Imamu Mkuu wa Al-Azhar ampokea balozi wa Misri nchini Vatican na kutuma ujumbe kwa Papa Francis

  • | Tuesday, 3 October, 2023
Imamu Mkuu wa Al-Azhar ampokea balozi wa Misri nchini Vatican na kutuma ujumbe kwa Papa Francis

     Mheshimiwa Imamu Mkuu profesa Ahmad Al-Tayyeb Shekhi wa Al-Azhar alimpokea katika makao makuu ya Al-Azhar Al-Shareif balozi Mahmoud Talaat, balozi wa Misri nchini Vatican.  
Akimkaribisha kwanye makao makuu ya Al-Azhar Al-Shareif, Mheshimiwa Imamu Mkuu alimpa balozi wa Misri nchini Vatican ujumbe wa heshima kwa kakake Papa Francis, akisema: “rafiki yangu mpendwa Papa Francis, nina upendo na heshima kwako, na namwomba Mwenyezi Mungu akupe na kudumisha neema ya afya, na ninakumbuka kwa furaha juhudi yetu ya pamoja kuhusu kuuhudumia ubinadamu, na ninataraji kukutana hivi karibuni na kukamilisha juhudi za kuimarisha #udugu_wa_kibinadamu katika kukabiliana na changamoto za kisasa. 
Kwa upande wake, balozi Mahmoud Talaat alieleza furaha yake kwa kukutana na Imamu Mkuu wa Al-Azhar, akithamini juhudi kubwa zilizofanywa na Imamu Mkuu wa Al-Azhar pamoja na Papa Francis, zilizohitimishwa na kutia saini hati ya kihistoria ya Udugu wa kibinadamu katika mwezi wa Fibruari mwaka wa 2019, na kushughulikia kwake kwa kutumia juhudi za diplomasia ya kimisri kwa ajili ya kuendeleza na kuimarisha uhusiano uliopo baina ya Al-Azhar na Vatican.
 

Print
Categories: Kujibia tuhuma
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.