Al-Azhar yalaani vikali kuendelea kudhuru Qur’an huko Uswidi: aibu kwenye paji la uso la Uswidi

  • | Monday, 24 July, 2023
Al-Azhar yalaani vikali kuendelea kudhuru Qur’an huko Uswidi: aibu kwenye paji la uso la Uswidi

     Al_Azhar: Uswidi imethibitisha kwa vitendo vyake kwamba ndiyo jamii iliyo karibu zaidi na ubaguzi na iliyo mbali zaidi na kuheshimu dini na watu.
Al_Azhar yatoa wito kwa watu wote walio huru duniani kuendelea kususia bidhaa za Uswidi ili kuunga mkono Qur’an, kitabu cha  Mwenyezi Mungu. 
Al_Azhar yatoa wito kwa nchi za Kiarabu na Kiislamu kuendelea kuchukua misimamo thabiti kuhusu siasa za Uswidi dhidi ya Uislamu.
Al-Azhar Al-Sharif inaelezea kulaani kwake vitendo vya uchochezi  vinavyofanywa mara kwa mara na serikali ya Uswidi dhidi ya matakatifu yetu ya Kiislamu chini ya kauli mbiu ya uwongo ya "uhuru wa kujieleza", ikisisitiza kwamba kile ambacho serikali ya Uswidi inafanya ili kuendelea kutoa idhini za kuchoma Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu kinaonyesha siasa za machafuko, fikra kali yenye chuki, kuunga mkono ugaidi, na kuonyesha uadui dhidi ya Waislamu duniani kote.
Al-Azhar inatia mkazo kwamba kuwaruhusu magaidi hao wahalifu kuichoma Qur’an kunawakilisha jinai dhidi ya Uislamu, haki ya dini na ubinadamu, na aibu kwenye vipaji vya jamii hizi, ambazo zimethibitisha kupitia vitendo vyao kwamba wao ndio watu walio karibu zaidi na ubaguzi wa rangi, machafuko na misimamo miwili, na wao ndio mbali zaidi na uhuru wa kweli na kuheshimu kwa dini na watu.
Al-Azhar inatoa wito kwa watu wote wa Kiarabu na wa Kiislamu kuendelea kususia bidhaa zote za Uswidi ili kumnusuru Mwenyezi Mungu na Kitabu Chake Kitukufu, na wajibu juu ya watu wote walio huru duniani kujiunga na wito huu, na inathibitisha kwamba ulegevu wo wote katika kuchukua misimamo thabiti dhidi ya kile ambacho Uswidi inakizalisha ni kuunga mkono uhalifu huu, na kuwatia moyo wale wahalifu wanaoonyesha uadui wao kwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu na dini ya Kiislamu ili kuendelea katika uhalifu wao, na kuunga mkono jamii hizi ambazo hazijui isipokuwa pesa kama ni mbinu na lengo.
Al-Azhar, ikitoa wito kwa watu wa Kiarabu na wa Kiislamu kuendelea kususia bidhaa za Uswidi; pia inatoa wito kwa nchi zote za Kiislamu na Kiarabu kuendelea kuchukua misimamo ya umoja na makini dhidi ya siasa za Uswidi zenye kishenzi na chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu ambazo haziheshimu matakatifu ya dini, na hazielewi ila lugha ya fedha na maslahi ya kimaada tu.

Print
Categories: Habari
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.