Mchango wa Mwanamke katika kupambana na fikra potofu

Imeandaliwa na Dkt.; Alaa Salah Abdulwahed

  • | Wednesday, 8 November, 2023
Mchango wa Mwanamke katika kupambana na fikra potofu

    Kwa kutambua nafasi yake katika jamii, mwanamke ana mchango mkubwa katika kuhakikisha amani na utulivu wa familiya na jamii kwa jumla, kwa kuwa anaweza kuathiria familiya nzima akiwa mama, mke, dada au binti. Kwa hiyo, Uislamu hutambua umuhimu wa mwanamke kutekeleza majukumu yake katika kuwakinga jamii kutoka fikra na misimamo mikali iliyoenea zama zetu na kusababisha vijana wengi kupotea na kufuata wakatili na magaidi wenye kuharibu nchi na kuwua watu wasio na hatia hapa na kule.  

 Uislamu umekuja wakati mahusiano ya kifamiliya yakikuwa yakipuuzwa na kupotezwa kwa hiyo dini hii ikawa sababu ya kuwaokoa na kuwakomboa wanadamu kutoka hali mbaya ilivyo. Kwa kutekeleza lengo hili, Uislamu ulianza kwa familiya ambayo ni msingi wa kwanza kabisa wa jamii yoyote, ikatunga sheria zinazohusiana na familiya na zenye kuunda jamii bora. Uzingatifu huu wa Uislamu kwa familiya umegusia wanachama wote wa familiya yaani mume, mke na watoto, jambo linaloeleza umuhimu wa suala hilo kwa Uislamu kuwa uzingatifu huu unaanza hata kabla ya familiya haijaundwa, kuanzia kipindi cha kuchagua mume na mke wake ambapo uchaguzi huu huwa msingi muhimu wa kuunda familiya inayotarajiwa.

Kwa hiyo, kuchagua mke na mume ni jambo lililopewa shime na sheria ya kiislamu na kuweka vidhibiti kwa zoezi hili, kwani mume na mke ndio nguzo kuu za familiya kisha jamii. Mwenyezi Mungu (S.W.) Amesema: {Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanaofikiri} [30/21] katika tafsiri yake kwa aya hii Imamu Al-Tabariy amesema: “Maana ya aya hii ni kuwa Mwenyezi Mungu Amekujaalieni utulivu na mapenzi ya kukuunganisheni na rehma kwenu wenyewe kwa wenyewe”.

Kwa sababu ya hayo Uislamu umesisitiza umuhimu wa kuchagua mke bora kwa kuwa yeye ndiye nguzo wa msingi wa familiya yote, pia yeye ndiye anayeweza kuathiria sana kizazi kwa malezi, ambapo anatarajiwa kuwa mama mlezi anayewasaidia wana wake kuwa kizazi chema na watoto wenye tabia na maadili mazuri. Kwa kuainisha sifa muhimu za mwanamke, Mtume (S.A.W.) amebainisha kuwa sababu na vidhibiti vya kumchagua mke ni: “Mwanamke huchaguliwa kuolewa kwa kuzingatia utajiri wake ama ukoo wake ama uzuri na urembo wake ama dini yake, basi chagua yenye dini ni bora kwako”. Na katika hadithi nyingine iliyosimuliwa na Abdullah bin Omar bin Al-As (R.A.) kwamba Mtume (S.A.W.) amesema: “Dunia ni anasa na anasa bora zaidi katika dunia hii ni mke bora”. Al-Hassan alijiwa na mtu akasema: Ewe Hassan binti yangu ameombwa kuolewa na wanaume wengi, basi ni nani nimkubali awe mumewe?! Akasema: aliye mcha Mungu kwani akimpenda atamkirimu na kumtunza na akimchukia hatamfanyia dhuluma”.

Kutokana na hayo wataalamu wa malezi wanaona kuwa mchango wa mke na nafasi yake kujenga familiya ni kubwa zaidi kuliko mchngo wa mume kwa kuwa yeye ndiye huambatana na mtoto wajati wote tangu alipokuwa mimba tumboni mwake mpaka awe mtoto mchanga kisha mtoto halafu kijalunga halafu kuwa kijana na kuendelea. Mtume (S.A.W.) alipokuwa anawahotubia vijana kuwajimiza kuoa aliwaambia kuwa ndoa ni kutoka Sunna yake akikusudia kumwoa mke bora anayewajibika maamrisho na makatazo ya sheria ya kiislamu, akibinisha faida na umuhimu wa ndoa kwa kusema: “Enyi Vijana! Yeyote anaye uwezo wa kuoa basi aoe kwani hii ni bora kuhifadhi tupu na kulinda macho, ama asiye uwezo huu basi hutakiwa kufunga saumu kwani ni himaya yake kutokana na makosa

