_Azhar Al-Sharif, katika kuimarisha maadili na kuweka misingi ya amani katika sehemu mbalimbali za dunia, hasa katika bara la Afrika, ambapo imamu hivi karibuni alifanya mkutano wa "Kongamano la Uadilifu na Amani kwa Afrika Yote na Madagaskar" Mheshimiwa Imam mkuu aliwakaribisha wajumbe wa kongamano hilo kwenye mkao wa Sheikh wa Al_Azhar, na akaeleza shukurani zake kwa juhudi za "Kongamano la Uadilifu na Amani kwa Afrika Yote" katika kueneza amani na udugu baina ya wananchi wa Bara la Afrika, na kutoa wito wa kuishi pamoja na mazungumzo kati ya watu wote wa dini na tamaduni mbalimbali.
Mheshimiwa Imam mkuu ameongeza kwamba, watu wa Afrika wana uwezo wa kufanya ufufuo wa bara lao na kulijaalia tajiri, ingawa kuwepo changamoto na matatizo mengi yanayolikabili bara hilo la Afrika, akieleza kwamba Al_Azhar Al-Sharif iko tayari kutoa msaada kwa juhudi zote zinazolenga kupata maendeleo endelevu na kuondoa vikwazo vikuu vitatu ambavyo bara la Afrika linakabiliwa ambavyo ni ujinga, umaskini na maradhi.
Ama kuhusu matukio ambayo ulimwengu unayashuhudia wakati hivi sasa, basi tunaweza kusema kwamba vita havina chochote isipokuwa damu na uharibifu. Hili ndilo somo jipya ambalo ubinadamu unajifunza kutokana na vita vinavyoendelea leo huko Ulaya baina ya Urusi na Ukraine.
Baada ya kushindwa juhudi za mapatano, na vita vimeanza, wakati hii ulimwengu ulianza kutambua pigo hili jipya lililozipiga juhudi zote za kuleta amani katika uwanja wote. Hapana shaka kwamba wajibu wa viongozi ni mkubwa katika suala hili. kwani wao wamebebwa jukumu la kufanyakazi kwa harakati zisizo na kikomo za kumaliza vita hivi haraka iwezekanavyo; kwa ajili ya kuzuia umwagaji wa damu na kuziokoa roho.
Ama viongozi wa dini ndio wanaohisi uchungu wa vita hivi zaidi. Hao ndio watetezi wa amani na wabeba mwenge wa udugu wa binadamu hapa duniani, jukumu ambalo wamejibeba kwa kuzingatia wajibu wao wa kidini wa kuwaongoza watu kwa yale ambayo yupo ndani yake manufaa yao.
Tangu ashike wadhifa huu, Mheshimiwa Imamu Mkuu wa Al_Azhar, Profesa Dk. Ahmed Al-Tayyib, amekuwa akifanya kila alichoweza na asichoweza ili kueneza kanuni za amani na udugu baina ya wanadamu, hasa kupitia mipango yake aliyoyafanya, na misimamo madhubuti aliyoichukua kuhusu masuala mengi ya kibinadamu, akikataa dhuluma zote zilizotukia na wanadamu, bila kujali lugha yao, kabila, dini au rangi. Kuhusiana na suala la Palestina, kwa mfano, Mheshimiwa Imamu Mkuu alikuwa na misimamo mingi inayounga mkono suala hili na inayozungumzia dhamiri ya walimwengu, akijaribu kuiamsha ili iunge mkono na kusimama pamoja na wananchi wa Palestina wanaovumilia. Mheshimiwa Imamu Mkuu akazingatia suala hili "mama wa maswala ya Mashariki ya Kati", akisema kwamba "nchi nyingi za ulimwengu zimepata uhuru wake  isipokuwa Palestina, na tunaamini kwamba ikiwa suala hili halitatatuliwa kwa suluhisho la uadilifu, basi ulimwengu hautastarehe wala hautaona amani, kwa sababu suala hili ni suala la ukweli na haki". 
Misimamo ya Mheshimiwa Imamu Mkuu ilikuwa wazi kuhusiana na masuala mengine, likiwemo suala la Iraq. Msimamo wa Imamu Mkuu kuhusu suala hili ulikuwa maarufu sana katika kupiga kura ya Kurdistan mwaka 2017, pale ambapo serikali ya Iraq ilipotangaza kuwakaribisha kwa msimamo wa Al_Azhar Al-Sharif wa kukataa kura ya maoni ya "eneo la Kurdistan la Iraq" na matakwa yake ya kuhifadhi umoja wa Iraq na kukataa wito wa kugawanyika. Hii ni pamoja na mshikamano wa Al_Azhar na Iraq ndugu wetu kwa uongozi, serikali, na watu wake, kuhusu kupambana na ugaidi wa kikatili uliomwaga damu ya watu wasio na hatia katika mashambulizi mengi ya kigaidi.
