Kiashirio cha operesheni za kigaidi kwenye nchi za Kiafrika kwa Mwezi wa Juni 2023

  • | Saturday, 8 July, 2023
Kiashirio cha operesheni za kigaidi kwenye nchi za Kiafrika kwa Mwezi wa Juni 2023


     Mwezi wa Juni 2023AD ulishuhudia ongezeko wazi katika kiwango cha operesheni za kigaidi zilizofanywa na makundi yenye fikra kali barani Afrika kikilinganishwa na mwezi wa Mei uliopita kwa kiwango cha 20%; Ambapo mwezi huu ulirekodi operesheni (36) za kigaidi ambazo zilitofautiana kati ya mabomu na mauaji, na ongezeko hilo lilisababisha kuongezeka kubwa kwa idadi ya wahanga, na waliojeruhiwa na waliotekwa nyara wakati wa mwezi huu; Ambapo operesheni zilisababisha vifo vya watu (295), na (114) walijeruhiwa, na (70) walitekwa nyara. Wakati idadi ya operesheni mnamo Mei ulifikia operesheni (30) za kigaidi, zilisababisha vifo vya watu (268), (33) walijeruhiwa, na kutekwa nyara kwa (33) wengine.
Kwa mujibu wa takwimu, eneo la Afrika ya Mashariki lilishika nafasi ya kwanza kulingana na idadi ya operesheni zilizosababisha kuwepo kwa wahanga na waliojeruhiwa; Ambapo eneo la msukosuko lilishuhudia mashambulio (14) ya kigaidi, ambayo ni sawa na (38.9 % ya jumla ya operesheni za kigaidi), yalisababisha vifo vya watu (122), (101) walijeruhiwa na (30) wengine walitekwa nyara. Somalia peke yake ilipatwa na operesheni (8)zilizosababisha vifo vya watu (58), waliojeruhiwa (97), na (30) walitekwa nyara. Ama kuhusu "Kenya" ilipatwa na operesheni (4) ambazo zilisababisha kifo cha (23) na (4) waliojeruhiwa. "Uganda" pia ilishuhudia operesheni moja ambayo iliwaua watu (41) bila ya kuwepo kwa waliojeruhiwa, wakati "Ethiopia" ilipatwa na operesheni moja, lakini haikufanikiwa, na haikusababisha vifo au majeraha.
Kituo cha Uangalizi cha Al-Azhar cha kupambana na Fikra Kali kinaamini kwamba ugaidi katika Mashariki na Pembe la Afrika bado ni tishio kubwa kwa usalama, ingawa kufikia serikali za eneo hilo -haswa serikali za Somalia- kwenye kiwango karibu na kuondolewa kwa wanamgambo wa kundi la Al-Shabab la kigaidi. Hii inaweza kuelezewa kuwa mikakati ya serikali katika eneo la Afrika ya Mashariki ya kukabiliana na ugaidi wa Al-Shabab ilijaalia kundi la Al-Shabab la kigaidi linaongeza vitisho vyake mwezi huu.
Wakati wa mwezi, eneo la Sahel la Kiafrika, -ambalo ni chanzo cha wasiwasi- lilishika nafasi ya pili kuhusu suala la idadi ya operesheni na wahanga; Ambapo lilishuhudia mashambulizi (10) ya kigaidi, sawa na (27.8% ya jumla ya idadi ya operesheni za kigaidi zilizofanywa na makundi ya kigaidi katika bara wakati wa mwezi huo), operesheni hizi zilisababisha kuuawa (101) na kujeruhiwa (5). "Niger" ilipatwa na operesheni mpili za kigaidi, zilizosababisha kuwauwa raia (7) bila ya kuwepo majeraha yoyote. Na "Mali", ilishuhudia operesheni moja ambayo ilisababisha kifo cha (2) na kujeruhiwa (3) wengine.
