Wito ya Al-Azhar Al-Shareif kwa Umma wa kiarabu na wa kiislamu

  • | Wednesday, 18 October, 2023
Wito ya Al-Azhar Al-Shareif kwa Umma wa kiarabu na wa kiislamu

     Umma wa kiarabu na wa kiislamu wanapaswa kuangalia upya tena kwa makini kuhusu faida ya kuwategemea madhalimu wamagharibi wa Ulaya – Marekani, ilhali wapalestina wanatakiwa kuwa na imani ya kwamba wale madhalimu wa kambi ya magharibi ingawa silaha na zana za kijeshi za kuwawezesha kuharibu na kuwaangamiza wanawaogopa na kuwahofia wanapokutana nao katika vita, kwani wale madhalimu wanapigania ardhi ambayo si ardhi yao, na kutetea fikra potofu isiyo na ukweli hata kidogo jambo ambalo ni la kushangaza ni kwamba mnapigana nao wakati ambapo mnashikilia uongofu wa Mwenyezi Mungu (S.W.) na mafunzo ya Mtume (S.A.W.) na kupambana na jeuri na mashambulizi yao ya kikatili, na kwa hakika hadhi ya hawa madhalimu kwenu ni sawa na sawa na hadhi ya nchi kama Somali na Afghanistan ikilinganishwa nanyi, kwa hiyo umma wa kiislamu wanatakiwa kufaidika kwa walio nao kati ya nguvu, mali, silaha na zana za kuwawezesha kuwashinda maadui wao.

Pia, Umma wa Kiarabu na wa Kiislamu wanatakiwa kuwaunga mkono ndugu zetu wa palestina kwani wanadhulumiwa sana na kuangamizwa na maadui ambao hawana huruma wala hisia za kibinadamu, maadui ambao wamepuuza ubinadamu, tabia na mafunzo yote ya Mitume na Manabii.

Enyi! Umma wa Kiarabu na wa Kiislamu mnapaswa kuwajibika kwa kauli yake Mwenyezi Mungu (S.W.): {Wala msilegee, wala msihuzunike, kwani nyinyi ndio wa juu mkiwa ni Waumini}, na mkitaka kujua ukweli wa adui wenu, basi mfikirie na tambueni kauli yake Mwenyezi Mungu (S.W.): {Kisha nyoyo zenu zikawa ngumu baada ya hayo, hata zikawa kama mawe au ngumu zaidi}

Tunamwomba Mwenyezi Mungu Awarehemu mashahidi wetu, na kuwaangamiza wale wanaofanana na wanyama pori.

Al-Azhar Al-Shareif

Print
Categories: Kujibia tuhuma
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.