Waarabu walitambua umuhimu wa kuunda familiya kwa jamii, umma na staarabu, wakaona kuwa kuangamiza familiya ni sababu ya kuuangamiza ustaarabu mzima. Mmoja wa wataalamu wa masuala ya mashariki (Mustashrikin) alisema: ukitaka kuangamiza ustaarabu wa umma wowote basi unatakiwa kuangamiza mambo matatu: familiya, elimu na mifano bora yaani viongozi, na kwa kuangamiza familiya unatakiwa kuathiria nafasi ya mama na ukitaka kuangamiza elimu basi unatakiwa kuathiria nafasi ya mwalimu na kumfanya adharauliwa na kupuuzwa na wanafunzi wake na kwa kuangamiza viongozi na mifano bora unatakiwa kupuuza na kuchafua nafasi ya wataalamu na wazazi mpaka wakawa hawafuatwi na yetote.

Kwa hakika, mama ana nafasi kubwa sana kuwatunza watoto na kuwalea kuanzia kujifungua mpaka mwisho wa maisha yake au yao, huchangia kwa kiasi kikubwa kuunda tabia yao na mwenendo wao, ambapo wakati baba huwa ameshughlikiwa na kazi na kupata hela za kuendesha maisha ya familiya yake, mama huwa na majukumu ya kuwalea watoto na kuwapa mafunzo yaliyo muhimu zaidi kuliko mafunzo ya kusoma na kuandika, baba akipatwa na shida ya ukosefu wa kazi au uhaba wa ujira familiya wanateseka lakini siyo kama wakikosa malezi na utunzi wa lazima kutoka kwa mama.

Inafahamika kuwa mama ni mfano wa kuigizwa wa kwanza kwa watoto, kwa maana yeye ndiye dira ya kuainisha mwelekeo wa watoto akiwa bora hivyo ndivyo huwa watoto ama akiwa mbaya basi watoto hawana budi kumfuata kama ilivyokuja katika kisa cha mtu aliyezoea wizi akakamatwa na kupelekwa mahakamani ili apate adhabu ya wizi akaomba mamake aje ili ambusu, mama alipokuja akamumiza vibaya na alipoulizwa juu ya sababu ya kitendo chake hiki, alijibu: aliniona nikiiba yai utotoni mwangu bila ya kunikataza au kunifahamisha kuwa wizi ni kitendo kibaya mpaka nikafika kiwango hiki cha wizi na uhalifu.

Kwa hiyo, mama akifanya uzembe kuhusu majukumu yake ya malezi huwa sababu kubwa ya kuharibu watoto wake bali kizazi kizima na kupotezwa kwao. Hali hii haimaanishi kuwa mama anahusika peke yake juu ya malezi, hapana bali baba pia ana majukumu yake kuwaelekeza na kufuatilia watoto wake na kuwapa nyasia na mashauri. Jambo lililosisitizwa na Mtume (S.A.W.) kuwa wazazi wana majukumu ya kusimamia familiya pamoja, yaani baba na mama kila mmoja huwa na wajibu maalumu na wanatakiwa kushirikiana na kusaidiana kufanikisha mradi wao ambao muhimu zaidi kuliko katika maisha yao.

Mtume (S.A.W.) ameelezea kuwa wanandoa wako sawa sawa kuhusu majukumu na wajibu wanaotakiwa kuzingatia, ambapo alibainisha kuwa kila mmoja ni mtawala katika majukumu yake na kwamba kila mmoja ataulizwa na kuhesabiwa kwa mujibu wa majukumu ya utawala wake huu. Mtume alisema: “Kila mmoja wenu ni mtawala na ana majukumu juu ya walio chini yake, ambapo kiongozi ni mtawala atakaeulizwa kuhusu watawaliwa wake, na mwanamume katika nyumba yake ni mtawala na ataulizwa kuhusu watawaliwa wake ambao ni jamaa zake, na mwanamke pia ni mtawala wa nyumba ya mumewe na watoto wake na ataulizwa kuhusu watawaliwa hawa, na hata mtumishi ni mtawala wa mali na kazi ya bwana wake na ataulizwa kuhusu watawaliwa wake, kwa kweli nyote ni watawala na mtaulizwa kuhusu raia wenu” na katika hadithi nyingine: “Kwa hakika Mwenyezi Mungu Atamwuliza kila mmoja kuhusu majukumu yake, ameyatekeleza au ameyapoteza?! Mpaka mtu ataulizwa kuhusu jamaa zake”.

 

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.