 Al_Azhar ilifanya juhudi chini ya usimamizi wa mheshimiwa Imamu Mkuu kutatua suala la Waislamu wa Rohinga, na mheshimiwa Imamu Mkuu alipokea katika mkao mkuu wa Sheikh wa Al_Azhar ujumbe wa Waislamu wa Rohinga. Kisha Al_Azhar imepeleka misafara ya misaada ya kibinadamu kwa Myanmar, pamoja na kuzungumzia suala hilo katika mikutano mingi ya kimataifa. Kupitia hotuba yake katika Mkutano wa Kimataifa wa Amani mjini Berlin mwaka 2017, mheshimiwa Imamu Mkuu alikosoa msimamo wa jumuiya ya kimataifa kuhusu mauaji na mateso ya Waislamu wa Rohinga akisema: Jumuiya ya kimataifa imeyapa kisogo mayowe na machozi ya watoto na wanawake. Chini ya hali ya sasa, na kuzuka kwa vita. 
Imamu Mkuu alitoa taarifa rasmi kupitia akaunti yake ya Twitter, akitoa maoni yake juu ya vita hivi vikali kati ya Urusi na Ukraine, akitoa wito wa kusitishwa vita kwa haraka, na kurejea kwa mazungumzo kama ni suluhisho pekee lisiloweza kubadilishwa ufumbuzi. Mheshimiwa Imamu Mkuu alisema: "Vita havitaleta kwa ulimwengu wetu ila uharibifu na chuki, na haiwezekani kutatua migogoro ila kwa mazungumzo, naitakia Urusi na Ukraine kuhukumiwa kwa sauti ya akili, na nawatakia viongozi wa nchi kuunga mkono suluhisho za kiamani kwa kumaliza migogoro baina  ya jirani mbili". 
Imamu Mkuu wa Al_Azhar pia aliandika katika ukurasa wake rasmi wa Facebook, akisema: "Mimi na walio na rika langu, tumeshuhudia ukatili wa vita na uchungu wa migogoro, na tumeona athari zake mbaya; kama kuporomoka kwa uchumi, kupoteza kwa rasilimali, kuenea kwa umaskini, kutojua kusoma na kuandika, maradhi na chuki" pia akasema akiwahutubia viongozi wa dunia: "fanyeni kila mnavyoweza kwa ajili ya kuzima moto wa vita, muungane na muunganishe juhudi zenu kuwaokoa wanyonge na wasio na makazi., kwani historia itawakumbusheni kwa mlivyoweza kuitekeleza kwa wananchi wenu na ubinadamu kama utulivu, uadilifu na amani.
Juhudi hizi za Mheshimiwa Imamu Mkuu zilikuwa ni hatua muhimu katika kuweka maadili na dhana nyingi zinazohusiana na mazungumzo na amani, hasa kwamba zilihitimishwa kwa Hati ya Udugu wa Kibinadamu, ambayo inazingatiwa kwa shahada ya viongozi wengi, raisi, wanafikra, na wanaosuluhisha, ni katiba mpya ya amani ya dunia na udugu wa binadamu. 
Kituo cha Uangalizi cha Al_Azhar cha Kupambana na Fikra kali kinaamini kwamba jukumu hili ndilo linalotarajiwa kutoka kwa Imamu mkuu katika hali hii ngumu ya kimataifa, ambayo ni kwamba kutafuta amani na mazungumzo ndiyo suluhisho pekee linalopendekezwa kumaliza mgogoro huo, na sisi tuna imani kamili kwa imani ya Imamu Mkuu kwa jambo hilo, imani ya kina inayotokana na jukumu kweli, na hamu kweli katika kusimamisha misingi ya udugu, amani na haki duniani kote.
Kituo cha Uangalizi pia kinasisitiza umuhimu wa mazungumzo na matumizi ya akili, ili kuepusha umwagaji wa damu ya wasio na hatia, na kukomesha hali ya uharibifu inayoipiga Ukraine, ambayo watu wake sasa wanalipa bei kubwa isiyoweza kuvumiliwa.

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.