Suala la kipalestina na Ukandamizaji wa kielektroniki… Facebook kama ni mfano

Imeandaliwa na Kitengo cha Utafiti .. Imetafsiriwa na Bw. Farid Mohammed Farid

  • | Saturday, 18 November, 2023
Suala la kipalestina na Ukandamizaji wa kielektroniki… Facebook  kama ni mfano

Je, mitandao ya kijamii inafanikiwa kunyamazisha midomo na kufunga mikono?

Kwenye Tarehe ya 7 Oktoba 2023, nguvu kinzi ya kipalestina “Hamas” ilianzisha opersheni kubwa ya kijeshi inayoitwa (Mafuriko ya Al-Aqsa) dhidi ya utawala wa Kizayuni, ambapo Kwa mara ya kwanza katika historia ya ukinzani wa kipalestina, ilijumuisha mashambulizi ya ardhini, baharini na angani kwenye vitongoji kadhaa vya Ukanda wa Gaza. Operesheni hizi zilivutia mshikamano wa maoni ya umma pamoja ya ndugu wetu wa  Palestina dhidi ya ukiukwaji wa kila siku, ulioongezeka sana baada ya kuundwa kwa serikali ya Kizayuni ya hivi sasa yenye msimamo mkali zaidi inayoongozwa na “Benjamin Netanyahu” mwanzoni mwa mwaka huu.

Njia za usaidizi wa ummati zilitofautiana na kujumuisha usambazaji wa maposti (Machapisho),makala, picha na video za shambulio kali  dhidi ya wasio na hatia ndani mwa ukanda wa Gaza, kwenye mitandao ya kijamii kama vile (Facebook) wakitamani kufika kwake kwa idadi kubwa ya watu duniani,  Na kupata huruma na kuunga mkono zaidi, kwa ajili ya kuushinikiza utawala wa Kizayuni, na Kusitisha mapigano, na kuepuka sera ya adhabu ya pamoja. Hivyo, mitandao ya kijamii yamegeuka kuwa vyombo mbadala vya habari kwa vile vya kimagharibi vinavyopendelea upande wa Kizayuni.

Lakini ilidhihirika wazi kwamba msimamo wa kampuni mhusika ya Facebook hautofautiani na vyombo vya habari vya kimagharibi, ambapo unaficha ukweli na kusambaza hadithi na uongo za kizayuni dhidi ya maisha ya mamilioni ya wanawake, watoto na  wasio na hatia wa Kipalestina, Kwa kufuta maposti (Machapisho) yanayounga mkono haki ya ukinzani dhidi ya uvamizi, na kufichua ukiukaji wa mara kwa mara wa kizayuni dhidi ya raia wasio na hatia, na kuzuia ufikiaji kwake, Na kuzuia makala na habari zote zinazoshughulikia suala hilo, na kuonya wamiliki wa maposti hayo kuendelea kuunga mkono suala hilo, bali inawapiga marufuku ikiwa ni lazima, ni sera ya kimfumo na ukiukaji wazi wa kile ambacho nchi za Magharibi huitaka katika suala la uhuru wa kujieleza na uhuru wa maoni

Kwa mfano; Mwanaharakati mmoja alirushia (post) ambalo halikuwa na ukiukaji au uhalifu wowote, haliungi mkono kikundi mahususi, halichochei vurugu au mapigano, ingawa na hayo wahusika wa Facebook walilizingatia ukiukaji wa vigezo vya jamii na kuliainisha ni hatari kwa vikundi na watu binafsi; Kwa hoja kwamba lina neno "Tel Aviv" na maneno mengine ambayo algorithms ya Facebook inayatambua na  kuyapiga marufuku. Kuna mifano mingi na hakuna nafasi ya kutosha ya kuihesabu na kuitaja. Lakini mgogoro halisi wa kimaadili unaofichua vigezo vya undumakuwili, kwamba idara ya jukwaa haikutosheleza kufuta au kuzuia machapisho yanayounga mkono upande wa Palestina tu, bali ulijitahidi kueneza mada zenye kuunga mkono utawala wa Kizayuni, kupitia kueneza kampeni za matangazo zinazofadhiliwa na zinazotakia ama kusitisha kwa kile unachokiita (shughuli za kupambana na kizayuni), zikiambatana na picha na kanda za video za hali ya hofu inayowakabili raia wa Kizayuni, au kuanzisha kurasa bandia za kizayuni zinazoungwa mkono na idadi kubwa ya wanachama bila ya kufichua utambulisho wa wanachama hawa; ambapo huonekana mbele ya jamii za Magharibi kama kurasa za Kizayuni zinazoungwa mkono na Waarabu dhidi ya suala lya Palestina.

Mwishoni, sera ya ukurugenzi wa mitandao ya kijamii, miongoni mwake Facebook, katika kusaidia utawala wa Kizayuni kielektroniki na katika vyombo vya habari, ndiyo ushahidi wa utofauti wa nyanja za vita vya hivi sasa dhidi ya ukanda wa Gaza, ikiwa ni vya uwanjani, ambavyo vinapuuza vigezo na sheria zote za kimataifa zinazohusiana na haki za binadamu, na vya kisaikolojia vinavyotumia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kama zana ya kughushi ukweli na kuficha ukiukaji unaotekelezwa na utawala ya uporaji. Hilo si jambo jipya, Daima  wale wametakia uhuru wa maoni na kujieleza, nao ndio wa kwanza kuuvunja kwa maslahi yao wenyewe, Hawatakiwi kuunga mkono suala la Palestina, Au kuunga mkono haki za watu wa Palestina ambao haki yao ya kurejesha ardhi zao zilizokaliwa kwa mabavu, bali, wanachotakiwa kuyafanya ni kuacha nafasi kwa kila mtu ambaye anataka kutoa maoni yake bila kuzuiwa, kufutwa, au kupigwa marufuku,  Lakini wao ni woga zaidi kuruhusu kalamu ziandike kwa uhuru, au midomo iseme ukweli.

 

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.