Imamu Mkuu ameelekeza kwamba mwanafunzi wa Guinea Mamadou Barry atunzwe

  • | Wednesday, 27 September, 2023
Imamu Mkuu ameelekeza kwamba mwanafunzi wa Guinea Mamadou Barry atunzwe

     Mheshimiwa Imamu Mkuu, Prof. Dr. Ahmed El-Tayeb, Imamu Mkuu wa Al-Azhar, alitoa maagizo yake kwa kumtunza mwanafunzi/ Mamadou Savayo Barry,aliyetoka nchini Guinea, ambaye alikuja kutoka nchi yake, akiendesha baiskeli yake ndogo, na kuvumulia shida na hatari za safari, kwa mapenzi na kujitolea kwa Al-Azhar, na kwa nia ya kutaka kupata elimu ya kidini, kutoka kwa chanzo cha ukati na kati na kinara cha sayansi.

Image

Pia, Imamu Mkuu wa Al-Azhar aliwaagiza wahusika kuchunguza uwezekano wa kumpa mwanafunzi huyo tuzo ya masomo na kumlipa posho ya kila mwezi ili kumsaidia kwa gharama zake za maisha na masomo yake, licha ya kuchukua hatua zote zinazohitajika ili kurahisisha maisha yake nchini Misri, na kumsaidia kujitolea kupata elimu na maarifa ndani ya Al-Azhar.

Print
Categories: Kujibia tuhuma
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.