Ili kupanuka utawala wake ... Daesh yaua magaidi 80 wa Al-Qaeda kati ya Mali na Burkina Faso

  • | Wednesday, 30 November, 2022
Ili kupanuka utawala wake ... Daesh yaua magaidi 80 wa Al-Qaeda kati ya Mali na Burkina Faso

Kuna matukio kadha wa kadha yanayoshuhudiwa na eneo la kigaidi barani Afrika, baadhi ya matukio hayo yanahusiana na Daesh, mengine yanahusu Al-Qaeda pekee, na baadhi yake yanahusu makundi yote mawili, na miongoni mwa maeneo muhimu yaliyoshuhudia matukio hayo ni eneo la Sahel (hasa Burkina Faso, Mali, na Niger), basi eneo hilo limekumbwa na ongezeko kubwa la shughuli za makundi ya kigaidi; ambapo eneo hilo likikumbwa na takriban mashambulizi 800 ya kigaidi mwaka wa 2019 AD, na idadi ya vifo vilivyotokana na operesheni hizi za kigaidi ilikadiriwa kuwa takriban watu 2,600, nayo inawakilisha maradufu ya vifo vya 2018 AD.

Mashambulizi haya yanahusishwa na makundi makuu matatu: kundi la "Ansar Al-Islam", kundi la "Nusrat Al-Islam Walmuslimin", na "Daesh tawi la Sahara Kubwa". Hata hivyo, hivi karibuni mashambulizi hayo yamejikita kwenye sehemu ya mashariki ya Mali hadi Burkina Faso, ambayo imekumbwa na ongezeko la kasi la operesheni za kigaidi katika miaka ya hivi karibuni. Idadi ya vifo iliongezeka kutoka 80 mwaka 2016 hadi zaidi ya 1,800 mwaka 2019.

  • Daeish na matamanio ya kutandika tena kwenye pwani ya Afrika

Daesh ilijitahidi kutafuta maeneo mapya ya ushawishi na ya mbadala baada ya kupoteza ngome zake kuu huko Syria na Iraq, kwa hivyo mtazamo wake wa kwanza wa kimkakati ulijikita katika bara la Afrika, kutokana na asili yake ya ardhi ionyeshayo milima na mabonde ambayo inaweza kuisaidia kujiweka na kuchukua mapango mapya na vituo vya uongozi, pamoja na udhaifu wa baadhi ya vituo vya mpakani baina ya nchi, licha ya hali ya kisiasa na kuenea kwa uhalifu katika baadhi ya nchi, jambo ambalo linafanya kuwa mawindo rahisi ya ugaidi na fikra kali. Na eneo la Sahel na Sahara lilikuwa chaguo zuri kwa kundi lijiweke upya, na hivyo kwa sababu ya udhaifu wa mshiko wa usalama huko, na kutoroka kutoka kwa nguvu ya kundi la Shabaab kama kundi lenye mshikamano ambalo Daesh labda lashindwa vita vyake mbele ya Al-shabab, haswa katika wakati huu, na pia kutoroka kutoka kwa jeshi la Nigeria na vikosi vya muungano wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Ziwa Chad na pembetatu ya mpaka, ingawa udhibiti wa kundi hilo maeneo hauko baada ya kudhoofika kwa kundi la Boko Haram, na kujisalimika idadi kubwa ya wafuasi wake, ama kwa jeshi la Nigeria au kwa Daesh. Eneo hilo pia linazingatiwa kuwa ni lango la udhibiti wa kivuko cha ghuba ya Guinea ya mpaka, ambacho ni kivuko cha kibiashara ambacho hurahisisha unyonyaji wa kundi hilo wa magendo na usaidizi wa vifaa kwa kundi hilo.

Wapiganaji wa kundi hilo nchini Niger, Nigeria, Burkina Faso na Mali walipanga mfululizo wa operesheni za kigaidi kwa shabaha za kijeshi na raia, kufuatia kundi hilo kuzindua kile ilichokiita (vita vya kulipiza kisasi la Abu Bakr al-Baghdadi na Abu al-Hasan al- Muhajir). Afrika na eneo la Sahel ya Afrika pia ni miongoni mwa vichwa vya habari vya gazeti la Al-Naba', linalochapishwa na Daesh.

Kwa sababu hii, Daesh inajitahidi kuweka nguvu na udhibiti juu ya eneo hilo na kushirikiana na kundi lingine lolote, liwe lina uhusiano na Al-Qaeda au la, mradi haliungi mkono nalo au kulifuata.

Hivi karibuni, kwa mujibu wa tovuti ya (Akhbar Al-Aan), Daeish katika Mkoa wa Sahel ilidai kuwa ilipambana na wanachama wa kundi la kigaidi la Al-Qaeda katika maeneo kati ya Mali na Burkina Faso. Kwa mujibu wa taarifa ya Daeish, takriban wanachama 80 wa kundi la kigaidi la al-Qaeda waliuawa na makumi wengineo walijeruhiwa, na magaidi wa Daesh waliwakamata wengine 10 na kuwaua katika makabiliano hayo. Daesh imeongeza katika taarifa yake kwamba wapiganaji wake walichoma gari na kukamata magari mengine 6, pamoja na kiasi kikubwa cha risasi na silaha.

Na kwa upande wake Kituo cha Uangalizi cha Al-Azhar cha Kupambana na Fikra Kali katika habari, ripoti na makala nyingi kimetahadharisha matamanio ya makundi ya Daesh na Al-Qaeda katika kudhibiti na kueneza upya katika bara la Afrika, hasa eneo la Sahel ya Afrika. Pia Kituo cha Al-Azhar kinatazama kwa mzozo unaoendelea kati ya makundi hayo mawili kwa mtazamo wa kuwa ni jambo zuri ambalo serikali na majeshi ya nchi za Kiafrika yanapaswa kuchukua fursa hiyo, kwani mizozo kati ya makundi hayo inayadhoofisha na kumaliza nguvu zake.

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
5.0

Please login or register to post comments.