Sababu ya kuongezeka kwa operesheni za kigaidi katika eneo la Sahel inarudia kwamba eneo hilo linakabiliwa na changamoto nyingi za kijamii, kiuchumi na usalama, kwa sababu ya kutokuwepo hali ya utulivu wa kisiasa, ambayo inaweza kudhoofisha hali muhimu ya kufikia viashirio vya amani katika eneo hilo, na hayo yanaliweka eneo katika mzunguko wa vurugu na udhaifu.
Ama eneo la Afrika ya Magharibi, lilishika nafasi ya tatu, ikiwa lilishambuliwa na ISIS ya Afrika ya Magharibi na magaidi wa "Boko Haram" kwa operesheni (8) za kigaidi, sawa na (22.2 % ya jumla ya operesheni za kigaidi), zote zilikuwa nchini Nigeria, na kusababisha kifo cha (59), (5) walijeruhiwa, pamoja na (40) wengine waliotekwa nyara.
Kituo cha Uangalizi kinaamini kwamba makundi ya kigaidi huko Magharibi mwa bara hilo, ingawa yanafanya mashambulio yaliyoratibiwa katika wakati nyingi, lakini yanapigana yenyewe kwa yenyewe ili kudhibiti rasilimali, jambo ambalo husababisha mamilioni ya wakazi kukimbia na kuenda maeneo mengine ili kutafuta usalama.
Kuhusu eneo la Afrika ya Kati, lilishika nafasi ya mwisho. ambapo eneo hilo lilipatwa na mashambulio (4) ya kigaidi, ambayo ni sawa na (11.1 %) ya jumla ya operesheni za kigaidi), yote yalisababisha kifo cha watu (4), bila ya kuwepo waliojeruhiwa. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ilipigwa na mashambulio mawili yaliyofanywa na "vikosi vya Kidemokrasia vya Washirika" vya ISIS, ambayo yalisababisha kifo cha (2). Cameroon ilipigwa na mashambulio mawili pia, wakati ambao (2) yaliyosababisha kifo cha raia (2).
Ama kuhusu juhudi za kupambana na makundi ya kigaidi barani Afrika, idadi ya waliouawa kutoka makundi ya kigaidi ilifikia (467), (15) walikamatwa, pamoja na kujisalimisha kwa (83). Katika eneo la Afrika ya Magharibi, juhudi za Jeshi la Nigeria katika kupambana na makundi ya "Boko Haram" na "ISIS" yalisababisha kuwaua (201) na kujisalimisha (73) kutoka magaidi.
Na katika mashariki mwa bara hilo, haswa nchini Somalia, serikali iliwaua (160) magaidi wa kundi la kigaidi la "Al-Shabab", iliwakamata (15), na magaidi (10) walijisalimisha kwa vikosi vya jeshi.
Katika eneo la Sahel, juhudi za vikosi vya usalama zilisababisha kuwaua magaidi (103) huko Burkina Faso, na (3) wengine huko Niger.
Kwa upande wake, Kituo cha Uangalizi kinaamini kwamba makundi ya kigaidi barani Afrika yanatumia fursa ya mizozo ya kikabila, na mizozo ya wachungaji na wakulima wa ardhi na mifugo, katika kuwavutia baadhi yao ili kushambulia serikali. Kwa upande mwingine, makundi haya yanaunda alama za kimkakati kwao kwenye mipaka, ili kuwezesha kutoroka kutoka serikali kwa upande mmoja, na kurahisisha operesheni za kutoa silaha, mamluki, magaidi, dawa za kulevya, pesa, na bidhaa kati ya mipaka ili kupa mkono kwa operesheni zao kwa upande mwingine. Kituo cha Uangalizi cha Al-Azhar kinatoa wito kwa nchi zinazohusika ili kutoa msaada zaidi wa usalama na ujasusi kwa nchi zinazoathiriwa na janga la ugaidi barani Afrika na kuwapa zana na mbinu za ulinda kutoka teknolojia, uangalizi na kuangalia mipaka, ili kuondoa janga hili ambalo limeenea kwa muda mrefu

Print
Categories: Infographic
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.